General Mangi
JF-Expert Member
- Dec 21, 2013
- 15,303
- 23,064
Kumiliki au kuchimba gesi?Kumiliki Kitalu cha gesi ni bei,?gani
Kuna u tofauti hapo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kumiliki au kuchimba gesi?Kumiliki Kitalu cha gesi ni bei,?gani
Hawana ela hao.Twambie kwanza kuwekeza kwenye ges kunahitaji mtaji wa tsh.ngap na utuambie mo na bakhresa wakiungana wana tsh ngap ndo ulete porojo zako hizi
Pamoja na kwamba Taifa la Norway lina kiwango kikubwa cha gesi linategemea kwa kiasi kikubwa umeme wa maji (Hydroelectric power)
Kwenye suala la umeme uchaguzi wa kutumia umeme wa maji (hydroelectric power) ni bora zaidi ukilinganisha na vyanzo vingine vya umeme.
Nchi ya Norway ni moja ya nchi duniani inayotegemea pia uchumi wa gesi. Lakini pamoja na kwamba Norway wana kiwango kikubwa cha gesi lakini bado umeme wa maji umekuwa wa gharama nafuu na ndio unatumika sana kama chanzo cha umeme.
Kwa Norway umeme wa gesi huwa wanautumia kipindi cha baridi pale ambapo umeme wa maji umezidiwa.
Gesi ni nishati ambayo mara nyingi ni nzuri kwa matumizi ya kupikia. Hivyo mimi nadhani kama serikali ina nia ya kuendeleza uchumi wa gesi. Basi ijikite kuitumia hiyo gesi katika mambo mengine mfano kupikia, na kuanzisha viwanda vinavyotumia gesi asilia. Mfano viwanda vya mbolea ni viwanda ambavyo hutumia gesi asilia kuzalisha mbolea.
Pamoja na kwamba tutaitumia gesi pia kuzalishia umeme lakini tuyape maji kipaumbele cha kwanza kwasababu maji ni bure na pia ni renewable resources. Na uzuri ni kwamba geographia ya taifa letu tumejaliwa vyanzo vingi vya maji, hivyo tukizitumia akili zetu vizuri tutaweza kufanya vizuri hata dunia ikatushangaa.
View attachment 1748264View attachment 1748265View attachment 1748266View attachment 1748267View attachment 1748268
Hali ya Norway ni tofauti. Nchi yao ina miamba na fjords ambayo kwa asili imekuwa ikitumika kuzalisha nishati hata kabla gesi yao ya North Sea kupatikana. Kwa sababu ya miamba, mabwawa yao hayajai matope hata siku moja, na kwa sababu ya wingi wa fjords maporomoko ya maji ni mengi na hivyo kufanya uzalishaji wa umeme kuwa wa gharama ndogo. Ingekuwa vizuri kama ungetuambia Norway imejenga miradi mingapi ya hydro power toka gesi yao ipatikane. Ninavyojua Norway wako mestari wa mbele kupinga ujenzi wa hydropower projects. Ndio maana walikataa kuufadhili huu mradi pamoja na kuwa walifadhili hatua zote za awali za utafiti. Athari ya mabwawa makubwa inajulikana dunia nzima. Ni nchi chache sana ambazo zinawekeza kwenye miradi ya aina hii.
Amandla...
Unaona sasa akili za ajabu?Mtanzania gani anauwezo wa kuwekeza kwenye gesi?
Hata Mo na Bakhresa wakiungana hawawezi
Watanzania wengi hawawezi kuchakata mambo.. Na ni washamba wa wazungu wao wanaamini kitu kifanikiwe awepo mzunguUnaona sasa akili za ajabu?
Kwani wewe unadhani wanaokuja kuwekeza toka nje huwa na pesa za kuwekeza taslimu?
Mo na Bakhresa ni benki gani inaweza kukataa kuwapa mkopo?
Hata umeme wa gesi ni mihimu vilevile. Tatizo hatujui mmiliki wa hiyo gesi ni nani na itatugharimu kiasi gani kuzalishia umeme.Umeme wa maji bado ni muhimu sana duniani. Hao wakina mhongo na shule zao za kukariri wanataka kuturudisha nyuma.
