Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 29,909
- 32,414
Baba Mtakatifu Fransisko ameridhia ombi la kustaafu Mhashamu Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa wa Jimbo la Iringa, na kumteua Padre Romanus Elamu Mihali wa Jimbo la Mafinga, kuwa Askofu mpya wa Jimbo la Iringa, leo tarehe 28/01/2025.
Mhashamu Askofu Mteule Romanus Elamu Mihali, alizaliwa tarehe 10/06/1969 Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa.
Baada ya masomo na majiundo ya kipadre, alipewa Daraja Takatifu la Upadre tarehe 13/07/2000 Jimboni Iringa, na kuhudumu katika nafasi mbalimbali za utume Jimboni Iringa. Mnamo mwaka 2010 alitunukiwa Shahada ya Uzamili, katika fani ya Sayansi ya Wanyama kutoka Chuo Kikuu cha Kerala nchini India.
Mhashamu Askofu Mteule Romanus Elamu Mihali tangu mwaka 2024 hadi sasa, amehudumu nafasi ya Makamu wa Askofu kwa Waklero Jimboni Mafinga.
Aidha, Mhashamu Askofu Mstaafu Tarcisius Ngalalekumtwa atakuwa Msimamizi wa Kitume wa Jimbo la Iringa, hadi Askofu Mteule atakapowekwa Wakfu na Kusimikwa Jimboni humo.
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, linamwombea Mhashamu Askofu Mteule Romanus Elamu Mihali afya ya mwili na roho katika utume huo mpya.
Imetolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania.