Pamoja na kupanda bei, nyama ndiyo bidhaa inayonunuliwa zaidi

Iwensanto

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2019
Posts
1,228
Reaction score
1,157
Habari wana jamvi katika utafiti wangu bao siyo rasmi nyama imeendelea kuwa ni bidhaa inayonunuliwa kwa wingi.

Tafiti inaonesha kuwa matumizi ya mboga ya nyama yamezidi kwa sababu ni mboga ambayo maandalizi yake hayana gharama kubwa.

Watu wenye kipato cha wanaweza wakanunua nyama robo kilo na ikawatosheleza kwa milo 2 tofauti na mboga nyingine.

Nini maoni yenu wanajamvi.
 
Daah,Kuna mahali unakuta nyama Bei ghali Sana lakini bado tu ukichelewa kidogo tayari imeisha na ni mitaani tu ambapo ni choka mbaya...
 
Yaani huko mitaani sasa hivi ikifika saa 11 mpaka 12 mabucha hayana nyama
Daah,Kuna mahali unakuta nyama Bei ghali Sana lakini bado tu ukichelewa kidogo tayari imeisha na ni mitaani tu ambapo ni choka mbaya...
 
Kinachofanyika kunawekwa viongo vingi ili mradi watu kama wale wanaokula ugali kwa papa
Sababu robo kilo ya nyama inaweza kutoa mchuzi wa kutosha familia kubwa kwa ajili ya kulia Ugali na watu wakashiba kisawasawa, kila mtu anapewa kakipande kidogo tu cha nyama, ili kusindikiza mchuzi mwingi
 
Ndio furaha ya CCM na matajiri wachache wanafurahi watanzania wakiishi kwa ufukara na kubahatisha bahatisha kama hivi. Na wanafurahi Sana hali hii iendelee.
 
Nadhani wafanya biashara wanajipanga pia watu wa visiwani kama Ngazija wananunua ng'ombe wangi kutoka huku
 
Sio kwa kula nyumbani labda kwa mama ntilie na ma hotelini.
 
Hata nyumbani gharama za kuaandaa nyama ni ndogo
 
Habari wana jamvi katika utafiti wangu bao siyo rasmi nyama imeendelea kuwa ni bidhaa inayonunuliwa kwa wingi.

Tafiti inaonesha kuwa matumizi ya mboga ya nyama yamezidi kwa sababu ni mboga ambayo maandalizi yake hayana gharama kubwa.

Watu wenye kipato cha wanaweza wakanunua nyama robo kilo na ikawatosheleza kwa milo 2 tofauti na mboga nyingine.

Nini maoni yenu wanajamvi.
INATEGEMEA SEHEMU NA SEHEMU

Halafu kafanye utafiti wako uwe rasmi
 
Back
Top Bottom