Hapa chini ni taarifa kwa kutumia google:Hizo data sio za zama hizi.TUSIDANGANYANE.Norway kamwe hawatumii hydroelectric power.Wana Mafuta na gesi kibao.Wanatumia Nuclear Plant unaoendeshwa na Gesi.Isitoshe ni kisiwa kidogo hata Zanzibar kubwa.Nchi zote alizozitaja huyo Profesa Bashite mpya hazitumii (H.E.P).Zote zinatumia aidha Nuclear Plants,Gesi,Diesel.Huu mradi wetu ni upotevu wa pesa.Isitoshe Dunia inakabiliwa na janga liitwalo Climate Change,ambalo Mfadhili mkubwa Marekani wamejitoa.Hii hali inasababisha uharibifu mkubwa wa mazingira kama vile joto kali sana,Ukame,Nchi nyingi kugeuka Jangwa n.k.Profesa Original Mr Muhongo yupo sahihi kabisa.Nyie ndio wale CAG aliwataja kwenye ripoti yake.
)Hizo data sio za zama hizi.TUSIDANGANYANE.Norway kamwe hawatumii hydroelectric power.Wana Mafuta na gesi kibao.Wanatumia Nuclear Plant unaoendeshwa na Gesi.Isitoshe ni kisiwa kidogo hata Zanzibar kubwa.Nchi zote alizozitaja huyo Profesa Bashite mpya hazitumii (H.E.P).Zote zinatumia aidha Nuclear Plants,Gesi,Diesel.Huu mradi wetu ni upotevu wa pesa.Isitoshe Dunia inakabiliwa na janga liitwalo Climate Change,ambalo Mfadhili mkubwa Marekani wamejitoa.Hii hali inasababisha uharibifu mkubwa wa mazingira kama vile joto kali sana,Ukame,Nchi nyingi kugeuka Jangwa n.k.Profesa Original Mr Muhongo yupo sahihi kabisa.Nyie ndio wale CAG aliwataja kwenye ripoti yake.
Pamoja na uliyosema kuwa jweli, kwa nini na bssisi kama kuna mahali pana fursa hiyo tusiitumie! Rufiji ipo, kwa nini tuiache.Hali ya Norway ni tofauti. Nchi yao ina miamba na fjords ambayo kwa asili imekuwa ikitumika kuzalisha nishati hata kabla gesi yao ya North Sea kupatikana. Kwa sababu ya miamba, mabwawa yao hayajai matope hata siku moja, na kwa sababu ya wingi wa fjords maporomoko ya maji ni mengi na hivyo kufanya uzalishaji wa umeme kuwa wa gharama ndogo. Ingekuwa vizuri kama ungetuambia Norway imejenga miradi mingapi ya hydro power toka gesi yao ipatikane. Ninavyojua Norway wako mestari wa mbele kupinga ujenzi wa hydropower projects. Ndio maana walikataa kuufadhili huu mradi pamoja na kuwa walifadhili hatua zote za awali za utafiti. Athari ya mabwawa makubwa inajulikana dunia nzima. Ni nchi chache sana ambazo zinawekeza kwenye miradi ya aina hii.
Amandla...
Childish response.Naona umenivuta kwa nguvu nije nivuruge hali ya hewa humu ndani. Huyu mleta uzi kasema Norway wanatumia umeme wa maji, hivyo inabidi na sisi tuwaige Norway. Akija mwingine akisema Brazil wanatumia umeme wa gas, na wamepiga hatua kwenye viwanda nao pia tuige? Ama hapa unataka nijadili nini?
Rafiki kwa mazingira ni swala la kulinganisha, na ukilinganisha njia zote za kufua umeme iliyo reafiki kwa mazingira ni ile ya maji. mLakini hii haina maana in zero. Inaathiri mazingira lakini kiwango ni cha chini ukilinganisha na njia zingine.Kwenye suala la emission ya green house gas, hydro power haiko nyuma. Mimea na mapori yatayofunikwa na bwawa itaoza na kutoa methane ambayo ni mbaya mara 20 kuliko carbon dioxide gases. Kutuambia kuwa hydro power ni environmental friendly ni ujinga uliopitiliza.
Amandla...
