Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 593
- 1,376
Wakuu,
Hali ya usafiri Kigamboni leo sio shwari. Kama mnavyoona watu wapo wa kutosha. Pantoni linalotumika ni moja tu, likipakia tunasubiri ligeuze kuja kutufate wengine huku. Utafikiri sio weekend.
Hakuna backup ikitokea kuna shida kama hivi? Maana jinsi watu wanasukumana kuingia ni balaa, yanaweza kutokea maafa hivihivi kimasihara huku tunaangalia.
Ikiwa hatuna backup basi kuwe na utaratibu mzuri kusimamia watu yasitokee mengine, hasa ukuzingatia kuna watoto, wanawake, wazee na wenye ulemavu ambako kwenye msongamano kama huu bila usimamizi mzuri kuna uwezekano mkubwa wa tatizo kutokea.