Pamoja na mziki wao kuwa tofauti je kati ya Michael Jackson na Bob Marley nani alikubalika zaidi ulimwenguni

Pamoja na mziki wao kuwa tofauti je kati ya Michael Jackson na Bob Marley nani alikubalika zaidi ulimwenguni

Bob ni Reggae,MJ ni pop,R Kelly ni R'n'B na 2pac ni hip hop.Ila kati ya uliowataja Bob ni issue nyingine kabisa.MASHAIRI NA UJUMBE WA NYIMBO ZAKE,NI NEXT LEVEL UKICOMPARE NA MJ.JAPO MTOA MADA UMEBASE KWA MJ,KAMSIKILIZE TENA BOB!
 
Hauwezi ukafananisha uzito wa Reggae na pop hata siku moja.Reggae ni mziki unaopendwa,kusikilizwa,kueleweka na kuchezeka na wengi kuliko pop.Bob ni zaidi ya MJ.Just assume,Bob asingekufa mapema?Ungekaa umlinganishe na MJ?
 
Acha ujinga basi!

Umeanzisha mada acha watu wachangie kwa uhuru wao,kama hutaki kupingwa kua Bob ni Zaidi ya Mj kwanini ulianzisha hii thd?

Siku nyingine unapokua una jambo jadili na watu wa nyumbani kwenu kuliko kutuletea utoto humu,JF ni home of great thinkers.
Jamaa nimemuona ni dizaini kama choko Fulani hivi.. Bora mada angeiandika kabisa kwamba Maico ni zaidi ya Bob kuliko kuingizia maneno yake kama shoga huyo anaye mshabikia.
 
Hebu kasikilize wimbo wa bob unaoitwa Redamption song.(kama sijakosea,unahusu uhuru wetu watu weusi).Nipo tayari kwa marekebisho wakuu.
 
yah kutokana na ufanisi kwa nafasi yake katika mchezo husika.. mpira wa miguu yoyote anaweza kuwa mchezaji bora wa mechi kuanzia kipa mpk no 11..
Hivi unaweza kumpambanisha Golikipa na Fowadi na ukategemea kupata majibu ya Kina ambayo yatakutosheleza kweli?
 
Michael Jackson alitokea kukubalika na wapenzi wengi wa muziki kwanza aina ya muziki wake ni pendwa zaidi, alikuwa anaburudisha sana jukwaani, alikuwa pia anajitolea kwa jamii yote. mfano mzuri ebu angalia shows mbalimbali zilizofanywa na MJ sehemu tofauti duniani utapata jibu haraka.

Bob Marley alikuwa mwanaharakati na aina ya muziki wake ni sehemu ndogo ya jamii ilikuwa inaukubali sana mpk sasa iko hivyo.. kwa kifupi hakufocus kuburudisha bali kuleta mapinduzi kuona jamii yote inakuwa sawa
 
Michael Jackson alitokea kukubalika na wapenzi wengi wa muziki kwanza aina ya muziki wake ni pendwa zaidi, alikuwa anaburudisha sana jukwaani, alikuwa pia anajitolea kwa jamii yote. mfano mzuri ebu angalia shows mbalimbali zilizofanywa na MJ sehemu tofauti duniani utapata jibu haraka.

Bob Marley alikuwa mwanaharakati na aina ya muziki wake ni sehemu ndogo ya jamii ilikuwa inaukubali sana mpk sasa iko hivyo.. kwa kifupi hakufocus kuburudisha bali kuleta mapinduzi kuona jamii yote inakuwa sawa
Well said
 
Ukijulikana zaidi/sanaaa basi ujue unakubalika zaidi/sanaa.
Tukitumia mantiki hiyo basi hakuna mwanamziki aliyejulikana/anayejulikana zaidi kumshinda Michael Jackson hivyo basi yeye ndiye wa kwanza na wengine wanafwata

Kwangu mimi linapokuja wazo la regga
nawaza luck dube tu
 
Uzuri wa mpira tunahesabu magoli na watu hujali matokeo kusema chenga tumewala ingawa wametufunga haitiliwi maanani. Mziki ni tofauti kabisa kila mtu anachake, mziki pia una utamaduni wake na ukoloni wake na masoko/marketing yake. Hivyo mimi huwa sioni sababu ya kukomaliana sana, lakini kwangu na haya ni mapenzi yangu binafsi moja nampa Le Grand Maitre Franco Luambo & TP OK Jazz, mbili ni Bob Marley and The Wailing Wailers na tatu Wako Jacko-Michael Jackson. Ununuzi wangu wa santuri na usikilizaji uko kwenye mtiririko huo.
 
