Panya Magawa mahiri kwa kubaini mabomu ya kutegwa ardhini amekufa nchini Cambodia

Nikiwa kama kaka mkubwa wa magawa naomba kuuliza
Je amelipwa stahiki zake na mafao? Yako wapi?
Maana aliacha mke na michepuko wawili kabla hajaenda huko kambodia, na watoto sita.
Serikali naomba ishughulikie hiki
 
Watakua wamemuua tu hakuna namna
 
*Wasifu wa MAREHEMU MH.PANYA MAGAWA

>>KUZALIWA
Panya MAGAWA amezaliwa tarehe 05/11/2014 mkoa wa morogoro akiwa na uzito wa kilo 1.2

>>>KABILA
Panya MAGAWA ni Mluguru wa Morogoro

>>>>MASOMO
Panya Magwa alisomea Chuo kikuu Cha SUA na kufaulu vyema kwenye masomo yake na mwaka 2016 akaanza kazi yake RASMI

>>>KAZI

Magawa ameweza kunusa mabomu 39 na silaha 28 kwa mafanikio makubwa


TUZO [emoji16]
Shirika la matibabu ya wanyama la Uingereza la PDSA lilimtuza medali ya dhahabu kwakuokoa maisha kupitia kazi yake ya kubaini mabomu hatari yaliyotegwa ardhini Cambodia

MAHUSIANO
amejihusisha na mapenzi na baadhi ya Panya wenzake ila hakufanikiwa kufunga NDOA


KUSTAFU
Panya magawa amestafu mwaka 2021 akiwa na miaka 8 na akiwa na umri mkubwa kulinganisha na Panya wengine

KIFO
Panya magawa amefariki usiku wa kuamkia jumapili mwaka 2022.

MAZISHI
utaratibu wa maziko unaendelea kupangwa japo tuendelee kutoa rambirambi za shukurani

≥>>>>>>>>>
tutamkumbuka Sana MH.MAGAWA kwa weledi wake na uchapa kazi wake

Bwana ametoa ,bwana ametwaa Jina lake lihidimiwe[emoji112][emoji112][emoji112][emoji112]
View attachment 2079565
 
Siamini yaani hii habari ya kifo cha panya nimeikuta The citizen, MSN na CNET.
Yaani huyu panya amefanya contribution kubwa duniani na alikuwa na faida na thamani kubwa kuliko asilimia 50% ya waafrika wote.

For the first time in the world history, human the most advanced but mostly stupid creature, needs to learn something from an animal especially a Rat.
 
"Magawa hajawahi kuwa na Mwanamke, maisha ya mafunzo yali-focus kwenye kwenda kuokoa maisha ya watu kwa hiyo hakuwahi kukutana na Mwanamke, nimemlea toka akiwa mdogo na jina la Magawa nimelitoa mimi kwa hiyo maisha ya Magawa yamenigusa kwa asilimia kubwa, ndio maana alipokufa nilijisikia vibaya, Tanzania tuna bahati duniani kote training centre ya panya ni Morogoro Tanzania" ——— Pendo Msegu, Mwalimu wa Panya Magawa kwenye Leo Tena ya Clouds FM
#MillardAyoUPDATES
 
Magawa kakosewa sana kukoseshwa urithi. Wahusika wachukuliwe hatua za uzembe mkubwa wa kimkakati na kiusalama.
 
Kuna panya alitafuna suti na kanzu yangu mwe sijui alitumwa na nani!
 
Wewe lijamaa ni liongo sana! Amezaliwa na KG1.2 na urefu SM70!!?

Ujue hiyo ni futi moja na theluthi acha kutufanya mambumbumbu
 
Sasa hizi nishani panya anazifanyia nini au ndo majambo tu ya walimwengu!!!
 
Unyanyasaji wa wanyama: “Panya Magawa hajawahi kukutana na panya wa kike, maisha ya mafunzo yali-focus kwenye kwenda kuokoa maisha ya watu kwa hiyo hakupata muda wa kukutanishwa na panya wa kike” - Dr. Pendo Msegu, mwalimu wa Panya Magawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…