Pamoja na Katiba Mpya Kenya, Polisi wapiga marufuku Maandamano. CHADEMA jifunzeni kitu Hapo!

Hata chanzo cha maandamano yenyewe ni kupanda kwa gharama za maisha wakati makuwadi wa katiba mpya bongo wanaaminishi watu katiba mpya ni muarobaini.
 
Katiba nzuri + watu wenye uzalendo =100%
katiba nzuri + watu wenye njaa =hamna kitu mnatibu
Alafu kuna watanzania watu wasiojua wanataka nini katiba yenyewe mpaka waombewe na wanasiasa hata hii ya sasa inavunjwa hakuna mtu anashugulika nayo wala kujali wasio taka kusumbuka na matatizo ya nchi yao kila kitu wao n sawa hata ije katiba mpya kwa hii nchi watafaidi wanasiasa tu
 
Punguza ujinga.Kama hujui faida ya katiba bora wewe huna faida yoyote duniani.
 
Mimi naamini kabisa tunahitaji Katiba Mpya, ila Katiba Mpya sio kila kitu, nyie CHADEMA msiwaaminishe wafuasi wenu huo uongo.

CHADEMA karibu 90%+ wanafikiria Katiba Mpya itawapatia kila kitu, yaani itawapa

1: CHAKULA
2: MVUA
3: MAANDAMANO KILA SIKU
4: FEDHA
5: UONGOZI BORA SANA
6: UTAJIRI MKUBWA
7: UHURU WA KILA KITU
8: KUFANYA WATAKAVYO
9: KUAGA UMASKINI
10: KUWA NCHI YA MAZIWA NA ASALI.

Hivi CHADEMA, mmechanganyikiwa nn? Katiba Mpya mkipata nyie mnajua ndio kila kitu ndio KITAKUJA TOKA WAPI SIJUI, AU MKAJUA VITU VITAKUJA TOKA MBINGUNI BURE BURE TU.

CHADEMA, acheni kuwaaminisha wafuasi wenu kuwa Katiba Mpya ndio kila kitu, sio kweli, hapana, Katiba ni Sheria tu kama nyingine, unaweza kuwa na Katiba nzuri sana, ila shida na matatizo, njaa, umaskini, rushwa, ujinga na elimu mbovu sana iko pale pale..!!
 
Mbona Nchi nyingi hazina hizo Katiba Mpya na mambo ni bambam?

Egypt Ina Katiba kama hizo zenu? Kipi mnaizidi?China Je?

Acha upuuzi wako
Wewe ndo uache ujinga.unadhani hizo nchi zimeshushwa toka mbinguni zikawa hivyo zilivyo.Ukiona jambo zuri jua halikuja kama ndoto,kuna watu walilipambania.wewe kama hauko kwenye kundi la watu wakuliweka hili taifa lije kua mfano uko mbele kama ambavyo unatoa mifano kwa nchi zingine kaa utulie wenye akili wafanye.
 
Ilo unasema wewe.Acha kuweka mawazo yako kwenye vichwa vya watu wengine ambani ni smart kuliko wewe.
 
Tofauti ni kubwa sana , kwani Zanzibar bado imekaliwa kwa mabavu na Tanganyika
 
Mkuu Yohane,
Dikteta hata ungeweka msaafu na Bibilia, udikteta haumtoki.
Ujifunze na wewe kitu hapo
 

Umeona leo? Wameenda mahakamani kupata katazo, mahakama ikagoma.... Be informed before display your ignorance
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…