  • Thanks
Reactions: ARV
Michael Jackson alitokea kukubalika na wapenzi wengi wa muziki kwanza aina ya muziki wake ni pendwa zaidi, alikuwa anaburudisha sana jukwaani, alikuwa pia anajitolea kwa jamii yote. mfano mzuri ebu angalia shows mbalimbali zilizofanywa na MJ sehemu tofauti duniani utapata jibu haraka.

Bob Marley alikuwa mwanaharakati na aina ya muziki wake ni sehemu ndogo ya jamii ilikuwa inaukubali sana mpk sasa iko hivyo.. kwa kifupi hakufocus kuburudisha bali kuleta mapinduzi kuona jamii yote inakuwa sawa
Haters hawataki kabisa huu ukweli hahahahhaha
 
Asee nimeufuatilia huu Uzi kimya kimya tangia mwanzo na sikutaka kuchangia chochote but nimejikuta nalazimika tu.

Anyways, nianze kwa kutangaza interests zangu kwamba Mimi Shabiki mkubwa wa wote hawa hivyo sitegemei maandishi yangu kuwa na upendeleo wa upande wowote.

Nikianza na MJ who was considered to be "The instrument of the world" in case of entertainment.. mj alikuwa the best entertainer to ever walk in this world...alikuwa anajua kucompose mziki wa kuburudisha na kuinspire watu kwa namna ya ajabu sana. Michael Jackson is truly definition of a musical genius..anajua kucheza, anajua kuimba, anajua kuprovoke hisia za hadhira yake ndio maana akiwa mtoto kabisa alikweza kuwa star wa band ya nyumbani kwao ya Jackson 5, tukubaliane kuna kitu hatuwezi kumnyanganya Michael he was a musical genius and akibebwa zaidi na ile natural talent yake.. Alipata pia bahati ya kukulia Kwenye spotlight na platform kubwa za kimziki kama MTV, BET, e.t.c, world class music facilities, great producers and directors akina Quincy Jones e.t.c kutoboa kwake na kurindima dunia nzima kulikuwa hakuepukiki.

But Bob Marley alienda mbele zaidi ya kuwa musical genius zaidi ya MJ, alikuwa na kipawa cha unabii ndani yake kama nyongeza yake..mazingira aliyozaliwa na kukulia yalikuwa magumu na hatari kufanikiwa kimziki na kimaisha..alizaliwa baada ya mama yake kubakwa na mkoloni mzungu Sinclair Marley then akatelekezwa yeye na mama yake pale Kingston Jamaica wasijue la kufanya hapa ndipo "No woman no cry" ikatengenezewa.. Being born fatherless. Hakuwa na namna akajikuta anakuwa Fundi welding na baadae msoma viganja vya watu ili kuganga njaa then akaachana navyo na kujiunga na Peter tosh na Bunny wailer kufanya music then yaliyofuata ni history tamu ya kazi nzuri zisizosahaulika milele.

Bob alikuwa na charismatic ya kuongea jambo likapokelewa kwa nguvu ya ajabu na watu..rejea aliweza kusimamisha vita iliyokuwa inataka kuibuka Jamaica kwa kuanzisha concert ya one love iliyowafanya maadui wa kisiasa wakawambia wafuasi wao waweke silaha chini wakaja pamoja jukwaani na kuanza safari mpya ya amani na Upendo..likapigwa riddim la love and prosperity all day long pale kwenye concert.. That's was huge success ya reggae na Marley kwa ujumla Duniani.

Sikia na hii hapa tena!, Nyimbo ya Bob natural mystic ilipewa tuzo ya kuwa song of the century kutokana na mashairi yake kutabiri ujio wa ugonjwa wa ajabu utakaotesa watu na kuua mamilion Duniani soon baada ya ngoma kutoka Ukimwi ukagundulika Afrika na kuanza kuua maelfu ya watu na unabii wake ukatimia. Nitajadili nyimbo hii kwenye reply inayofuata hapo chini.

