Mfano Agent atamchukua nani kumpeleka huko nje?
Kuna kijana ni mtoto wa rafiki yangu somebody Mabuyu, yule mtoto aliibuka kuwa mchezaji bora kwenye Copa coca cola iliyofanyika Brazil.
Lakini kilichoendelea kinasikitisha sana, kwakuwa alikuwa under age kuna mshkaji mchezaji wa zamani alikuwa anamsimamia lakini michongo hajui, kuna nchi kadhaa za ulaya ilibidi akafanye majaribio lakini hakuna kilichoendelea hata sasa sijui yuko wapi maana baba yake alishafariki.
Kwahiyo nakubaliana na point kwamba hatuna agents, kwa sababu haiwezekani eti Salama Jabir naye uambiwe naye ni agent, huu ni mzaha.
Agent ni zaidi ya kujuwa English language, agent ni lazima uwe lobbyist mzuri ikiwezekana na wewe unakuwa ña sub agent wako nchi mbalimbali ambaye anachukuwa commission kwako kwa kila deal.
Nimeliona hili nimefanya kazi kwenye tourist industry Bongo kwa muda mrefu nimejifunza mengi na kuwajuwa aina za watalii wanaokuja Tanzania.
Watalii matajili hawaji kutalii Tanzania kwa vikampuni vya kupost mitandaoni, ni lazima agent mzungu mwenzao wanayemuamini ndio anawaletea wageni na unakuta hizo kampuni Bongo ni za wazungu wenzao.
Watalii wa kawaida ambao ndio wanafikia YMCA mnakutana mpaka Kidimbwi hao ndio wanatembelea nchi kwa kutumia mitandao na kwa kifupi ni watu wa kawaida tu.
Hakuna Mtalii tajiri utakuja kukutana naye wavuvi camp never, safari zao zinaratibiwa kwa kuzingatia usalama, Tena mwingine hata Kilimanjaro hotel hafiki, anakuja na Private jet yake inapaki yeye anapanda charter plane anakwenda porini, siku ya kurudi akitoka Porini na charter plane anashuka kwenye ndege ndogo anapanda gulf stream yake bomba, unakuta tajiri Dar anaijuwa airport tu hajawahi kutoka nje ya airport ya Dar kwa miaka hata 20.