Pascal Mayalla amchambua Dkt. Bashiru, adai aliandaliwa kuwa Rais 2025

Marehemu alikuwa anatuandalia watu wa ajabu ajabu .. eti Makonda awe waziri mkuu, Sabaya awe waziri mambo ya ndani - kutakuwa na nchi hapo ndugu zangu.
Hivi akifufuka na kukuta mabadiliko yote haya si atamvua uanachama Rais Samia?
 
The game is on again
Duh...!. Umenikumbusha mbali
Pl
 
Quote "Mayala amedai pia haoni njia ya Bashiru kufufuka tena kisiasa na ndiyo hivyo Mama Samia Suluhu ameshampoteza na Wana CCM wamefurahi mno." EOQ.

Hayo aliyasema Paskali wakati ule. Kwa sasa katika haya yaliyojitokeza jamaa ndo wamefurahi kupitia kiasi. Je, atakwepa kitanzi hiki ambacho kinaning'inia shingoni mwake. