FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,500
- 8,060
Habari!
Pantsir-SM, mfumo wa ulinzi wa anga (short-medium range mobile air defense system) unaosubiriwa kwa hamu, unatarajiwa kuzinduliwa panapo Juni 24 katika gwaride la kijeshi jijini Moscow katika sikukuu maalumu inayofahamika kama Siku ya Ushindi ama Victory Day nchini Urusi.
Mfumo huu wa Pantsir-SM ni toleo jipya na lililoboreshwa zaidi kutoka lile la awali la Pantsir-S1.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya serikali ya Urusi, toleo la Pantsir-SM litakuwa na makombora madogo kwa ajili ya kushambulia ndege ndogo zisizo na rubani (mini-drones) pia makombora mapya ya masafa marefu, mfumo ambao unatarajiwa kuonesha uwezo mkubwa wa kukabiliana na makombora na ndege zisizo na rubani.
Matayarisho ya uzinduzi wa zana hiyo mpya ya kiulinzi yangali yakiendelea kama inavyoonekana katika picha (picha ni kwa hisani ya Wizara ya Ulinzi ya Urusi):