PAROKO: Tusikae kimya sasa kusubiri Miaka 10 ijayo Rais wetu aandike Kitabu cha kujutia kuingia mkataba huu mbovu wa Bandari.

PAROKO: Tusikae kimya sasa kusubiri Miaka 10 ijayo Rais wetu aandike Kitabu cha kujutia kuingia mkataba huu mbovu wa Bandari.

Mafanikio yapi na Dola imekuwa finyu?

Au siku hizi Wazungu na watalii wanakuja na Pesa ya madafu ya TShilings?

Namba hazidanganyi.
hizo Finyu zimepatikana chini ya kitanda chako? si ndio hizo wameleta, au hujui jana Ma Bank yamekomba mamilioni ya dola toka Bank kuu kuwezesha miamala?
Nchi jirani wanavuka mpaka kuja kugombania dola za Marekani na ndio sababu Serikali ikadhibiti ili kulinda upatikanaji wake …tatizo mlikimbilia kuvaa uanaharakati kabla ya elimu sahihi ya masuala mnayotaka kujadili
 
Hoja ipi? ya kusema hawataki kabisa uwekezaji kwa kigezo kuwa tunayo local capacity?…hiyo hoja angeisema Gwajima au Mwamposa ningemuelewa kwa kuwa ana autonomy ya kuongoza kanisa lake 100%, hao wengine kila kitu wanategemea Muongozo kutoka Ulaya halafu wanashangaa Serikali kualika wawekezaji wa nje?

inakuaje huu uchungu wa Bandari hawakuwa nao wakati migodi ikibinafsishwa kwa wazungu?
Maaskofu wamemtendea vibaya sana Rais Samia na ameamua kukaa kimya tu maskini. Wamemkwaza na kutaka kumtisha labda wakijua ataogopa kwa sababu ni mwanamke.

Wameshindwa kuitazama picha pana ya masuala ya shoroba haswa hii vita ya kiuchumi ya ufaidikaji wa nchi kupitia bandari tulizonazo.
 
Acg
hizo Finyu zimepatikana chini ya kitanda chako? si ndio hizo wameleta, au hujui jana Ma Bank yamekomba mamilioni ya dola toka Bank kuu kuwezesha miamala?
Nchi jirani wanavuka mpaka kuja kugombania dola za Marekani na ndio sababu Serikali ikadhibiti ili kulinda upatikanaji wake …tatizo mlikimbilia kuvaa uanaharakati kabla ya elimu sahihi ya masuala mnayotaka kujadili
Acha porojo
 
Leo ikiwa ni Wiki ya Pili ya Tamko la Maaskofu kusomwa Makanisa yote ya Roman Catholic, nimevutiwa na Maneno aliyoyaongea Paroko mmoja kwenye Ibada " Tusikae kimya sasa kusubiri miaka 10 ijayo Rais wetu aandike Kitabu cha kujutia kuingia mkataba huu mbovu wa Bandari, tumkosoe mapema ili akija kuandika kitabu hicho aseme nilishauriwa ila nilikataa Ushauri"

Amenukuu Maneno yaliyopo kwenye Kitabu cha "My Life, My Purpose" cha Hayati Benjamin Mkapa alipojutia mambo mbalimbali ya Ovyo aliyoyafanya wakati wa Utawala wake ikiwemo kashfa maarufu ya EPA "Wahuni walitumia uaminifu wangu kwa chama kunishawishi nikubali Ninajisikia kuwa nilitumika na kusalitiwa..."

"Kama Wahuni waliweza kumlaghai Rais Mkapa kuingia Mikataba ya ajabu basi hawawezi kushindwa kumlaghai Rais Samia kwamba Mkataba huu una tija"

SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU
Huyu wa kwetu atasema makamaba na mwigulu ndo waliomshauri vibaya
 
Acg

Acha porojo
Soma ili uwe mwanaharakati mwenye vision badala ya kujidanganya kila kitu kinasubiri Katiba Mpya

Dunia nzima kuna uhaba wa dola kutokana na kuongezeka riba Marekani pamoja na Marekani kuchuka hatua yake ya kufanya treasury Management kulinda fedha yake lakini bado Nchi ipo salama tunapata kila kitu hata Chama chako kinazunguka mikoani wanajaza mafuta unadhani yale mafuta yananunuliwa kwa kwacha ya Malawi ?
 
Na umefuata njia sahihi kwenda bungeni. Nchi yenye watu wenye kujielewa ingekuwa imeshaachana na kina Mwabukusi mara tu baada ya kushindwa kesi kule Mbeya.
Nyie mna tabia za vinyonga mnabadilika kulingana na Mazingira.
Kesho Samia akitangaza kufuta mkataba huo mtaitisha Press kumpongeza kwa kusikia Sauti ya watu
 
Hii nchi itakuja kukaa Sawa kukiwa na uwajibikaji. Hili swala watu wanakosea wanaachwa wanadunda mitaani ni janga kubwa Sana

Leo hii ukimuuliza Kikwete akwambie faida ya gesi ya Mtwara aliyoenda kuichukua kwa mitutu ya bunduki sijui atajibu nini na bado ndio kwanza anajengewa bangaloo pwani baharini aishi kwa Amani. Hawa watu wanatakiwa wawajibishwe kwa matendo yao ili wengine waogope hata kujaribu. Hivi hadi leo ukimuuliza Kikwete hela za Escrow ni za serekali au si za serekali atajibu nini?

Magufuli kaharibu biashara ya korosho kusini yote ikazimika na nchi ikakosa mapato. Kaharibu biashara ya maduka ya kubadilishia fedha leo hii msemaji wa serekali aliyekuwa mstari wa mbele kusifu na kuabudu anasimama mbele ya vyombo vya Habari anasema tumerudisha bilioni 9 zilizonyang'anywa bureau de change, hivyo tu yaani. Just hivyo tu!

Huyo Mkapa anajifanya kujutia kwa kuandika kitabu, hivi Kuna mtu alikuwa mbabe kama Mkapa Enzi zake? Aliambiwa mara ngapi kuhusu ishu ya EPA mnakumbuka maneno yake ya ubabe aliyokuwa anayatoa? Kitabu makaratasi hayo sisi yanatusaidia nini sasa hivi baada ya Ile hela kupigwa?

Tutafanyana wajinga hadi lini hivi?
Wahuni wameshaatajirikia ,utasikia mwizi anatetewa kuwa samia anawaonea watu ,sijui anavunja haki za binadami , due process haikufuatwa, R I P jpm
 
Nyie mna tabia za vinyonga mnabadilika kulingana na Mazingira.
Kesho Samia akitangaza kufuta mkataba huo mtaitisha Press kumpongeza kwa kusikia Sauti ya watu
Hawezi kufanya hivyo kwani atakwenda kuua uchumi mzima wa nchi hii. Usidhani kinachofanyika muda huu ni matokeo ya maamuzi ya jana au juzi.
 
Hawezi kufanya hivyo kwani atakwenda kuua uchumi mzima wa nchi hii. Usidhani kinachofanyika muda huu ni matokeo ya maamuzi ya jana au juzi.
Rais Mkapa alishasema Wahuni sio watu, Mlimpotosha.
Sasa mmehamia kumpotosha Samia
 
Hakika, alilosema Paroko ni jambo la msingi sana, inaonekana imekuwa style ya viongozi wa nchi hii, kila wakiharibu kwenye awamu zao, wanasubiri muda wao ukishamalizika ndio watunge vitabu kujuta kwa maovu waliyotufanyia.
Kikwete alisema atakuwa rais wa mwsho kuongoza nchi maskini kikowapi
 
Back
Top Bottom