Hapo stendi hapakuwepo na wanaume?
Hivyo vitoto vitavamiaje stendi na kuanza kupiga na kupora watu?
Watanzania wengine ni watu wa ajabu sana. Yaani watu mpo stendi mnaachia vitoto viwapore na kuwapiga?
Wahshi kabisa!!
Mkuu Nyani Ngabu;
Nadhani maisha ya ughaibuni yamekukolea zaidi. Msemaji au mleta thread wetu kasema; Trafiki, yaani Polisi wenye nguo nyeupe walizivua na kubaki na singlend tu huku nao wakikimbilia maporini.
Yaani, wewe fikiri ni ajali ngapi zilitokea hapo baada ya kukosa maongozi ya magari kutokana na waoga kukimbia kutoka kituo cha kazi??
Wanaume wapo wengi tu lakini, Tz ukiua panya mmoja tu, wanasema; Umejichukulia sheria mkononi wao waumize watu tu wanalindwa. Maneno ya viongozi wetu watukufu ndo kinyaa kwetu. Mh. Afande Sirro alisema; Nimeshamaliza tatizo la panya rodi. Je hao mi misukule au mizimu ya kipanya rodi?? Tuweke akiba ya maneno. Kama hao wenye uwezo wa kudhibiti wanatimua mbio, mwanaume atatoka wapi?? Jibu kwako ni kuwa; Hakuna mwanaume darisalama acha Mbagala.