Pantoni moja tu ndio linafanyakazi Kigamboni leo, nyingine ziko wapi? Kashikashi ya kusukumana kuwahi kuingia ni balaa!

Pantoni moja tu ndio linafanyakazi Kigamboni leo, nyingine ziko wapi? Kashikashi ya kusukumana kuwahi kuingia ni balaa!

Unafikiri Kwa nn watu wengi bado wanapanda pantoni kama hilo daraja ni rahisi kihivyo?
Kumbuka daraja linatumiwa zaidi na wenye usafiri pantoni linajazwa na watembea kwa mguu... Kuna mtu anatembea from kkoo to kivukoni ili apande pantoni avuke aende tena mpaka mnadani kwa mguu ila wengi wanaopitia darajani anakua kapanda bus pikipiki au gari binafsi huwezi tembea kkoo mpka kiga kwa mguu kupitia daraja utasaga kende😂😂😂
 
Unafikiri Kwa nn watu wengi bado wanapanda pantoni kama hilo daraja ni rahisi kihivyo?
Alafu kama unajipenda bora upite darajani nimeshashuhudia kivuko kikipoteza uelekeo kikaenda kukwamia jeshini kule nilikua nasubiri kivuko nikageuza ngoma nikalitafuta daraja na tiketi nilishakata majamaa wananiambia pantoni linakuja subiri nikawaomba tu nimepata dharura nikazunguka ya darajani nikaendelea na harakati zangu
 
Wakuu,

Hali ya usafiri Kigamboni leo sio shwari. Kama mnavyoona watu wapo wa kutosha. Pantoni linalotumika ni moja tu, likipakia tunasubiri ligeuze kuja kutufate wengine huku. Utafikiri sio weekend.

Hakuna backup ikitokea kuna shida kama hivi? Maana jinsi watu wanasukumana kuingia ni balaa, yanaweza kutokea maafa hivihivi kimasihara huku tunaangalia.

Ikiwa hatuna backup basi kuwe na utaratibu mzuri kusimamia watu yasitokee mengine, hasa ukuzingatia kuna watoto, wanawake, wazee na wenye ulemavu ambako kwenye msongamano kama huu bila usimamizi mzuri kuna uwezekano mkubwa wa tatizo kutokea.

Kwani zile za azam hazipo?
Lile moja liko kenya huko limepaki vichakani tuliaminishwa hapa linaenda kurekebishwa kwa ma bilioni ya fedha lakini kwa sasa watoto wanachezea kombolela huko
 
Watanganyika wanateseka kuliko maelezo.poleni kigamboni
 
Maeneo yote dar mtu anajenga kigamboni si bora nikaishi zanzibar tu hvi watanzania nani alituroga.
 
Mimi ndio maana kigamboni kumenikalia kushoto aisee. Imagine unapangiwa kurudi nyumbani kwako.
Hata bure wagawe viwanja mkuu kule sio kwa kukaa huna tofauti na mzanzibar siku bakhresa akikasirika hamna usafiri.
 
NCHI INAUKAKASI MWINGI SANA WATU WAKO BIZE NA BIRTHDAY YA BI KIZIMKAZI
 
Wakuu,

Hali ya usafiri Kigamboni leo sio shwari. Kama mnavyoona watu wapo wa kutosha. Pantoni linalotumika ni moja tu, likipakia tunasubiri ligeuze kuja kutufate wengine huku. Utafikiri sio weekend.

Hakuna backup ikitokea kuna shida kama hivi? Maana jinsi watu wanasukumana kuingia ni balaa, yanaweza kutokea maafa hivihivi kimasihara huku tunaangalia.

Ikiwa hatuna backup basi kuwe na utaratibu mzuri kusimamia watu yasitokee mengine, hasa ukuzingatia kuna watoto, wanawake, wazee na wenye ulemavu ambako kwenye msongamano kama huu bila usimamizi mzuri kuna uwezekano mkubwa wa tatizo kutokea.

Pigeni mbizi

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
TRA wamekusanya kodi kubwa kupita awamu zote chaajab walipa kodi wanapata tabu sio usafiri hadi huduma nyingine za kijamii,,,Sijui nn tutaweza mwendokasi shida,vivuko shida,,hapo ukute mtu wa kigamboni anasubir kivuko halafu aje tena kugombania mwendokasi awahi kazin inasikitisha sana!
 
Kumbuka daraja linatumiwa zaidi na wenye usafiri pantoni linajazwa na watembea kwa mguu... Kuna mtu anatembea from kkoo to kivukoni ili apande pantoni avuke aende tena mpaka mnadani kwa mguu ila wengi wanaopitia darajani anakua kapanda bus pikipiki au gari binafsi huwezi tembea kkoo mpka kiga kwa mguu kupitia daraja utasaga kende😂😂😂
Kwanini utembee kutoka Kariakoo mpaka Kivukoni,Kg na kuna daladala kutoka Machinga complex kwenda Kg?
 
Mkiambiwa yule mwamba aliiweza hii nchi mnakaza fuvu. Wakati wa Magu pantoni zote tatu zilikuwa zinafanya kazi. Mtu hata mwenye gari ilikuwa hukai dakika 20 hapo ushavuka. Nilikuwa sipiti darajani kabisa.
Ila mwamba alipoondoka tu upiuzi ukaanza hadi leo kuna pantoni moja tena dogo!
Pantoni inaenda kutengenezwa Mombasa kisa mbongo mwenzenu kawanyima cha juu,stupid!
 
Back
Top Bottom