Pasaka hii twende tukapumzike Kisiba Campsite. Hautojutia, wewe na umpendaye

Mm hilo ziwa kwa story zake nimetokea kuliogopa..sijui kwanini..huwa naona kibao cha kuelekeza uelekeo wake..mwaka huu naweza kuja na familia tupaone panafananaje..
Zamani tulikuwa tunasimuliwa kuwa hilo eneo lilikuwa kavu tu yaani lilikuwa halina maji. Ikatokea siku moja Mtu mmoja wa Kabila la Wakinga alikuwa safarini alipita hayo maeneo akiwa na kiu ya maji na njaa, akawaomba watu wa eneo hilo wampe chakula na maji wakamtolea nje ila mtu mmoja katika watu wote wa eneo hilo ndiye alimpa chakula na maji Mkinga huyo. Basi mara baaada ya kupata chakula na kunywa maji Mkinga akamwambia mwenyeji wake huyo ahame eneo hilo maana atawaangamiza wale watu wote waliomnyima chakula na maji. Ndio ikatokea hivyo wakaangamizwa kwa kuletewa maji na kuzamishwa kwenye maji hayo. Ndio ukawa mwanzo wa hiyo kitu Kisiba. Hizo zilikuwa simulizi za Bibi zetu enzi hizo. Funzo la simulizi hiyo ni kuwa Tusiwe Wachoyo hasa kwa Wageni.
 
Hivi kwani Wanyakyusa ni wachoyo?
 
Hebu taja majira rafiki bhana manake Rungwe na yenyewe ina sifa sana manake usikute kuna majira ukipiga mbizi, unaanza ku-freeze huko huko ndani.
Mwezi wa sita na wa saba ndio kuna baridi sheikh. Pasaka haiwi miezi hiyo
 
Hujazungumzia malazi na chakula ? Au lazima sisi watalii tufanye day trip na lunch box zetu?
 
Mbeya never disappoint ni vile Utalii wa Tanzania wamekariri huko Arusha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…