Pamoja na kwamba Taifa la Norway lina kiwango kikubwa cha gesi linategemea kwa kiasi kikubwa umeme wa maji (Hydroelectric power)

Pamoja na kwamba Taifa la Norway lina kiwango kikubwa cha gesi linategemea kwa kiasi kikubwa umeme wa maji (Hydroelectric power)

Hydro inaonekana ina bei nafuu kwa sababu gharama za uharibifu wa mazingira haziingizwi kwenye hizo hesabu. Ni kama vile mkaa unaonekana ni nafuu kuliko gesi kwa sababu gharama za deforestation haziingizwi kwenye bei. Tungekuwa tunajumuisha na gharama ya kupanda upya miti na athari katika tabia nchi, bei ya mkaa isingeshikika.

Amandla...
Mjinga pekee asiyejua kwamba hydroelectric power ni environmental friendly energy source. Natural gas ni fossil fuel inachafua mazingira ya anga letu kwa kuemit green house gases ambazo zinaongeza joto duniani.
 
Muhongo alikurupuka bila kuwa na data , uprofesdor ni pamoja na kuzungumza kisayansi .

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
Muhongo Ni afisa masoko anatafuta soko la gesi kwa commison ikikubaliwa umaskini anauaga

Wabunge nchi nyingi hutumika kama maafisa madoko ili kusukuma mambo yaende ndio Maana hata spika Ndugai uliona akiobgelea mradi wa bandari ya bagamoyo ya wachina kuwa uendelee!! Yeye ndie makerting officer wao iki tick atakuwa bilionea commission yake sio ya kitoto
 
Kumbuka gesi imevumbuliwa hivi karibuni na tayari Norway ilisha wekeza ktk nishati ya umeme ya vyanzo maji vya maji toka 1891 The History of Norwegian Hydropower in 5 Minutes. Pia gesi na mafuta vilianza kuwa chanzo tajwa Norway 1959 Black Gold: Norway's Oil Story - Life in Norway.

Umeme wa maji katika nchi baridi za kaskazini kama Niagara Falls USA, Yangtse China ni sahihi vyanzo vyake ni mvua na barafu tofauti na nchi za joto za tropiki .

In 1974, the Norwegian Parliament granted license for Norway's largest hydropower project ever. More than 1500 people worked on the development at peak, and the construction was officially concluded in 1988. Today, the Ulla-Førre power system plays a key role in Norwegian energy supply. The watershed covers 2000 sq km. Total output of the power plants is more than 2 gigawatts, or about 7 per cent of the total installed capacity of all Norwegian hydropower plants

ila nchi za joto za tropiki ambazo wananchi wake wanaharibu mazingira kwa kuwa wengi ni wakulima wadogo na wachoma mkaa umeme wa kutegemea vyanzo vya maji pekee ni changamoto kubwa.


Hii ndiyo tofauti ya kijiografia na hali ya hewa inatakiwa kuzingatiwa kwa nchi za joto za tropiki kuwa na vyanzo mchanganyiko vya umeme yaani gesi ,maji ili kushinda upungufu wa nishati ikitokea ukame n.k
 
Mjinga pekee asiyejua kwamba hydroelectric power ni environmental friendly energy source. Natural gas ni fossil fuel inachafua mazingira ya anga letu kwa kuemit green house gases ambazo zinaongeza joto duniani.
Mjinga ni yule anamuita mwenzake mjinga. Uharibu wa mazingira sio suala la emission ya green house gases peke yake. Kuondoa carbon sink kwa kufunika mapori ni environmental damage. Kuzuia natural flow ya maji na kuzuia virutubisho vilivyokuwa vinapelekwa down stream ni uharibifu wa mazingira. Kuongeza joto la maji ambalo lita affect viumbe down stream ni uharibu wa mazingira. Kufyeka mapori ili kujenga barabara za kuhudumia bwawa ni uharibifu wa mazingira. Kujenga kamji kadogo kwa ajili ya wahudumiaji wa mitambo ni uharibifu wa mazingira. Kuua wanyamapori na wadudu wengine waliokuwa wanaishi eneo la mradi ni uharibu wa mazingira. Kujenga distribution network ya umeme katika heritage site ni uharibifu wa mazingira. Huo u environmental friendliness wa huu mradi uko wapi?

Siku nyingine uwe na adabu.

Amandla....
 
Naona umenivuta kwa nguvu nije nivuruge hali ya hewa humu ndani. Huyu mleta uzi kasema Norway wanatumia umeme wa maji, hivyo inabidi na sisi tuwaige Norway. Akija mwingine akisema Brazil wanatumia umeme wa gas, na wamepiga hatua kwenye viwanda nao pia tuige? Ama hapa unataka nijadili nini?
Ahaaa, nafikiri kwa busara tu, sababu nchi nyingi duniani wanatumia HEP ni wazi hakuna mtu atakayependekeza matumizi ya gas
 
Pamoja na kwamba Taifa la Norway lina kiwango kikubwa cha gesi linategemea kwa kiasi kikubwa umeme wa maji (Hydroelectric power)

Kwenye suala la umeme uchaguzi wa kutumia umeme wa maji (hydroelectric power) ni bora zaidi ukilinganisha na vyanzo vingine vya umeme.

