JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Inaelezwa kwamba fedha hizo anazotuhumiwa kuziiba zimetokana na mirathi ya shemeji yake.
Kesi hiyo namba 44 ya mwaka 2022 imesomwa na hakimu Mariam Luselwa katika Mahakama ya Mkoa wa Manyara.
Kesi hiyo inawakabili washtakiwa wa tatu ambao ni Sule pamoja na watumishi wawili wa Benki ya NMB, Cynthia Nyamtiga (27) na Winfrida Rwakilomba (30) kwa pamoja wametajwa mahakamni hapo kuhusika na kesi hiyo.
Imeelezwa Mahakamani hapo, Paroko Baltazari anakabiliwa na makosa mawili, kosa la kwanza wizi kinyume na kifungu namba 258 kifungu kidogo cha kwanza na kifungu namba 265 vya kanuni ya adhabu sura namba 16 marejeo kama ilivyofanyiwa marejeo ya 2022.
Washtakiwa wengine ni watumishi wawili wa Benki ya NMB, Cynthia Nyamtiga pamoja na Winfrida Rwakilomba, ambapo Hakimu Mariam Luswelwa ameiambia mahakama washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na kosa la kushindwa kuzuia utendekaji wa kosa kinyume na kifungu 383 na kifungu cha 35 vya kanuni ya adhabu sura 16 kama ilivyofanyiwa marejeo 2022.
Washtakiwa hao watatu wamekana kutenda mashtaka yanayowakabili wote watatu wapo nje kwa sharti la kuwa na mdhamini mmoja kwa kila mshtakiwa na bondi ya milioni saba kwa kila mdhamini.
Shauri hilo limepangwa tena tarehe Desemba 21, 2022 kwa ajili ya kusomewa hoja za awali.
Chanzo: EATV