Paulsylvester
JF-Expert Member
- Oct 15, 2021
- 1,464
- 3,379
Kundi la vijana wanaojulikana kama Panya road' limekuwa ni tishio kwa wananchi kwa siku za hivi karibuni!
Vijana hawa wamekuwa wakitishia usalama wa jamii na hata kufanya mauwaji mbalimbali kwa lengo LA kuiba na kupora kila kilicho mbele ya macho yao!
Tunapenda kulishukuru Jeshi la police kwa kuanza kudhibiti hawa vijana na kuanza kurudisha amani katika mitaa iliyokuwa ikivamiwa Mara kwa Mara kwa kuwakamata hawa vijana alimarufu kwa jina la Panya road
Mbali na kuwakamata, wengine wamekuwa wakipigwa risasi na kufa papo hapo, adhabu hii ndiyo inayopelekea kuuliza juu ya wezi wa Mabilion ya fedha za kodi za wananchi
Wezi hawa wa kodi zetu, ndio wauwaji wakubwa wa watu wanaokufa kwa kukosa huduma mahospitalini!
Watu wanaokufa kwa kukosa gari la wagonjwa ili tu kuwahi huduma katika hospital zetu kuu!
Wajawazito wanakufa kutokana na mtu mmoja tu kuiba kodi ambazo zingeondoa kero hiyo, halafu police wetu wana ng'aa ng'aa sharubu badala ya kutandika risasi liuwaji kama hilo
Badala yake, anauliwa kijana mwenye njaa tuu, kaiba kuku ili akale na wanae, anatandikwa risasi badala ya kukamatwa ili akajibu makosa yake
Ni lini yataanza kupigwa risasi majizi na mauwaji ya wananchi haya yanayoiba kodi zetu ambapo zingewezesha upatikanaji wa huduma nzuri mahospitalini na kuweza kupatiwa bima kwa watanzania wote?
La hatutaki kuwashuti hawa wezi wa mabilioni yetu, tusiwauwe na hawa wanaoiba Mchele ili wakakidhi njaa zao