Badala ya kuniuliza mimi, ungejiuliza kwa nini pamoja na kuwa na mabwawa hayo makubwa ya kuzalisha umeme, mara kwa mara tumekuwa na upungufu mkubwa wa umeme. Mara ngapi tumeambiwa kuwa kina cha maji Mtera na/au Kihansi kimepungua mno kiasi cha kuathiri uwezo wao wa kuzalisha umeme? Mara ngapi tumeombwa tufanye maombi ili mvua zinyeshe za kutosha ili mabwawa yajae? Una uhakika gani kuwa kila mwaka tutakuwa na mvua za kutosha kulijaza hilo bwawa hasa ukizingatia kuwa kiasi cha maji yanayoingia katika mto Ruaha yamepungua sana toka Feasibility study kuhusu mradi huu ilipofanyika miaka 50 iliyopita? Tumejiuliza impact ya mabaliko ya tabia nchi katika kiwango cha maji yatakayopatikana? Kitu kingine ambacho kinapunguza uzalishaji katika mabwawa yaliyopo ni kiasi kikubwa cha matope kilichomo katika mabwawa hayo hali ambayo itatokea katika bwawa hili jipya. Matope pia yanachangia uharibikaji wa mfumo wa kuzalisha nishati ( soma taarifa ya utafiti kuhusu bwawa la Masinga kwq jirani zetu Kenya).Wewe unaongea mambo ya.ajabu sana.
Hapa Tz tunayo mabwawa mangapi ya umeme wa maji??, tunayo toka lini???, je hadi sasa yameshindwa kuzalisha umeme??, je teknolojia ya leo ya kutengeneza hayo mabwawa ni sawa na teknolojia ya miaka ya nyuma mfano miaka ya 60-70??
Mazingira yetu ni tofauti na nchi kama Norway. Fursa ipo katika gesi asilia, geothermal, upepo, sola n.k.na sio mto Rufiji. Kitu kingine tunachoweza kufanya ni kupunguza umeme unaopotea wakati wa usambazaji na kuhakikisha vifaa vyetu vinavyotumia umeme vina efficiency ya hali ya juu ya matumizi ya umeme.Pamoja na uliyosema kuwa jweli, kwa nini na bssisi kama kuna mahali pana fursa hiyo tusiitumie! Rufiji ipo, kwa nini tuiache.
Yes! Watanzania sisi ni wapumbavu na wajinga.. Miaka nenda miaka rudi mambo ni haya haya, wanatuchezea KENDE tu, tunapiga piga kele mitandaoni kama MAZWAZWA/MAPOPOMA, usishangae hili nalo kupita..Muhongo haifai kuzungumzia suala la electrical power.
Hatujasahau aliwaambia watanzania wanafaa kuwekeza kwenye juice tu na siyo gasi ili wazungu wake wapate vitalu vya gas.
Hao hao aliowagawia vitalu ndo anawapigania sasa hv wapate soko la gasi.
Watanzania siyo wapumbuvu na wajinga kiasi hicho. Mradi wa Bwawa la Nyerere uendelee na umaliziwe una tija kubwa kwa Taifa!!
Ingekuwa gasi ina manufaa tungeshaona bei za umeme zikishuka bei! Mbona hamna unafuu wowote?
Hatupendi udalali sisi!!
Ukicheka na mtoto mwishowe anakushika makalio tu..Thanks maneja kwa DATA; ukweli alioyasema profesa Muhongo hata kama yana ukweli but kwa gharama ambazo tumeisha ziingia, sioni kama ni busara kuachana na mradi ule wa Rufiji. Asante pia kwa hizi data; binafsi maprofesa wa Tanzania hua nawaamini pale wanapokua darasani kufundisha, huku field wana pwaya sana, sijui tatizo huaga ni nini? Tumeisha tumia zaidi ya Trilion kadhaa halafu eti tusitishe tu kwasababu umeme wa dunia ni wa gas? Point nyingi alizozingumza Muhongo pamoja na CAG ukweli zote Zitto Kabwe alizizungumza bungeni, kwamba utafiti wa mradi ule ulifanywa na mwalimu Nyerere miaka ya 70, kapitieni Hansard za Bunge, wabunge wa ccm walipinga, Muhongo (nadhani alikua bado waziri ) alikaa kimya, hakum support Zitto wakati ule halafu leo tumetumia pesa nyingi hivyo, "wasomi" wa bungeni wanataka tusitishe, BIG NO, twendage hivyo hivyo
Sina la kukuambia maana hutaki kusikiliza. Athari za mabwawa makubwa kama hili ni makubwa kuliko njia nyingi za uzalishaji nishati. Mbaya zaidi ni kuwa uzalishaji wake sio predictable hasa katika mazingira ya mabadiliko makubwa katika tabia nchi. Yote haya tunayaona Kihansi na Mtera lakini hatutaki kujifunza.Rafiki kwa mazingira ni swala la kulinganisha, na ukilinganisha njia zote za kufua umeme iliyo reafiki kwa mazingira ni ile ya maji. mLakini hii haina maana in zero. Inaathiri mazingira lakini kiwango ni cha chini ukilinganisha na njia zingine.