Pamoja na kushusha bei wananipita wanaenda kwingine, najiuliza nakosea wapi?

Mjue mshindani wako nje ndani ikiwezekana mtume mtu wako wakaribu ambaye anaweza kukupa taarifa kamili yaani aende pale akanunue kwa huyo mshindani wako akupe full information kwanzia alivyohudumiwa had anaondoka na pia uone tofauti ya bidhaa yako na yake . Pili jua wateja wake haris ni watu wa aina gani kwan biashara nyingi huwa kwanza ina target customers na wengine ndio watafata .jua weakness na strength zake the go beyond.
 
Vumilia kila kitu kitakuwa sawa
 
Sawa mkuu ntalifanyia kazi
 
Biashara zinahitaji uvumilivu sana, usione watu wanafanya biashara kila siku ukadhani ni rahisi, hapana biashara inahitaji moyo na kuwa na matumaini.

Tena kwa aina ya bishara unayoifanya wewe ndio kabisaa, kwa sababu inaharibika, ila usikate tamaa komaa
 
Mimi nina miezi 3 naona jau siuzi wananipita tu
 
Wateja wanaenda kwa wahudumu waliowazoea vumilia nawewe watakuzoea huwa kunakuwa na kamlolongo hadi uzoeleke kikubwa uwe mcheshi

1. Mtu anapita anakuona unauza kuku ila atapita maana hakujui ataenda sehemu anapomjua muuzaji

2. Siku yule muuzaji wake kafunga atakuja kwa kujishauri utakuta anaona unauza kuku ila anaweza kukuuliza "hapa unauza kuku"

3. Ukimhudumia atapima huduma uliyompa(kumbuka hapa anapima urafiki na uchangamfu wako na ulivyojiweka karibu)

4. Kama umemhudumia tu ilimradi aende siku jamaa akifungua anarudi kulekule kwahiyo atakupita na kama ulimhudumia kama rafiki na kumsemesha na kujifanya kuwa karibu nae au mnafahamiana kesho akitaka kupita atajiuliza mwisho wa siku atakuja kwako

NB Biashara haina formula maalum wateja wengine hawatakagi story
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…