Pamoja na madhaifu ya Kanisa Katoliki lakini kwenye kipengele cha kukemea na kuonya watawala ambayo ni Kazi ya kinabii na kitume, Hongereni Sana

Pamoja na madhaifu ya Kanisa Katoliki lakini kwenye kipengele cha kukemea na kuonya watawala ambayo ni Kazi ya kinabii na kitume, Hongereni Sana

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Kwema Wakuu!

Ingawaje Mimi ni mtibeli msabato lakini hiyo hainifanyi nisione mazuri ya madhehebu na dini zingine.

Sisi wasabato tunajinadi na huenda kwa sehemu tunajulikana kwa kufuata maandiko matakatifu ya Biblia. Hiyo inatufanya tuwakalie kooni watu wa dini na madhehebu mengine yasiyofuata maandiko matakatifu ya Biblia, hasahasa amri ya Sabato ambayo dini zote za Abraham zinajua fika kuwa sabato ni moja ya amri kuu ya MUNGU wa Ibrahim, Isaka na Yakobo kama ilivyoandikwa kwenye Torati ya Musa.

Dini zote za Abraham ikiwemo uislam, Ukristo na Uyahudi zinatambua siku ya Sabato ni Jumamosi hilo Wala hakuna atakayebisha.

Lakini katika nchi yetu Kanisa la Katoliki licha ya madhaifu yake mengine ikiwemo kutofuata amri ya Sabato lakini wanafanya Kazi nyingine kubwa ambayo ni Kazi ya kitume na kinabii Kam walivyofanya Mitume na manabii waliondikwa katika vitabu wanavyoamini ni vitakatifu.

Wakatoliki hukemea uovu au wakiona mambo hayaendi sawasawa wanautume ndani yao, wanakereketwa kuukemea.

Biblia inatoa maagizo watu ikiwemo Kanisa kukemea maovu sio maovu kijumlajumla tuu Bali hata maovu ya watawala wanaoongoza watu.

Katika Hilo nalipongeza Kanisa Katoliki kwa kufanya Kazi ya MUNGU ya utume kwa sababu hiyo ndio Kazi namna Moja ya Kanisa, kukemea maovu hasahasa maovu ya watawala. Kwa sababu kama watawala wakikemewa waache uovu automatically jamii inakuwa jamii ya HAKI.

Huwezi kemea waumini huko makanisani ATI waache maovu alafu wakati huohuo hukemei watawala wanaofanya uovu. Huo ni woga. Huo ni unafiki. Huko ni kumtumikia vibaraka vya shetani.

Ni jukumu la viongozi wa dini zote kukemea waovu hadharani ikiwa maovu yanafanyika hadharani.

Haiwezekani uovu ufanywe hadharani alafu wewe kama kiongozi wa dini uonye faraghani. Hiyo Sio busara Wala sio HEKIMA. Huo ni woga na unafiki.

Madhehebu mengine ikiwemo Wasabato tujifunze hapo.
Mambo ya kusema Kanisa halijihusishi na siasa ni kisingizio kisicho na maana yoyote.

Manabii karibia wote walikemea maovu ya watawala.

Yesu kusema Ya kaisari apewe kaisari na ya Mungu apewe Mungu hakumaanisha viongozi wa dini wasikmee maovu ya watawala.

Sisi kama Watibeli, hatutaweza kushiriki kwenye ibada na madhehebu ambayo hayana uwezo wa kukemea uovu wa watawala.

Alafu unakuta mtu anaingia kanisani wakati mnajua kabisa alipata uongozi kwa kuiba Kura. Hivi hizi dini ni dini za Mungu kweli au ni dini za mashetani?

Dini ya Mungu WA kweli, Dini ya HAKI kamwe, narudia Kamwe! Haitakubali muumini aliyeiba Kura na akawa kiongozi kuingia katika jengo la ibada. Lazima afukuzwe, achague kujiuzulu na kuachia nafasi ya uongozi alioupata kwa wizi ili aendelee kushiriki ibada katika Kanisa au hekalu au msikiti huo au aendelee na uongozi wake wa kishetani lakini asiwe muumini wa dini au dhehebu husika.

Dini ya kweli haihitaji mtu Bali watu ndio huhitaji dini ya kweli.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
" Dini ya kweli haihitaji mtu,, bali watu ndiyo huhitaji dini ya kweli " 🤝
 
Hao viongozi wa Katoliki Tanzania walipaswa kuandamana kupinga ujinga unaofanywa na serikali ktk chaguzi, kama vile viongozi wa katoliki DRC walivyofanya kupinga njama za Kabila kujiongezea mhula wa urais.

Maneno matupu hata kwenye kanga yapo.
 
Kanisa Katoriki limetoa dira tunasubiri na makanisa mengine yafuate mkondo huu siyo bwana asifiwe mwanzo mwisho wakati wanaona haki inavyopokwa waziwazi na hawa CCM wakisaidiwa na Serikali.
 
Leo wamekemea hadharani kesho wakifuatwa sirini kupewa milungula wanapokea hii haitoleta mtikisiko Kwa hao watawala wanaowakemea

Wakiona inawafaa kubadirisha mienendo ya hawa viongozi wetu walafi,wezi na maharamia basi ni vyema wakaiga walichofanya viongozi wa kikatolliki kule DRC Cha kuandamana kupinga na kulani hadharani na kufanya walichofanya viongozi wa kikatoliki wa hapo Kenya Kwa kukataa hadharani na kurudisha sadaka kutoka Kwa viongozi wa kiserikali yao


Wao wamesema tuwasubiri na viongozi wa madhehebu na dini zilizobaki
 
Back
Top Bottom