Amani kwenu nyote
Yesu Kristo alipofufuka kwa wavu mara baada ya kulala Karubini kwa siku 2, alifufuka siku ya 3 na neno lake la kwanza wa binadamu wenye hofu na mashaka ni Amani iwe kwenu...Peace on Earth. Aliwatakia amani mitume wake kwa sababu walikuwa wanatafutwa na utawala wa Rumi kama walivyomkamata yeye (Yesu) na kumtesa kwa kisingizio cha kujitangazia ufalme wa Uyahudi
Takribani siku 5 hivi kumeibuka mijadala mikubwa ikiwahusisha viongozi wakubwa wa Kisiasa kujibu HOJA za CAG hasa ile ya Trilion 1.5 ambayo CAG ameshindwa kuona matumizi yake wala viambatanisho wakati yatari imetumika.
Kwa kuwa Paschal Mayalla ni mchambuzi mzuri wa ukweli - Truth na kwa kuwa haogopi kuisema kweli popote kwa sababu itatuweka huru nasi tutakwa huru kweli nimeona ni vyema kuulizia afya yake maana hajasomeka maoni yake nasi wasomaji wake waaminifu hasa tuliosoma naye tumeshidwa kujua ukimya wake maana yake nini?
Trilion 1.5 kukosa maelezo kulitosha kabisa kumwajibisha mlipaji Mkuu wa hazina kwa sababu ndiye anayeidhinisha malipo yote ya serikali; HAIWEZEKANI ,HAIKUBALIKI na HAIVUMILIKI Mkuu wetu wa Nchi anayefnaya juhudi kubwa kwa maarifa yote kuijenga Nchi na kuinyoosha aje aaibishwe kwa kashifa kubwa namna hii.
Hivyo basi naombeni aliye karibu na Paschal amwambie aje ajibu hoja naye, aeleze msimamo wake upo upande gani? maana tumeshamsikia CAG,ZZK, Polepole na bado wale wa upande wa Pili, labda ndio wamezikwapua? Kimya chao kinatoa tafsiri gani?
Dunia itakuwa mahali pa hatari kuishi kama wale wema watakaa kimya dhidi ya ubaya unaotendwa
Martin Luther King Jr aliwahi kusema kuwa Ni mwanga tu ndio wenye uwezo wa kuondoa Giza na kamwe giza haliwezi kuondolewa kwa kuongeza giza nene
Bill Graham naye alisema kuwa Mwanga wa muhimu sana ni ule mdogo utakaokusaidia kumwona Nyoka karibu na Miguu yako