Papa Francis amtimua Askofu anayempinga kuhusu kuruhusu ndoa za jinsia moja, kutoa mimba na waliobadili jinsia

Siyo kweli. Maaskofu wenzake wanaofanya naye kazi ndio waliopendekeza aondolewe kwa sababu walizozieleza na pope alifanya endorsement tu kama anavyofanya kwa kumteua askofu maana pia huwa ni mapendekezo ya maaskofu nani awe askofu wa jimbo fulani na pope anafanya endorsement. Hata kuwa padri, wanajumuiya wakikubali na wanakigango chako/parokia yako unapendekezwa kwa askofu na kisha yanatolewa matangaza kwa miezi mitatu mfululizo kama kuna mtu mwenye kikwazo na ukishapita huo muda, basi muda wa kupokea mapingamizi unakuwa hakuna tena na hapo ndipo kinajana anapaingiwa ratiba ya lini atapewa daraja la upadri. Kila kitu kiko kwenye utaratibu. Hivyo, pope hawezi tu akaamua akamteua mtu fulani kuwa askofu au akamfukuza bila kufuata utaratibu uliopo kisheria (kwa mujibu wa canon law). Wewe chanzo chako cha habari ni BBC. Yaani habari za Kanisa Katoliki kuzitoa BBC ni kama za Chadema uzitoe gazeti la Uhuru, Mzalendo na Tanzanite.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…