Pamoja na kushusha bei wananipita wanaenda kwingine, najiuliza nakosea wapi?

Pamoja na kushusha bei wananipita wanaenda kwingine, najiuliza nakosea wapi?

Jifanye zuzu, kuwa mpole na mwenye ukarimu tele.

Watu wanapenda kunyenyekewa na kuabudiwa... waite majina kama BOSS, MKUU, MAMA, MZEE WANGU.... n.k

Usikaze uso sana. Jilegeze, jibebishe, jidogoshe.

Mimi watu huwa wananiona kama kakijana kapumbavu kasicho na ufahamu, maana najishusha haswa nakuwa kama zezeta ila NAPIGA HELA MBAYA.

Kuna faida gani kujikweza? Kiburi kitakupa ugali??

Usiwabinulie wateja midomo wala kuinua sana uso unapoongea nao! Tena jifanye kama una aibu aibu hivi..... ongea kwa sauti ya chini....

Kuwa zezeta kabisa, GO LOW, STAY STUPID AND FOOLISH... waache wawe juu yako kisaikolojia huku ukiendelea kupiga pesa.

Cc: Lamomy Mbaga Jr Mzee wa kupambania Extrovert Poor Brain The Icebreaker fundi bishoo mshamba_hachekwi Kapeace Dejane Depal cocastic dronedrake
 
Jifanye zuzu, kuwa mpole na mwenye ukarimu tele.

Watu wanapenda kunyenyekewa na kuabudiwa... waite majina kama BOSS, MKUU, MAMA, MZEE WANGU.... n.k

Usikaze uso sana. Jilegeze, jibebishe, jidogoshe.

Mimi watu huwa wananiona kama kakijana kapumbavu kasicho na ufahamu, maana najishusha haswa nakuwa kama zezeta ila NAPIGA HELA MBAYA.

Kuna faida gani ya kujikweza? Kiburi kitakupa ugali??

Kuwa zezeta kabisa, GO LOW, STAY STUPID AND FOOLISH... waache wawe juu yako kisaikolojia huku ukiendelea kupiga pesa.
Sawa bichwa komwe nimekuelewa
 
Usiwaze sana.Ni jambo la la kawaida kwani wateja wengi Wana tabia ya kikariri eneo moja.We endelea kukonaa hivyo hivyo utapata wateja wako wapya na ukiwapata waboreshee huduma hadi wakakutangaze
 
Komaa muda utaongea wenyewe pia zingatia
1.Nidhamu yako
2.costomer care yako
3.ubunifu wako
4.saikojilia ya mteja(msome mteja haraka kabla yake)
5.UVUMILIVU...
Mwisho kuwa mafia wasome wanaofanya biashara kama yako nje ndani.
 
Ukute story zina sambaa una uza ata mizoga ..uchawi sio lazima kuroga ata maneno tu
 
unafanya biashara sahihi eneo sahihi lakini kuna namna unakosea ambapo naamini mazingira yako yatakua yanakuangusha.

Kushusha bei si sababu ya watu kununua bidhaa yako (hii sio mbinu nzuri)

badilika Zingatia mazingira ya bidhaa yako naamini wewe unafelishwa na mazingira,usafi usafi eneo ulilopo vitendea kazi vyako,nk

unafanya biashara ya chakula kumbuka hata kama unaanza na mtaji mdogo kuna standard lazima uanze nazo usipoanzia hapo utadoda na msosi wako hamna mtu anatka risk afya yake kukuonea huruma uuze.

Jitathmini biashara yako.
 
Wakuu tangu nifungue biashara yangu ni wiki Sasa. Mazingira na miundombinu ya hapo ninapofanyia biashara yapo vizuri ila cha ajabu siuzi vile inavyotakiwa.

Yaani mtu anakuja anauliza kidali Tsh ngapi unamwambia bei anakigeuza geuza wee anakitathmini halafu anasema anarudi ndo imeisha hiyo. Nikasema ngoja nishushe bei miguu niuze 100 ila wananipita wanaenda kwingine!

Najiuliza nakosea wapi ila sioni kama Mungu namuomba Kila siku Kila muda hata nikiwa naweka kuku kwenye mafuta naomba pia ila wapi
TUBU OMBA REHEMA KWA MUNGU
HAPO N KIBALI TU MKUU UNARUKWA
MUNGU AKUPE KIBALI
 
Back
Top Bottom