Nchi ya Norway ni moja ya nchi duniani inayotegemea pia uchumi wa gesi. Lakini pamoja na kwamba Norway wana kiwango kikubwa cha gesi lakini bado umeme wa maji umekuwa wa gharama nafuu na ndio unatumika sana kama chanzo cha umeme.

Kwa Norway umeme wa gesi huwa wanautumia kipindi cha baridi pale ambapo umeme wa maji umezidiwa.

Gesi ni nishati ambayo mara nyingi ni nzuri kwa matumizi ya kupikia. Hivyo mimi nadhani kama serikali ina nia ya kuendeleza uchumi wa gesi. Basi ijikite kuitumia hiyo gesi katika mambo mengine mfano kupikia, na kuanzisha viwanda vinavyotumia gesi asilia. Mfano viwanda vya mbolea ni viwanda ambavyo hutumia gesi asilia kuzalisha mbolea.

Pamoja na kwamba tutaitumia gesi pia kuzalishia umeme lakini tuyape maji kipaumbele cha kwanza kwasababu maji ni bure na pia ni renewable resources. Na uzuri ni kwamba geographia ya taifa letu tumejaliwa vyanzo vingi vya maji, hivyo tukizitumia akili zetu vizuri tutaweza kufanya vizuri hata dunia ikatushangaa.

View attachment 1748264View attachment 1748265View attachment 1748266View attachment 1748267View attachment 1748268
Uko sahihi lakini ni mwendawazimu peke yake anayeweza kukubali kwamba inajengwa JNHPP mwaka 2020 kwa kutumia feasibility study na design ya mwaka 1970/72 tutegemee kupata matokeo chanya na endelevu tukizingatia mabadiliko ya teknolojia, hali ya hewa, uchumi na mifumo ya biashara!
 
Hivi hawa wasomi wa kiafrika baada ya kumaliza kisoma, huwa wanaweka taaluma zao ndani ya briefcases na kufikiri kwa kutumia matumbo yao?

Huyu muhongo alikuwa waziri wakati wa JK, na wakati wa scandal ya Escrow alituthibitishia kwamba yale mabilioni ya pesa hayakuwa ya Watanzania. Lakini tume ilikuja na majibu tofauti na kututhibitishia kwamba muhongo aidha hana alichokijua au na yeye nae alikuwa ni duka. JK hakuwa na namna aling'oa katika nafasi yake ya uwaziri.

JPM alipoingia madarakani alimrudisha katika nafasi ileile ya uwaziri wa nishati na madini, hakukaa muda mrefu makinikia yakamtoa madarakani. Pia alituthibitishia ule ulikuwa ni mchanga na hakukuwa na kiwango kikubwa cha madini..

Leo huyu muhongo anapata wapi nguvu za kutuambia Watanzania kwamba umeme wa hydro ni gharama compare na gas?? Hembu atuache kwanza.
 
Mjinga pekee asiyejua kwamba hydroelectric power ni environmental friendly energy source. Natural gas ni fossil fuel inachafua mazingira ya anga letu kwa kuemit green house gases ambazo zinaongeza joto duniani.

Kwenye suala la emission ya green house gas, hydro power haiko nyuma. Mimea na mapori yatayofunikwa na bwawa itaoza na kutoa methane ambayo ni mbaya mara 20 kuliko carbon dioxide gases. Kutuambia kuwa hydro power ni environmental friendly ni ujinga uliopitiliza.

Amandla...
 
Uko sahihi lakini ni mwendawazimu peke yake anayeweza kukubali kwamba inajengwa JNHPP mwaka 2020 kwa kutumia feasibility study na design ya mwaka 1970/72 tutegemee kupata matokeo chanya na endelevu tukizingatia mabadiliko ya teknolojia, hali ya hewa, uchumi na mifumo ya biashara!
Sasa, ndio ilishaanza kujengwa, na mkataba tulishaingia. Ndio mchukue kamba mjinyonge. Madaraja tumejenga nendeni mkabomoe, fly over tumejenga nendeni mkabomoe, stendi ya Mbezi tumejenga nendeni mkabomoe, hospitali tumejenga nendeni mkabomoe, meli tumenunua nendeni mkaziuze, Bandari ya Dar tuliipanua nendeni mkaipunguze. Ni hayo tu.
 
Hizo data sio za zama hizi.TUSIDANGANYANE.Norway kamwe hawatumii hydroelectric power.Wana Mafuta na gesi kibao.Wanatumia Nuclear Plant unaoendeshwa na Gesi.Isitoshe ni kisiwa kidogo hata Zanzibar kubwa.Nchi zote alizozitaja huyo Profesa Bashite mpya hazitumii (H.E.P).Zote zinatumia aidha Nuclear Plants,Gesi,Diesel.Huu mradi wetu ni upotevu wa pesa.Isitoshe Dunia inakabiliwa na janga liitwalo Climate Change,ambalo Mfadhili mkubwa Marekani wamejitoa.Hii hali inasababisha uharibifu mkubwa wa mazingira kama vile joto kali sana,Ukame,Nchi nyingi kugeuka Jangwa n.k.Profesa Original Mr Muhongo yupo sahihi kabisa.Nyie ndio wale CAG aliwataja kwenye ripoti yake.
Toka lini Norway ni kisiwa na ndogo kuliko zenji?
 
Umeme wa maji bado ni muhimu sana duniani. Hao wakina mhongo na shule zao za kukariri wanataka kuturudisha nyuma.
 
Back
Top Bottom