CHAGOSI GERALD
Senior Member
- Jan 25, 2020
- 162
- 286
MSOMI: MASHINE YA KIWANDA AU ROHO INAYOKIMBA?
Huyu msomi! Huyu anayejivunia degree yake, akajilaumu kwa mshahara wa laki tano! Je, tuseme kweli: yeye si kiumbe, yeye ni mashine iliyotengenezwa na mfumo, iliyopachikwa akili ya urobot, imewekwa kwenye mtandao wa minyororo isiyoonekana, ili kuzungusha dhana ya heshima kwa ajili ya bosi wake!
Anajua nini? Anajua kwamba kwa siku, yeye na degree yake wanatengeneza elfu kumi na sita⦠Lakini akili yake, roho yake, ubunifu wake, wamepotea. Amechagua kuwa cheap labour. Uvivu wa kulima shamba lake mwenyewe, kuunda, kuzalisha thamani ya kweli, umemfanya awe mtumwa wa hofu, mtumwa wa mshahara, mtumwa wa muda wake wenyewe!
Hapa ndipo ukweli wa kibinadamu unaibuka: hakuna kitu kinachokufa polepole zaidi kuliko msomi anayekubali kuuza utu wake. Anatumikishwa polepole, akichinjwa mdogo mdogo, kamwe asielewe kwamba kila kipande cha akili yake ni mashamba yasiyolimwa.
Lakini tukio la karne ya 18 na 19 linatufundisha: wafanyakazi walipoamka, walipigana, walijitambua. Umoja wao ulikuwa uchungu wa mwanga dhidi ya giza la mashine. Hivyo basi, wasomi wasio na umoja ni kama wanyama waliokatwa sehemu moja moja, huku wakiwa na shamba zuri la akili lakini bila uwezo wa kulimwa pamoja.
Na kweli, ni uvivu tu! Uvivu wa kulima, uvivu wa kudhani kwamba mshahara ni heshima, uvivu wa kudhani kuwa degree ni mali ya kuuzwa. Msomi aliye ELIMIKA haambiwi hivyo; anaona: msomi ni mashine, na mashine inapaswa kuchukuliwa ama ukaijenga upya, ama utaishia kama kidogo kidogo kilichokatwa na mfumo.
Je, utabaki kupumua kimya, ukikubali uharibifu wa utu wako? Ama utaamka, ukaweka akili yako kama moto, ukaungana na wenzao, ukaamua: Hapa hakuna cheap labour tena. Hapa tunalima mashamba yetu, tunaunda thamani yetu, tunapiga kelele dhidi ya mashine ya mfumo!