Wote mnaweza kufikiria ni namna gani mtu asiye mkazi au mfanyakazi au mwenye appointment kwenye makazi rasmi ya Malkia wa Uingereza angeweza kupenya bila kuonekana, akafanikiwa kuingia ndani ya jumba hilo, akapiga misele kidogo, akaingia ofisi ya Malkia Elizabeth kufyonza mvinyo maalum wa Malkia, na mwisho wa siku akazama ndichi kwenye hiyo room ya Malkia na kumkuta Malkia akiwa katikati ya njozi tamu, akaketi pembeni yake na kumsubiri Malkia aamke ili wayajenge/wapeane maelekezo. Basi kunaye dogo mmoja alileta makwaru na kufankiwa mpaka Malkia mwenye alipomsanukisha.
Inadaiwa tukio hilo lilisababisha ulinzi zaidi uimarishwe na baadhi ya walinzi walifukuzwa.
Inadaiwa tukio hilo lilisababisha ulinzi zaidi uimarishwe na baadhi ya walinzi walifukuzwa.
- Tunachokijua
- JamiiCheck.com imepitia vyanzo mbalimbali na kubaini kuwa tukio la raia kuweza kupenya katika Kasri la Malkia Elizabeth mpaka Chumbani kwake ni la ukweli.
Vyanzo mbalimbali ikiwamo kurasa za The Guardian, Source and County na The Sun vinaeleza kuwa mnamo mwaka 1982, kijana mwenye umri wa miaka 22 kutoka Scotland aitwaye Michael Fagan aligusa vichwa vya habari Ulimwenguni baada ya kufanikiwa kuvuka ulinzi wa Ikulu ya Uingereza na kupenya katika Kasri la Buckingham mpaka akafika katika chumba cha Malkia Elizabeth.
Taarifa ya Polisi iliyoandikwa na Source and County ilisimulia kuwa mnamo Julai 9, 1982 saa 1 asubuhi Fagan aliingia katika historia ya ndani ya jumba la Malkia kifalme, baada ya kunywa pombe usiku wa kuamka Julai 9, 1982 Fagan alikwea ukuta wa Kasri la Buckingham na kufika kwenye paa na kuingia ndani ya makazi ya kifalme kupitia dirisha lililokuwa wazi.
Hata hivyo, inaeleza kuwa pamoja na kufanikiwa kupenya mpaka kwenye chumba cha Malikia lakini Fagan hakufanya jambo lolote baya.
Aidha, inaelezwa kuwa baada ya kukamatwa alifungwa jela kwa Miaka miwili kwa kosa lake