SI KWELI Papa amesema kuwa Wakatoliki wale chochote wanachokitaka wakati wa Kwaresima kwa kuwa dhabihu haipo tumboni bali moyoni

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Wao wakila kitimoto sio shida ila walikuta mtu anakula Punda, Mmbwa, Panya au Fisi wanaanza kumsema vibaya sijui wanatumia andiko gani?
 
Wanafunga waislamu tu?!!!

Vipi mkuu ndugu yangu. Umeshiba makande sasa unakurupuka TU.
Walokole hawafungi?
Walutheri hawafungi?
Wahindu hawafungi?

Mbona huwaga mnajishtukia sana!??
Tupunguze unafiki angalau kipindi hiki cha Kwaresma!
 
Wao wakila kitimoto sio shida ila walikuta mtu anakula Punda, Mmbwa, Panya au Fisi wanaanza kumsema vibaya sijui wanatumia andiko gani?
Hii ni biblia:

📖 Marko 7:18-19
"Akawaambia, Hivi nanyi bado hamwelewi? Hamjui ya kuwa chochote kilichoingia ndani ya mtu kutoka nje hakiwezi kumtia unajisi; kwa sababu hakimwingii moyoni mwake, bali tumboni, naye hutoka kwenda chooni? – Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote."


📖 Matendo 10:13-15
"Kisha sauti ikamjia, Simama, Petro, uchinje ule. Lakini Petro akasema, Hasha, Bwana, kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu au najisi. Sauti ikamjia mara ya pili, Vilivyo safi vilivyotakaswa na Mungu, usiviviite wewe najisi."


📖 Warumi 14:3
"Yeye alaye asimdharau yeye asiyekula, wala yeye asiyekula asimhukumu yeye alaye; kwa maana Mungu amemkubali."


Kwa maandiko haya, Yesu mwenyewe alitangaza vyakula vyote kuwa safi, na Mungu alimfundisha Petro asihukumu chakula kwa sheria za Agano la Kale. Kwa hivyo, kula kitimoto si tatizo kwa mtu aliye huru katika Kristo. Kila mtu ana uhuru wa kula au kutokula kulingana na dhamiri yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…