Pamoja na kushusha bei wananipita wanaenda kwingine, najiuliza nakosea wapi?

Ofsaa Kama uko uswahilini tafuta ma koshukoshugi wa mtaa huo Kama sio mwenyeji ukienda nao sawa wateja utaletewa na hao machizi boti miguu ya kuku au kwa jina lingine brake shoe na vichwa vya kuku au helmet vitauzika tuu
 
Swali fikirishi je kabla hujafanya biashara ulifanya utafiti wa soko lako? Na kujua washindani wako wa biashara ni wakina nani nguvu zao na mapungufu yao yakoje na wateja wao ni wakina nani wanaishi wapi, je wewe nguvu zako na mapungufu yako yakoje ukijilinganisha na wao, je wateja wako taraji ni wakina nani nini umekifanya ili kuwavutia, karibu nikusaidie kwa vile najua inawezekana umeanzisha biashara kimazoea kwa kuona wengine wanafanya biashara hiyo inawezekana pia huna tabia ya ujasiriamali kama huna hata moja huwezi fanya biashara yoyote
 
Dunia ya sasa biashara bila kujiongeza utaendelea kusindikiza watu na kuchoma mtaji.
 
Dah mfano kama mimi nauza viatu vya kike rangi 3 bei nayeuza elfu 6 nakutana na watu wanataka viatu vya 3500 na 4000 wengi wakati mimi nina elfu 6 na 7 dah hatari
Mkuu waletee ivo vya afu tatu daima usipingane na mteja unachotakiwa ni kuangalia unapata nini hivyo kafungashe mzigo wawekee wakihitaji kingine pia kilete utakuta hata hivyo vingine vinaenda

Huduma moja inauza huduma nyingine jitahidi uwe na huduma zaidi ya moja hasa wanazokuelekeza wateja kwani ndio wanunuaji
 
Dah pole sana mkuu, biashara huwa na changamoto zake, hasa mwanzoni. Ila usivunjike moyo, ni hatua ya kawaida. Cha muhimu sasa hivi ni kuangalia kwanini watu wanapita, labda sio bei tu, inaweza kuwa kuna vitu vingine kama quality ya bidhaa, huduma, au hata presentation ya biashara yako. Watu wengi wanavutiwa na vitu vidogo kama packaging, customer service, na hata promotion zako.

Jaribu pia kuchunguza wapinzani wako wanafanya nini tofauti. Inawezekana bei yako ipo sawa, ila labda hawajui faida au ubora wa bidhaa zako. Fanya promotion ndogondogo, toa offer, au hata ongeza vitu vya kuvutia kama "buy one get one half-price" ili kuwashika wateja wapya.

Kuhusu kuomba, endelea bro, Mungu yupo lakini pia anataka kuona unafanya kazi kwa bidii na kutafuta mbinu mpya. Kila biashara inahitaji ubunifu, usikate tamaa, badilika na endelea kujifunza kutoka kwa wateja wako na soko. Utafika tu, ni suala la muda na strategy. 💪👊
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…