Panya road waibua taharuki Mbagala

Hapo stendi hapakuwepo na wanaume?

Hivyo vitoto vitavamiaje stendi na kuanza kupiga na kupora watu?

Watanzania wengine ni watu wa ajabu sana. Yaani watu mpo stendi mnaachia vitoto viwapore na kuwapiga?

Wahshi kabisa!!

Mkuu Nyani Ngabu;
Nadhani maisha ya ughaibuni yamekukolea zaidi. Msemaji au mleta thread wetu kasema; Trafiki, yaani Polisi wenye nguo nyeupe walizivua na kubaki na singlend tu huku nao wakikimbilia maporini.
Yaani, wewe fikiri ni ajali ngapi zilitokea hapo baada ya kukosa maongozi ya magari kutokana na waoga kukimbia kutoka kituo cha kazi??
Wanaume wapo wengi tu lakini, Tz ukiua panya mmoja tu, wanasema; Umejichukulia sheria mkononi wao waumize watu tu wanalindwa. Maneno ya viongozi wetu watukufu ndo kinyaa kwetu. Mh. Afande Sirro alisema; Nimeshamaliza tatizo la panya rodi. Je hao mi misukule au mizimu ya kipanya rodi?? Tuweke akiba ya maneno. Kama hao wenye uwezo wa kudhibiti wanatimua mbio, mwanaume atatoka wapi?? Jibu kwako ni kuwa; Hakuna mwanaume darisalama acha Mbagala.
 
Aisee hao panya road wangehamishiwa hapo kwa kagame kwa wiki 1 tu, kama wangekuja kusikika tena.
Achana na ile ngome ya yule mtusi mkuu! Doria na misako yake mpaka unaogopa. Polisi na soja wana maredio yenye mkonga mrefu kama wacambodia wa Vietnam hawacheki na kima ni uso wa mbuzi tabasamu la ng'ombe mwanzo mwisho.

Kama RAIA wanagombana mtaani afu wazee wanakuja kombania saba...ahahahaha!
 

Hapana mkuu, tatizo MTU kama scorpion kajitolea kung'oa macho wajinga wamaume wa dar wanalalamika. Huku mkoani kwetu chuga tunapwila kabla ya kumtoboa macho. Pumbafu sana.
 
Wameshawahi gongo la mboto walivamia nyumba kadhaa na kuvunja milango

Halafu panya road ni general name ila hivi vikundi vina majina yao kiufupi mbagala wana camp yao,mtoni,tandale,manzese ,kigogo,kino,migo,mabibo nk mjumuisho ndio panya road ila kila camp wana majina yao wanajiita
 
Hata mimi ningekimbia viwembe vyauma sana mwilini
 
Hapo stendi hapakuwepo na wanaume?

Hivyo vitoto vitavamiaje stendi na kuanza kupiga na kupora watu?

Watanzania wengine ni watu wa ajabu sana. Yaani watu mpo stendi mnaachia vitoto viwapore na kuwapiga?

Wahshi kabisa!!
Wakati mwingine huwa hata hutafakari
Cha kwanza hao panya load walikuwa na silaha gani?
Pili ilikuwa saa ngapi?
Idadi ya watu ilikuwaje?? Approximation

ndo jambo la kwanza la kujua kabla ya kuongea.
 
Hahah asee pale hata panya hakatizi, mi najiulizaga chief hivi kwanini hata kwenye majiji yetu dar, mwanza wasingeamua soldiers wakawa wanapiga doria usiku kucha wako na full silaha tuone kama ujambazi na hao panya road watakatiza.
 
Mkuu kama unaweza kupambana na watu zaid ya 20 wenye mapanga bisibisi visu marungu pliz fanya uje utusaidie kuwaondoa hawa watoto[emoji28][emoji23]
Mkuu hapo stendi kuna zaidi ya mtu zaidi ya mmoja kwaiyo hapo ni kugawana mmoja mmoja.wakiingia mtaani wanagawana kila mmoja anaingia nyumba yake sasa hapo unashindwaje kupambana na mtu mmoja au wawili???km wakikifuata wakiwa 20 na vijivisu kama unavyosema kwakweli hapo nitauambia mguu sijawai kula nikakunyima kitu niokoe
 
Acheni kufukua makaburi.

Wanarudi upya hawa jamaa baada ya kubomolewa vibanda vyao
 
Mkuu; ukiwa Askari na likatokea tukio la ghafla(kushtukiza almaarufu kama Ambush) la HATARI ya UHAI pale ulipo, cha KWANZA ni kuhakikisha Usalama wako wewe kama Askari ndipo hatua zingine zifuate e.g. kama unavyosema- Adui yupo upande gani, wapo wangapi, wana silaha gani na ni silaha zenye uwezo gani etc.etc. na Uwezo wangu mm wa kukabiliana. Tofauti na hapo/ La sivyo Huyo askari atakuwa ni mzembe na yy ataongeza tu idadi ya majeruhi/waliouawa katika tukio. Kwa hiyo usishangae kuona Traffic kutimka mbio, kubadilisha muonekano wao n.k.n.k. ........hiyo ni sehemu tu ya mbinu za medani... Zingatia kwambaTraffic wenye kofia nyeupe mara nyingi hawabebi silaha. By the way mm sio polisi/askari ila nimepitia mafunzo JKT (Operation Tija) pale Mafinga JKT miaka hiyo ya Nineteen kweusi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…