Changamoto yako ni "customer base" (wateja) ambayo inahitaji muda ili watu wakuamini.
Kama biashara yako ni nzuri, mazingira masafi, una kauli nzuri kwa wateja, una haiba/mvuto wa kibiashara (yaani namna unavyojiwekaweka) na unamtanguliza Mungu basi jua tatizo lako ni patience (uvumilivu wa muda).
Mimi leo asubuhi nimeenda buchani kununua nyama kwa muuzaji niliyemzoea kabisa, hapo mahali kuna mabucha mengi sana, nikamkuta jamaa anamuhudumia mtu aliyehitaji kilo za kutosha, nadhani atakuwa ni mtoa huduma za vyakula, au sherehe, ikanibidi nisubiri ingawa nilikuwa nina haraka, pamoja na kwamba nyama ya leo haikuwa nzuri kihivyo ila nilisubiri, so kilichonifanya nisubiri ni ule UTEJA.
Nilivyokuwa naondoka, nikaona kuna nyama nzuri mpaka nikaitamani kwenye mabucha mengine, nikajisemea moyoni tu kuwa nimenunua kwa sababu ya UTEJA but hakuwa na nyama nzuri, na nikasema siku nyingine nitakuwa naangalia kwanza nyama iliyopo.
Hii maana yake ni kwamba, hiyo siku nyingine nitakayokuwa naangalia kama atakuwa na mboga nzuri ni kwamba mteja unaweza mvuta kwa huduma zako tu.
So jipe muda kuna wateja wanaendelea kukuchunguza, na ukifanikiwa kumteka mmoja basi jua mtaa mzima watahamia hapo. JIPE MUDA