Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Mwandishi wa kujitegemea, Ndg. Pascal Mayala (katikati) akihojiwa na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa kosa la kuandika habari yenye maudhui ya kudharau Bunge kwenye safu yake ya gazeti la Rai Mwema
Amefika hapo ikiwa ni baada ya Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai kuagiza Ndg. Pascal Mayala pamoja Wahariri wa Gazeti la Raia Mwema wafikishwe mbele ya kamati hiyo.
Habari zaidi, soma => Spika aagiza mwandishi Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la Raia Mwema wahojiwe kwa kulidhalilisha Bunge
Hii iishie humu humu jf, ikitoka tuu nje, ikachapishwa na gezeti lolote, jiandae kuitwa Dodoma!.Asalaam Tanzania! bilashaka mmejibu kazi iendelee.
binafsi nimehuzunishwa sana na kauli ya SPIKA akiwa bungeni siku ya alhamisi tarehe 8/4/2021 yakuwa
"MKUBWA akishasema wengine inabidi tukae kimya"
Aliyasema hayo akirejea maoni yake kuhusu ujenzi wa bandari ya bagamoyo ambapo alisema rais alishauriwa vibaya.
Kiukweli kauli hii inaonesha udhaifu MKUBWA katika taasisi ambayo ilipaswa kuheshimika na kusikilizwa sana! Taasisi ambayo ni mhimili mkuu, taasisi ambayo inapaswa kuisimamia serikali, kutunga sheria na kutupa bajeti bora kwa maendeleo ya kweli kwa taifa letu.
Kistaarabu kauli ile (YA AIBU) ilipaswa kufutwa kwenye Hansard kwani inawafundisha wabunge ambayo wengine niwageni sio tuu kutoshauri kitu mkubwa (rais) akishakiongea! Bali kuwa waoga! bubu! na kutowasilisha matakwa ya wananchi waliowachagua!
Endapo kiongozi wako ananyamazishwa wewe uliye chini yake utasema nini?
Na huu ni uthibitisho mwingine yakuwa serikali ililiweka bunge mkononi na kuliamulia vyakusema, kwa bunge la namna hii tusitarajie maendeleo hili ni 'rubber stamp' ya nini serikali inataka.
Si ajabu sasa kuona wooote waliokosoa serikali waziwazi wametupwa pembeni kwenye uchaguzi wa aibu wa 2020. Sio ajabu kusema wabunge wa upinzani kupitia viti maalumu kuingia bungeni litakuwa ni agizo toka kwa MKUBWA kwenda kwa MDOGO.
Mhimili umegeuka sio mhimili tena,haustahimili kulibeba taifa na hauwezi. Udhaifu huu ni lazima tuuongee bila kukubali kuogopa vitisho na mateso yanayoweza kutekelezwa juu yetu! Tupaze sauti tulikatae.
BUNGE LA AIBU, AIBU, AIBU TUPU!
Usije kusema hukujua, niulize mimi mwenzio, yalinikuta yepi?.
P