Pamoja na kusemekana ni mkoa wa kihalifu, Ni kwanini kuna matukio machache ya uhalifu Mara.

Pamoja na kusemekana ni mkoa wa kihalifu, Ni kwanini kuna matukio machache ya uhalifu Mara.

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
1713034911724.png

Tunasikia tu story kwamba Mara hakukaliki ni mkoa wa matukio kuuana, ujambazi, kupigana, n.k

Kuna picha zimetengenezwa za vibao vimeandikwa "sasa unaingia mkoa wa Mara" yameongezwa maneno, "kaza roho", "be strong", n.k. yanaleta picha kwamba ni mkoa wa matukio

Kwanini ni tofauti na uhalisia ?

Habari kibao za matukio haya tunazisikia Geita, Arusha, Manyara, n.k.
 
Enzi hizo walifanikiwa kuaminisha wengi huo uongo na ikapelekea wakajazana sana jeshini, kumbe ni waoga tu hakuna lolote.
 
Siku hizi wameweka mapanga chini, wamekuja mjini wanauza mayai....
kuuza mayai ni biashara halali kabisa, ni kinyume na story zinazosambaa kwamba ni wezi.

Hii biashara mwanzoni nilikuwa naichukulia poa ila nimekuja kugundua ina pesa, watu wanajenga, kununua magari, kusomesha watoto private, n.k.
 
Mtoa mada umewahi kuishi Mara? Wewe unataka matukio unayosikia Geita sijui mama kamuua binti yake? Hayo huyapati Mara. Huku ni ugomvi kidogo mtu kakimbilia silaha kakuramba kidogo. Matukio ya ugomvi wa namna hii mtu anaenda Hospital kupata PF3 yanaishia polisi,hayo ya Geita ndio yanaishia kwenye Media.
 
Tupo kizazi cha kidijitali, hizi simu zetu ni media tayari.

Matukio yakiwa ya kutokea mara kwa mara sehemu flani yana kawaida ya kuanza kupata attention hata kwenye media kubwa
 
View attachment 2962630

Tunasikia tu story kwamba Mara hakukaliki ni mkoa wa matukio kuuana, ujambazi, kupigana, n.k

Kuna picha imetengenezwa ya kibao "sasa unaingia mkoa wa Mara" yameongezwa maneno, "kaza roho", "be strong", n.k. yanaleta picha kwamba ni mkoa wa matukio

Kwanini ni tofauti na uhalisia ?

Habari kibao za matukio haya tunazisikia Geita, Arusha, Manyara, n.k.
Hakuna kibao chenye maneno hayo popote Tanganyika hii.
Kama kiliwahi kuwepo,je ni nani mwenye mamlaka ya kuandika na kuweka vibao hivyo hapa Tanganyika?

Waache kutuchafua sisi watu tunaojua kusimamia tunacho kiamini kwa uthabiti.
 
Mara sio mkoa wa kiharifu kwa maana ya uporaji na ujambazi bali ni mkoa wenye matukio ya kikatili kwenye sababu za kipuuzi....... imagine mtu anamkata mkewe mkono eti kwa kuwa amechelewa kurudi kisimani.......mtu anamuua mkewe eti kwa kuwa amemnyima muumba.......

Mtu amemuua mwanae wa kumzaa kisa ili apate michango ili alipie mikopo yake

Nadhani hata huko kungetakjws kujengwa hospital ya watu wa matatizo ya akili.......
 
Lakini haya matukio tunayasikia zaidi mikoa mingine

mfano mwaka huu Njombe huko mtu kaua mke wake kwa kunyimwa unyumba

Si wanaimba Hadi Taarabu siku hizi..
Aisha mashauzi si anaitwa Bhoke..ni mkurya nasikia...

Tanzania inabadilika haraka Sana ..nasikia kuna waimba Taarabu Hadi wachaga
Ni mwendo wa maokoto
 
Mkoa wa Mara unayo makabila maarufu kama:-
-Wakurya
-Wazanaki
-Wajaluo
-Wajita
-Wasimbiti
-Wakwaya
-Wakiroba
Na makabila mengineyo ambayo sio maarufu sana.

Kati ya hayo makabila mengi yaliyopo mkoa wa Mara ni kabila moja tu la wakurya ndilo kabila linalosifika kuwa na watu wenye hasira kali. Hawa watu ni watu wastarabu sana kama hutawachokoza. (Kosa unaloliona dogo, yeye anaweza kuliona kubwa na kufanya maamuzi magumu)

Hayo makabila mengine yote yaliyosalia hayana hizo mambo za kukatana mapanga.
 
Back
Top Bottom