tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,327
- 4,624
Wewe kwenu umejenga hotel gani? Usije ukawa wawapa majukumu tu wenzako, wakati wewe kwenu hufanyi lolote.Rungwe kuna:-
1. Hifadhi ya Misitu safu za Mlima Rungwe.
2. Safu za Milima ya Kipengele 'Livingstone Mountains'
3. Crater Lake Ngosi
4. Daraja la Mungu 'Lupoto'
5. Maporomoko ya maji na ya kipekee Kapologwe (Kisondela)
6. Ziwa Kisiba
7. Maporomoko ya maji Malasusa Kapiki (Nkunga)
8. Maji Moto Ilwalilo
9. Maporomoko ya Isabula, Ngomano
10. Mti Katembo
11. Hifadhi ya Kitulo (huyu jirani yenu)
12. Majengo ya Kale, Kambi za Wajerumani
13. Fukwe nzuri za Matema
Nakadhalika
Kinachosikitisha pamoja na vivutio hivi vya utalii Rungwe haina hoteli ya maana kuweza kuhifadhi watalii wenye hadhi aghlabu kutoka nchi za ng'ambo. Hoteli zilizopo ni za elfu 20 20 za akina samolo n.k.
Hoteli pekee 'ya hadhi' ni the dilapidated L*ndmark ambayo kwa sasa huwezi muweka mtalii decent pale.
MY TAKE: Ndugu zangu na majirani zangu Wanyakyusa najua mpo wenye ukwasi wa kutosha hebu mmoja wenu ajitose hapa Tukuyu Mjini aporomoshe Hoteli ya Hadhi ndipo utalii utangazwe. Hii wilaya pamoja na Busokelo zina potential ya utalii ila hakuna malazi.