SI KWELI Papa amesema kuwa Wakatoliki wale chochote wanachokitaka wakati wa Kwaresima kwa kuwa dhabihu haipo tumboni bali moyoni

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Wadau hamjamboni nyote?

Taarifa kamili hapo chini kwa kimombo:

“Eat whatever you want during Holy Week, the sacrifice is not in the stomach but in the heart.

People abstain from eating meat, but they do not talk to their siblings and/or relatives, they do not visit their parents and do not take care of their children.

They do not share their food with those who need it most, they distance their children from their father/mother and/or grandparents, they criticize the lives of others, mistreat their partner, etc. Meat does not make you a bad person, just as a fish fillet will not make you a saint.

Better to seek a good relationship with God by doing good to others. Let us be less arrogant and more humble of heart.”

Pope Francis
 
Tunachokijua
Papa Fransisko ni kiongozi wa kanisa Katoliki duniani kote ambaye alianza majukumu yake tarehe 13 Machi 2024 akipokea kijiti hiko kutokea kwa mtangulizii wake Papa Benedict wa 16. Wakristo huwa na mfungo wa siku 40 ukitanguliwa na siku ya jumatano ya majivu ukijulikana kama Kwaresma. Papa Fransisko amekuwa akitoa ujumbe wa pasaka kuanzia mwaka 2014.

Madai

Kumekuwepo na ujumbe unaosambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ukieleza kuwa Papa Fransisko ametoa ujumbe wake katika mfungo wa kwaresima akiwataka watu wale chochote katika kipindi hiki kwani mfungo siyo kufunga kula bali ni moyoni.

“Kula chochote unachotaka katika Wiki Takatifu, dhabihu haiko tumboni bali moyoni.

Watu wanajizuia kula nyama, lakini hawaongei na ndugu zao, jamaa zao, hawatembelei wazazi wao na hawawatunzi watoto wao.

Hawagawi chakula chao kwa wale wanaohitaji, wanawatenga watoto wao na baba/mama na/au babu zao, wanakemea maisha ya wengine, wanamtesa mwenzao n.k. Nyama haikufanyi wewe kuwa mtu mbaya, vile vile minofu ya samaki haitakufanya kuwa mtakatifu.

Afadhali kutafuta uhusiano mzuri na Mungu kwa kuwatendea wengine mema. Hebu tupunguze kiburi na tuwe wanyenyekevu zaidi wa moyo.”


Uhalisia wa Ujumbe huo

JamiiCheck imefuatilia na kubaini kuwa ujumbe huu unaosambazwa haujawahi kutolewa na Papa Fransisko na hivyo si wa kweli. Kupitia ufuatiliaji wa wa Jumbe za pasaka alizozitoa Papa kuanzia mwaka 2014 tumebaini hakuna ujumbe ambao papa aliongelea swala la watu kula chochote kipindi cha kwaresima. Tazama hapa kuona jumbe za papa Francis kuhusu kwaresma kuanzia mwaka 2014.

Ufuatiliaji pia umebaini kuwa ujumbe huo umekuwepo tokea Februari 2024, kutokea katika mtandao wa Facebook na baadae kusambazwa katika mitandao mingine ya ikiwemo X zamani, Twitter.

Ujumbe wa papa kuhusu kwaresima kwa mwaka 2025 kwenda kwa wakatoliki uliotolewa Februari, 6 una kichwa kinachosema “Tusafiri kwa pamoja kwa matumaini” ambapo katika ujumbe huo ameeleza ni kwa namna gani waumini wanaweza kushiriki katika safari ya matumaini. Tazama hapa
Tuwaulize wenzetu vipi?
Mtu unakuta amefunga ananuna hata ukimsalimia kama unamlazimisha. Funga gani hiyo?

Funga ipo moyoni kama kwenye msosi ni kuahirisha TU kula sio kufunga.

Haiwezekani ushibe vizuri saa 11 halafu ushinde TU Hadi 12 jioni uone ni bonge la ishu.

Ile ni kawaida., Kuna familia huko zinashinda njaa mlo ni mmoja tu kwa siku. Utawaambia nini kuhusu kufunga????

Kufunga ni moyoni na Kisha vile ulivyojinyima unavitoa kwa wengine wenye uhitaji.

Yaani kama umejinyima ile mchana basi Fanya umpe asiye nacho ale. Hiyo ndio ibada.

Sio unajinyima halafu SAA ya kufungua unakula kama fuko au saa 11 asubuhi unakula kama unaenda kuishi jangwani hutakaa upike Wala ule Tena?
 
“Eat whatever you want during Holy Week, the sacrifice is not in the stomach but in the heart. People abstain from eating meat, but they do not talk to their siblings and/or relatives, they do not visit their parents and do not take care of their children. They do not share their food with those who need it most, they distance their children from their father/mother and/or grandparents, they criticize the lives of others, mistreat their partner, etc. Meat does not make you a bad person, just as a fish fillet will not make you a saint. Better to seek a good relationship with God by doing good to others. Let us be less arrogant and more humble of heart.”

Pope Francis
 
Kufunga...? Ni fumbo sana

Naomba kila mtu na afanye yeye anachosemezana na Roho wa Bwana
 
Doh!

Kwani kufunga kukoje mkuu kati ya kushinda njaa na kutokula wala kunywa 24h?
Hakuna mkristo anaefunga hata masaa mawili , funga yenu ni kupumzika kula chakula flan, mtu anasema amefunga kula nyama, mwingine kafunga kula matembere ila vyakula vingine wanakula masaa yote kuna kufunga hapo? Migahawani muda huu wamejaa wakristo tupu
 
Mbona kama unateseka na ibada za watu.fanya yako ulio ambiwa na papa nq waache waslam nq imani yao
 
Mbona kama unateseka na ibada za watu.fanya yako ulio ambiwa na papa nq waache waslam nq imani yao
Wanafunga waislamu tu?!!!

Vipi mkuu ndugu yangu. Umeshiba makande sasa unakurupuka TU.
Walokole hawafungi?
Walutheri hawafungi?
Wahindu hawafungi?

Mbona huwaga mnajishtukia sana!??
 
Kwanini mleta mada asipigwe ban ya miezi kadhaa hata mwaka, kwa kuandika habari za chuki na uongo kama hii?
 
Funga yako wewe ni kuufanya usiku kuwa mchana

Kwa maana ya, wakati wengine wanalala na hawana bajeti ya kula usiku,wewe ndo kwanza unaamsha amsha, hulali unakula

Ni sawa tu na kusema, huli chakula mchana na badala yake unakula usiku wakati wengine wamelala

Hiyo ni funga kweli mkuu au kubadirisha ratiba ya kula?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…