Panya Magawa mahiri kwa kubaini mabomu ya kutegwa ardhini amekufa nchini Cambodia

[emoji95]BREAKING NEWS[emoji95]

TANZIA

Panya wa kiume kutoka Tanzania, Magawa ambaye mwaka 2020 alitunukiwa nishani ya dhahabu kutokana na uwezo wake wa kubaini mabomu ya kutegwa ardhini nchini Cambodia, amekufa akiwa ni panya Mzee mwenye umri wa miaka minane ambao ni umri mkubwa kwa panya.

Mwezi November mwaka jana Magawa alitimiza umri wa miaka minane na alistaafu pia mwaka jana kutokana na uzee wake kwakuwa alianza kupunguza kasi ya kutegua mabomu.

Magawa alizaliwa Morogoro, Tanzania November 5,2014 akiwa na uzani wa KG 1.2 na urefu wa Sentimita 70 na hadi anakufa amenusa mabomu na silaha nyingine zaidi ya 100.

Magawa amefia nchini Cambodia kwakuwa baada ya kustaafu hakurejeshwa Tanzania na amekufa usiku wa kuamkia Jumapili ya juzi, Magawa alipewa mafunzo Sokoine University of Agriculture (SUA) na APOPO.
 
Watanzania wengi wanakosa huduma za kijamii lakini kuna fungu la kuwatunza Hawa panya hadi uzeeni. Hii si sawa kabisa yani mnatunukia panya nishan ya dhahabu kweli?

Fakin' rodent!
 
Apumzike kwa amani Panya wetu,mpaka anafariki alikua na cheo kipi jeshini!? Je Kaacha watoto.. Au alikua single
 
Sp Sad. RIP Magawa
 
Nashangaa serikali ,Wala jwtz hawajatoa tamko la kifo Cha magawa . Kwa heshima ya taifa letu itakuwa vizuri Kama shujaa magawa atarudishwa nyumbani ,azikwe huku ili tuwe na kumbkumb ya shujaa wetu magawa. miradhi yake pia iwekwe wazi. Wizara husika isipuuze hiki kitu kwa kuwa et NI mnyama Basi ndo wapotezee, magawa amelitumikia taifa ndani na huko ng'ambo bado alifanya kazi kwa kujituma na umahili ,alijua amebeba bendera ya watanzania mil.60 huko ughaibuni Cambodia. R.IP MAGAWA ,bwana ametoa ,bwana ametwaa ,pumzika kwa amani (r.i.p soldier)[emoji24]
 
Respect to U solder Magawa.
 
Kwa hiyo watasafirisha au watazika huko huko tuu
 
Nimesoma vibaya au ni kweli. Huyu jemedari alizaliwa akiwa na KG 1.2?
Huo si uzito wa mtoto wa binadam kabisa?
Halafu alikuwa na urefu wa sm 70 alikuwa buku huyu maana si kama wale panya uhuru wala nguo
 
Watanzania wengi wanakosa huduma za kijamii lakini kuna fungu la kuwatunza Hawa panya hadi uzeeni. Hii si sawa kabisa yani mnatunukia panya nishan ya dhahabu kweli?

Fakin' rodent!
Unamuonea wivu Magawa?.
 
Poleni sana familia ya Panya Magawa.

R.i.p Luteni Magawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…