Pape Sakho atimkia Ufaransa

Pape Sakho atimkia Ufaransa

Wabongo wajifunze kuchagua mawakala bora, unaweza ukakuta Wakala kampambania sana mchezaji wake kupata timu ulaya na mijitu kutoka Magharibi inajua kutumia hizi nafasi,Sakho akiacha utoto wake baada ya misimu miwili au mitatu anaweza akacheza League 1.
 
Wabongo wajifunze kuchagua mawakala bora, unaweza ukakuta Wakala kampambania sana mchezaji wake kupata timu ulaya na mijitu kutoka Magharibi inajua kutumia hizi nafasi,Sakho akiacha utoto wake baada ya misimu miwili au mitatu anaweza akacheza League 1.
Hewala...hapo kwenye utoto hapo..unaweza kukuta yuko kwenye sehemu ambayo anaweza kupambana lakini anajiangusha kumtegemea refaa
 
Screenshot_20230724-150250.png
 
Kuna yule ameeenda Arabuni kufanyakazi za Ndani kutoka Uto lkn anavyosifiwa sasa! Simba is Next Level Sakho aongeze Bidii atafika mbaliiii
Waarabu wanasajili wachezaji wa ligi kuu za Ulaya.

Sadio Mane anakwenda Uarabuni, Mbape naye Uarabuni, huna hoja unaleta viroja.
 
Mfano Agent atamchukua nani kumpeleka huko nje?
Kuna kijana ni mtoto wa rafiki yangu somebody Mabuyu, yule mtoto aliibuka kuwa mchezaji bora kwenye Copa coca cola iliyofanyika Brazil.

Lakini kilichoendelea kinasikitisha sana, kwakuwa alikuwa under age kuna mshkaji mchezaji wa zamani alikuwa anamsimamia lakini michongo hajui, kuna nchi kadhaa za ulaya ilibidi akafanye majaribio lakini hakuna kilichoendelea hata sasa sijui yuko wapi maana baba yake alishafariki.

Kwahiyo nakubaliana na point kwamba hatuna agents, kwa sababu haiwezekani eti Salama Jabir naye uambiwe naye ni agent, huu ni mzaha.

Agent ni zaidi ya kujuwa English language, agent ni lazima uwe lobbyist mzuri ikiwezekana na wewe unakuwa ña sub agent wako nchi mbalimbali ambaye anachukuwa commission kwako kwa kila deal.

Nimeliona hili nimefanya kazi kwenye tourist industry Bongo kwa muda mrefu nimejifunza mengi na kuwajuwa aina za watalii wanaokuja Tanzania.

Watalii matajili hawaji kutalii Tanzania kwa vikampuni vya kupost mitandaoni, ni lazima agent mzungu mwenzao wanayemuamini ndio anawaletea wageni na unakuta hizo kampuni Bongo ni za wazungu wenzao.

Watalii wa kawaida ambao ndio wanafikia YMCA mnakutana mpaka Kidimbwi hao ndio wanatembelea nchi kwa kutumia mitandao na kwa kifupi ni watu wa kawaida tu.

Hakuna Mtalii tajiri utakuja kukutana naye wavuvi camp never, safari zao zinaratibiwa kwa kuzingatia usalama, Tena mwingine hata Kilimanjaro hotel hafiki, anakuja na Private jet yake inapaki yeye anapanda charter plane anakwenda porini, siku ya kurudi akitoka Porini na charter plane anashuka kwenye ndege ndogo anapanda gulf stream yake bomba, unakuta tajiri Dar anaijuwa airport tu hajawahi kutoka nje ya airport ya Dar kwa miaka hata 20.
 
Back
Top Bottom