Pascal Mayalla ahojiwa na kamati ya Bunge

Pascal Mayalla ahojiwa na kamati ya Bunge

Mwandishi wa kujitegemea, Ndg. Pascal Mayala (katikati) akihojiwa na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa kosa la kuandika habari yenye maudhui ya kudharau Bunge kwenye safu yake ya gazeti la Rai Mwema

Amefika hapo ikiwa ni baada ya Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai kuagiza Ndg. Pascal Mayala pamoja Wahariri wa Gazeti la Raia Mwema wafikishwe mbele ya kamati hiyo.

Habari zaidi, soma => Spika aagiza mwandishi Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la Raia Mwema wahojiwe kwa kulidhalilisha Bunge
Ona yalivyokaa kumbe mapigaji tu
 
Nimeangalia ‘swali lako’ & avatar yako;kweli mnaendana...unaachaje kumfahamu Pascal mayalla humu jukwaani,au wewe nawe ni ‘kibaraka’ wa kina nanilii!
Hata nami namshangaa huyu ndugu...Paskali wa JF hamujuwi? Yule ambaye walisema kwao jina hilo ni NJAA, badala ya kujibu swali (lenye mfumo wa KITI MOTO).
 
Pascal ana hoja.
Hi tabia ya kuzuia kuambiwa naona imekithiri sana.
Ni kweli kuwa muhimili wa bunge unaingiliwa sana. Mfano halali ni pale mkuu wa kaya alipomwambia spika awashughulikie wapinzani ndani ya bunge, wakitoka nje ana deal nao. Ile ni kama amri na imeingilia madaraka ya spika.


Tanzania inapotea kidemokrasia
Wapinzani watataabika bali maendeleo hayatapatikana Mungu yupo na amesikia kilio chenu!
 
Back
Top Bottom