Pamoja na Katiba Mpya Kenya, Polisi wapiga marufuku Maandamano. CHADEMA jifunzeni kitu Hapo!

Tunavyoiendea Katiba Mpya tujifunze kwa wenzetu waliotangulia kuzipata ili ya kwetu iwe bora zaidi

Mfano hapo Kenya pamoja na Katiba Mpya bado polisi wamezuia Maandamano ya kesho sasa Wana tofauti gani na Tanzania yenye Katiba ya zamani!!

Mlale unono!
Katiba mpya ya kweli ni wananchi wengi wa Tanzania kuwa na elimu nzuri na uelewa wa haki zao. Acha Kenya hata huko Marekani na katiba yao bado Sheria hizo hizo zinampendelea mzungu na kumkandamiza mmarekani mweusi hadi aingie barabarani. In short suala siyo tu katiba bali jamii.
Jamii ikihitaji maandamano au mikutano ya siasa ITAFANYIKA TU hata kama katiba inakataa. Nchii hii ina watu zaidi ya milioni 60 unadhani majeshi yasiofika hata milioni 1 watawafanya nini wakiamua kupinga kitu.
 
Tunavyoiendea Katiba Mpya tujifunze kwa wenzetu waliotangulia kuzipata ili ya kwetu iwe bora zaidi

Mfano hapo Kenya pamoja na Katiba Mpya bado polisi wamezuia Maandamano ya kesho sasa Wana tofauti gani na Tanzania yenye Katiba ya zamani!!

Mlale unono!
Kwani Katiba Mpya ni kwa ajili ya Chadema tu? Kama nchi inaongozwa vizuri maandamano ya nini tena? Jo wewe unaiwaza Chadema tu 24/7.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Tunavyoiendea Katiba Mpya tujifunze kwa wenzetu waliotangulia kuzipata ili ya kwetu iwe bora zaidi

Mfano hapo Kenya pamoja na Katiba Mpya bado polisi wamezuia Maandamano ya kesho sasa Wana tofauti gani na Tanzania yenye Katiba ya zamani!!

Mlale unono!
[/QUOTE
Ni kujitoa ufahamu tu; hii mifumo ya kikatiba, siasa na demokrasia siyo universal. Kila nchi ina historia yake. Pili, duniani kote hata huko wanakoamini kuna demokrasia ya juu hakuna uhuru wa siasa za uasi. Maelfu ya watu mnataka kwenda Ikulu kufanyaje? Wajifunze pia maandamano kuelekea Capitol Hill, US mbona hadi leo jinai inaendelea! Development as freedom; siyo kutumia uhuru kufanya jinai bali ni kutumia uhuru kuleta maendeleo kiuchumi, kijamii, kisiasa na kuwa huru kufikiri chanya. 🙏🙏🙏
 
Tunataka katiba mpya ila tunatazama sana kwenye kutupa uhuru wa kusiasa zaidi.
 
Hakuna Cha tofauti Mzee, principal ni zile zile na wanaosimamia utekelezaji ni watu Hawa Hawa wa Leo na kesho wanaotaka madaraka na pesa..

Don't exaggerate mambo au kuwa na matumaini makuubwa ambayo hayawezi tokea.
Huoni katiba katiba mpya inamuwajibisha mtu aliyeivunja hata atakapotoka madarakani?

Hii iliyopo mtu hawajibishwi hata atakapotoka madarakani. Huoni hilo kama ni tatizo?

Katiba mpya na imara inamfanya mtu anayetaka kuivunja ajitafakari mara mbili mbili endapo atakuwa nje ya mamlaka nini kitamtokea?

Katiba mpya ni mwarobaini wa mambo mengi ya nchi unless kama hujasoma masuala ya constitutional law huwezi kuelewa namna gani ubovu ama uimara wa katiba unavyoweza kubadilisha ustawi wa nchi ama kuididimiza nchi.
 
Inamuwajibishaje? Hata hii ya Sasa ukitoa Kinga inawajibisha tuu
 
Bob aliwaambia kuwa na Katiba Mpya ni jambo Moja na kuitekeleza ni jambo jingine..

Mfano Rais anamiliki Central Intelligence Unit ambao huwezi kuwajua akitaka kumshinikiza Spika au Jaji anaweza na ushahidi hakuna maana anawatumia hao hao Jamaa kuwatisha hawataki wanakufa kweli..

Mpaka hapo Katiba zenu zinakuwa zimewasaidia nini?
Kumbe angalau atatumia mbinu ya siri kabisa kuliko kuwa na katiba mbovu ambayo atafanya atakavyo hadharani.

Basi bado hitaji la katiba mpya ni muhimu sana kwa muktadha huo.

Waulize wanaopinga katiba mpya wanahofia nini ndo utajua umuhimu wake.
 
Hakuna anayefanyaga hadharani
 
Hakuna anayefanyaga hadharani
Rais kumwagiza Spika awafukuze wabunge wa upinzani bungeni wanaotoa hoja za kui challenge serikali ili awashughulikie na Spika akatii maagizo huoni ni ubovu wa katiba usioupa nguvu kamili muhimili wa mahakama?
 
Kwani ni kosa la Rais? Yeye Spika hajui majukumu yake?
 
Hakuna anayefanyaga hadharani
Rais kuupangia muhimili wa mahakama kwamba majaji hakuna kusafiri nje ya nchi kwenye likizo zao halali tena anatamka hadharani huoni ni ubovu wa katiba ndo mwanya wa kuagiza yote haya?

Mihimili mitatu ya nchi haiingiliani kimajukumu wala kimamlaka kwa katiba zilizo bora isipokuwa pale panapokuwa na dhana ya kikatiba ya "check and balance"
 
Kwani ni kosa la Rais? Yeye Spika hajui majukumu yake?
Rais aliyasema hayo alipoona kuna mwanya wa yeye kusema hivyo na hakuna wajibu wa katiba unaombana.

Inaonekana wewe ni layman kwenye masuala ya katiba na sheria za nchi hii.

Katiba hii ina mapungufu makubwa mno hadi unajiuliza walioitunga walikuwa na elimu walau darasa la saba tu?

Rais amepewa madaraka na kinga hadi ya kutoshtakiwa kwa makosa ya jinai yoyote aliyofanya ama atakayofanya akiwa madarakani.

Je, hadi hapo huoni ni mwanya wa kufanya atakavyo hata kama anavunja haki za binadamu kwa maksudi?

Wewe unahitaji kupewa elimu kuhusu umuhimu wa katiba mpya na jinsi itakavyochangia kukuza pato la mtu mmoja mmoja na taifa kwa ukumla.
 
Visingizio
 
Kuwa kiongozi ni kuweka pamba masikioni, Kuvaa mawani isiyoona utu na thamani ya binadamu alafu kuchapa kazi ..
 
Back
Top Bottom