Papa Francis ana mpango wa kuruhusu mapadri kuoa

Papa Francis ana mpango wa kuruhusu mapadri kuoa

Kwani mapadri kutooa ni agizo la nani? Ipo kwenye Biblia? Ni agizo la Mungu? Nini maana ya Padri kutoruhusiwa kuoa?
Ni agizo la kanisa katoliki, Biblia inamtaka Padre, Shemasi na Askofu ni lazima waowe.

1 Tim 3:2-3​

Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha.
 
Dk Matola PHD, hiyo 1 Timotheo 3:2-3 ni mafundisho ya Paulo, hebu tumuulize Yesu mwenyewe anasemaje kuhusu hilo katika Mathayo 19: 10-12?

Mathayo 19: 10... Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa.
11 Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa.
12 Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee.
 
Kuna wanawake watafaidi sadaka wazi wazi
 
Back
Top Bottom