Then nyimbo zake nyingi zinatumika katika vyuo mbalimbali kucites cross cutting ishu za philosophy and musicology. This is not simple.

Mwl Nyerere alishawai kumdharau Bob kutokana na muonekano wake kama sisi tunavyomdharau hapa ila Kwenye tamasha la Uhuru wa Zimbabwe Bob alipopanda jukwaani kufanya Sanaa zake Mwl alimwomba aje Tanzania maana kuna Mengi alikuwa anataka kuyasema lakini alikuwa hana lugha nyepesi na ya kueleweka kirahisi kwa watu ila Bob alikuwa anajua hii namna then na kipindi hicho agenda kuu ya Nyerere, Nkurumah, Kaunda e.t.c na afrika yote ilikuwa ni "Africa unite" na Bob ndio ilikuwa dhumuni lake na bahati nzuri alikuwa anajua lukiwasilisha kwa lugha nzuri na inayoeleweka na wote kirahisi na kugusa hisia zao za ndani zaidi....siku hiyo Mwl Nyerere alishangaa hadi akaenda kumsimulia mwanae makongoro na akaanza kuwa anavurumusha reggae tu za Marley akiwa magogoni..but sina hakika kama alikuwa anakula na sacrament ya akina Marley.. (Weed)...sina hakika.

Bob ana mengi sana tutajaza serve za Max bure.

But wote ni musical genius in their own way but Bob Marley alikuwa na some touch za unabii anaongea jambo then linatokea na amefanya mziki katika mazingira magumu sana ya kutaka kuuwawa na CIA because he was musical and philosophical powerful. Na walifanikiwa kumpachika cancer kidoleni na aliemuua alikiri last month nadhani akiwa death bed kwamba I killed Bob Marley.

Bob and MJ are truly definition of musical genius but Bob was ahead of time.
 

Attachments

  • Edward-Seaga-and-Michael-Manley.jpg
    Edward-Seaga-and-Michael-Manley.jpg
    12.3 KB · Views: 51
Bob Marley Lyrics

"Natural Mystic"

There's a natural mystic blowing through the air;
If you listen carefully now you will hear.
This could be the first trumpet, might as well be the last:
Many more will have to suffer,
Many more will have to die - don't ask me why.

Things are not the way they used to be,
I won't tell no lie;
One and all have to face reality now.
'Though I've tried to find the answer to all the questions they ask.
'Though I know it's impossible to go livin' through the past -
Don't tell no lie.

There's a natural mystic blowing through the air -
Can't keep them down -
If you listen carefully now you will hear.

There's a natural mystic blowing through the air.

"This could be the first trumpet, might as well be the last:
Many more will have to suffer,
Many more will have to die - don't ask me why." Hapa anakwambia hili linaweza kuwa parapanda la kwanza na la mwisho.. Jinsi tutakavyoteseka..jinsi tutakavyokufa..usiniulize ni kwanini" soon baada ya hii verse ngoma ikaanza kuua watu afrika vibaya.

There's a natural mystic blowing through the air -
I won't tell no lie;
If you listen carefully now you will hear:
There's a natural mystic blowing through the air.
Such a natural mystic blowing through the air;
There's a natural mystic blowing through the air;
Such a natural mystic blowing through the air;
Such a natural mystic blowing through the air;
Such a natural mystic blowing through the air.

Tafuta hii ngoma uisikilize kwa umaskini ndo utajua bob alikuwa anaimba maneno yenye unabii wa kimafunuo ndani yake.

Huyu mvuta bangi mwacheni tu jamani...he was so much underrated for so long
 
Let me declare kwamba ni shabiki wa MJ

Lakini Ogopa sana mtu ambae hatumii nguvu kuwa star...anatumia tu kipaji chake naturally

Bob marley angetumia nguvu alizotumia MJ sijui ingekuwaje
Let me declare kwamba ni shabiki wa MJ

Lakini Ogopa sana mtu ambae hatumii nguvu kuwa star...anatumia tu kipaji chake naturally

Bob marley angetumia nguvu alizotumia MJ sijui ingekuwaje
Nguvu gn izo mkuu
 
The wako jacko ndio mtu maarufu zaidi duniani kuliko kiumbe yeyote kwa karne ya 20-21,
then anafuatiwa na Pope John Paul ii,so acha kufananisha keki na vibama..
 
Back
Top Bottom