Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Mkuu Zawadi Ngoda, kiukweli jf ni kubwa sana!, huwezi amini, huu uzi ndio nauona leo!. Thanks, I feel honored!.Pascal Mayalla aliandika "Ingekuwa ni amri yangu, ningemwambia tuu naniliu aamue 2020 asigombee his second term, na badala yake, ampishe ili awe huyu mama!.
Mungu ambariki sana Mama Samia na kuwabariki wanawake wote leo siku ya Wanawake Duniani." -Paskali. Hii aliiandika hapa JF Mar 9, 2017.
Hivyo wanaosema Pascal Mayalla kabadilika baada ya Mh hayati Magufuli kufarika, hawakuutambua msimamo wa Pascal kuhusu Mama Samia hata wakati wa uhai wa Magufuli. Katika Thread hiyo yenye kichwa cha habari "Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth" Pascal kazianisha kwa kirefu sifa za Mama Samia zinazomfanya kuwa na uwezo wa kuwa Rais wa JMT. Binafsi nimezipitia tena mara 3 na kumpa Pascal 5.
Kuanzia sasa hivi sitapuuzia maandiko yako hapa JF, KWANI YANA WELEDI MKUBWA NA MAONO ya huko mbeleni.
Thread 'Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!' Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!
Na kuhusu Samia, sio uzi huu tuu pekee nilimzungumzia,
Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!
Samia nilianza nae 2010 kwenye uzi huu
New Cabinet: Baadhi ya Majina ni Haya Hapa!
Wanabodi, Bado niko hapa mjini Dodoma, nikijivinjari katika viwanja vya Bunge kwa haya na yale. Japo mpaka sasa kitendawili cha Waziri Mkuu bado hakijatenguliwa, nimeonelea niwatajie baadhi ya majina mapya kwenye new cabinet. 1. Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka. Huyu ndie mbunge mwenye...
"Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza
Wanabodi, Niko kwenye voluntariy lockdown, hivyo leo nimepata fursa ya kuangalia TV ya Zanzibar, ZBC, Mwandishi wa habari wa CCM Zanzibar, Daudi Ismail anamhoji Makamo wa Rais wa JMT, Mhe. Samia Suluhu Hassan anauzungumzia Muungano, kiukweli huyu Mama Samia anauzumguza vizuri muungano huku...
Pia hapaKwa hoja za muungano Mama Samia alizoshusha, ningekuwa ni uwezo wangu, ningeshauri October 2020, Mama Samia ndiye ampokee Dr. Shein kule Zanzibar, ili 2025, aje ampokee Magufuli, maana kwa maoni yangu, kwa uongeaji huu, huyu mama ndiye Mzanzibari pekee anayekubalika kuweza kuchagulika kuwa rais wa JMT kutokea Zanzibar, vinginevyo Wazanzibari wausahau kabisa urais wa Muungano, wao mwisho wao ni umakamo wa rais pekee.
Kwa hoja kama hizi za huyu mama Samia, kama age sio issue sana, si huyu mama atatufaa sana 2025 au tuwashauri kwa vile Magufuli analamika sana kuhusu urais, mara ni mateso, mara ni kazi ngumu, mara ni mzigo mzito, tumshauri rais Magufuli, kwa vile Samia anatosha sana, hivyo tumpunguzie mateso, hana haja ya kuendelea na mateso, mzigo mzito na kazi ngumu ya urais, na hata kama ni wale tausi au wanyama wa Magogoni, au yale majabali ya Chamwino, tutamjengea Chato na kumuomba bora apumzike tuu mapema, na kumpisha Mama Samia ndio amalizie ngwe yake iliyobakia?.
Paskali
Siku ya Wanawake Duniani: Je, tuna Wanawake wenye sifa za Presidential Material?
Wanabodi, Leo ni Siku ya Wanawake Duniani, katika safari ya kuelekea usawa wa kijinsia, kuna wanawake wengi wenye sifa na uwezo, lakini wamenyimwa fursa za kushika nafasi za juu kisiasa kutokana na nyingi ya nafasi hizo, kuhodhiwa na wanaume, katika kitu kinachoitwa "mfumo dume!" Swali ni je...
Ni katika kunikumbusha tuu, hotuba ya Rais Samia UN, imezidi kudhihirisha I was dam right nilipoyasema haya!.
P