Rais anapinga ufisadi jukwaani, haoni kuwa tatizo ni mfumo? Rais anachofanya ni kucheza siasa za kiki. Maamuzi ya kununua hilo gari yamefuata taratibu zote za manunuzi. Kama hakuridhika na huo ununuzi, angeanza na wote walioshiriki kwenye mchakato mzima wa ununuzi wa hilo gari. Hii ni ikiwemo na waziri/katibu Mkuu Tamisemi. Kwa taarifa yako kwa mtindo huo, hata rais anapaswa kutumbuliwa kwa ufisadi, maana hata yeye anatumia magari mengi na ulinzi ambao hauendani na hali ya usalama inayohubiriwa. Lakini kwakuwa tuna bunge kibogoyo ndio maana wanasubiri kucheza beat za rais. Kwa wenye upeo mdogo wanaweza kuamini rais anapambana na ufisadi, ukweli ni kuwa rais anapambana na matumizi ya neno fisadi.