Pamoja na kushusha bei wananipita wanaenda kwingine, najiuliza nakosea wapi?

Pamoja na kushusha bei wananipita wanaenda kwingine, najiuliza nakosea wapi?

Mjue mshindani wako nje ndani ikiwezekana mtume mtu wako wakaribu ambaye anaweza kukupa taarifa kamili yaani aende pale akanunue kwa huyo mshindani wako akupe full information kwanzia alivyohudumiwa had anaondoka na pia uone tofauti ya bidhaa yako na yake . Pili jua wateja wake haris ni watu wa aina gani kwan biashara nyingi huwa kwanza ina target customers na wengine ndio watafata .jua weakness na strength zake the go beyond.
 
Wakuu tangu nifungue biashara yangu ni wiki Sasa. Mazingira na miundombinu ya hapo ninapofanyia biashara yapo vizuri ila cha ajabu siuzi vile inavyotakiwa.

Yaani mtu anakuja anauliza kidali Tsh ngapi unamwambia bei anakigeuza geuza wee anakitathmini halafu anasema anarudi ndo imeisha hiyo. Nikasema ngoja nishushe bei miguu niuze 100 ila wananipita wanaenda kwingine!

Najiuliza nakosea wapi ila sioni kama Mungu namuomba Kila siku Kila muda hata nikiwa naweka kuku kwenye mafuta naomba pia ila wapi
Vumilia kila kitu kitakuwa sawa
 
Mjue mshindani wako nje ndani ikiwezekana mtume mtu wako wakaribu ambaye anaweza kukupa taarifa kamili yaani aende pale akanunue kwa huyo mshindani wako akupe full information kwanzia alivyohudumiwa had anaondoka na pia uone tofauti ya bidhaa yako na yake . Pili jua wateja wake haris ni watu wa aina gani kwan biashara nyingi huwa kwanza ina target customers na wengine ndio watafata .jua weakness na strength zake the go beyond.
Sawa mkuu ntalifanyia kazi
 
Biashara zinahitaji uvumilivu sana, usione watu wanafanya biashara kila siku ukadhani ni rahisi, hapana biashara inahitaji moyo na kuwa na matumaini.

Tena kwa aina ya bishara unayoifanya wewe ndio kabisaa, kwa sababu inaharibika, ila usikate tamaa komaa
 
Ngoja nikuelezee alichokimaanisha.
Yaani amemaanisha kwenye biashara ukiachilia mbali ubora wa bidhaa na bei kuna mambo mengine ya ziada.
Mambo hayo ya ziada hutofautiana kila mtu huwa ana mbinu zake au mambo yake ya ziada tofauti ya kumchota mteja ili asimsahau,akili za mteja zipo kama akili za mtoto mdogo vile unavyomzoesha kitu fulani basi atataka aendelee hivyohivyo na hataki kingine.
Hapa ndio kunaingia mambo ya ucheshi,kutoa ofa/zawadi/nyongeza,kutengeneza kachumbari tamu,buni mbinu zako binafsi za kumchota akili mteja na baada ya miezi kadhaa wanakuzoea na hawatataka kwenda kwa mwingine.
Hujawahi kuona baadhi ya wauzaji wa maduka/duka la Mangi au Mgahawa kwa nje anaweka TV watu waangalie bure ile ni mbinu mojawapo ili wateja wasimsahau iwe muda wote wanawaza kwenda kwake.
Kwa hiyo vumilia ndugu wiki moja ni ndogo mno kuitathmini biashara unatakiwa upambane angalau miezi 6 ili uwe na wateja wako na wewe
Mimi nina miezi 3 naona jau siuzi wananipita tu
 
Wateja wanaenda kwa wahudumu waliowazoea vumilia nawewe watakuzoea huwa kunakuwa na kamlolongo hadi uzoeleke kikubwa uwe mcheshi

1. Mtu anapita anakuona unauza kuku ila atapita maana hakujui ataenda sehemu anapomjua muuzaji

2. Siku yule muuzaji wake kafunga atakuja kwa kujishauri utakuta anaona unauza kuku ila anaweza kukuuliza "hapa unauza kuku"

3. Ukimhudumia atapima huduma uliyompa(kumbuka hapa anapima urafiki na uchangamfu wako na ulivyojiweka karibu)

4. Kama umemhudumia tu ilimradi aende siku jamaa akifungua anarudi kulekule kwahiyo atakupita na kama ulimhudumia kama rafiki na kumsemesha na kujifanya kuwa karibu nae au mnafahamiana kesho akitaka kupita atajiuliza mwisho wa siku atakuja kwako

NB Biashara haina formula maalum wateja wengine hawatakagi story
 
Back
Top Bottom