Idadi ya washarika imeongezeka kwa wingi.. Majengo yanalemewa.. Piga picha pale Morogoro mjini kuna Wakatoliki zaidi ya laki mbili.. Je, sharika zilizopo pale Moro mjini zina uwezo wa ku accomodate waumini wote, iwapo wote wataamua kuhudhuria kwenye misa? Jibu ni hapana.. So kanisa linapaswa lihakikishe linakuwa na majengo ya kutosha ku accomodate angalau 75% ya waumini iwapo wote wataamua kuhudhuria ibada kwa siku moja.. Jiwekeeni lengo la kufikia huko.
Jumuiya msizifanye minyororo kwenye shingo za waumini.. Baseline standard ni 'Kuikumbuka siku ya Bwana na kuitakasa', yani Jumapili. Kuwalazimisha waumini na kuwa sanction wasio sali kwenye jumuiya Jumamosi huwa mnaitoa kwenye Biblia gani? Kwa nini mnaenda nje ya scope na kutaka kuligeuza kanisa kuwa kama la Kisabato?