Pamoja na kipigo chote hicho, jeshi la Marekani lasema halitaweza kuwazuia Houth kwa njia ya vita.laomba itafutwe njia mbadala kupambana nao.

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Tamko la aina hiyo limeshatolewa huko nyuma na makamanda wa jeshi la Marekani na ikaonekana kama ni utani.Kwa mara nyengine limetolewa na kamanda mkuu wa vikosi vya wanamaji wa Marekani eneo la mashariki ya kati,vice admiral George Wikoff.
Katika hoja zake kamanda huyo amekumbusha kuwa vikosi vya Houth vimeshashambuliwa kwa nguvu kwa takriban miezi 10 lakini bado vikosi hivyo vina uwezo wa kuendelea kuzishambulia meli za kibiashara na za kimarekani zinazopita kwenye bahari yao.
Kauli hiyo imetolewa mara baada ya kurejea kwa kasi kwa mashambulizi ya Houth katika wiki hii ikiwa ni wiki ya tatu tangu vikosi vya Israel vilipoishambulia bandari ya Hodeada inayodhibitiwa na wanamgambo wa Houth
Katika tahadhari zake vice admiral Wikoff,amesema jeshi hilo limetumia zana nzito kupambana na silaha nyepesi za Houth kama vile droni za pigo moja na droni za baharini lakini bado wameshindwa kuzizuia silaha hizo na kutoa hakikisho la usalama kwa meli zinazopita bahari nyekundu na ile ya Yemen.
Kuonesha ugumu wa kupambana na Houth kiongozi huyo wa ngazi za juu wa jeshi la Marekani amesema jukumu la kupambana na Houth ni la ulimwengu wote kwani kila nchi ina maslahi yanayohusiana na eneo hilo.

The US Navy says it can't stop the Houthi attacks on shipping with force alone

 
Sawa bwana vice adriral George wikoff
 
Ninakataa kuambiwa kwamba WAZUNGU Wana huruma,mengine yote ni sawa mkuu.
 
America wanaficha juzi Al Houth waliripua carriers mbili za US.
 
Wayemen wengi hawawapendi Wahouthi kinachotakiwa ni msaada tu ili wawaondoe hao Puppets wa Ayatolah.
Saud Arabia, US, Israel, UAE, Morocco, Jordan, Egypt, Pakistan, Baharain, Sudan na Wayemen wa South walishindwa vita, labda nendeni wanajeshi mlio stafu na mizinga ya saba saba hio mitatu mlio nayo JWTZ 😄
 
Saud Arabia, US, Israel, UAE, Morocco, Jordan, Egypt, Pakistan, Baharain, Sudan na Wayemen wa South walishindwa vita, labda nendeni wanajeshi mlio stafu na mizinga ya saba saba hio mitatu mlio nayo JWTZ 😄
Sasa hivi ndio wamejiongezea Maadui Serious ngoja uone.
 
Waarabu wa Yemeni wa kabila la Jurhum ndiyo walioishi na Ishmael Mhebrania wa kutoka huko canaan wakamfundisha lugha ya kiarabu na kumfanya mwarabu "culturally" na kisha wakaanzisha civilization pale Makka ambayo ipo mpaka leo!
 
Wakati tunawaambia kama houthi hawawezi kupigwa wakabisha
Americant bila ya kutumia Nyuklia haitoboi sehemu
Nahapo bado imeshirikiana na mashoga wenzie
 
Saud Arabia, US, Israel, UAE, Morocco, Jordan, Egypt, Pakistan, Baharain, Sudan na Wayemen wa South walishindwa vita, labda nendeni wanajeshi mlio stafu na mizinga ya saba saba hio mitatu mlio nayo JWTZ 😄
Na kila unyama wa Israel unavyoongezeka kuna uwezekano mkubwa Houth kuanza kusaidiwa na jirani yao Oman.
Na Oman hiyo hiyo imewahi kuzuia silaha zilizokuwa zikipelekwa kwa wapinzani wa Houth ili kuchochea machafuko zaidi ndani ya Yemen.
Hapo sasa ndio vita vitapanuka na kuongeza nguvu zaidi za Houth
 
Kila kitu kinawezekana na point yako nakubaliana nayo 💯
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…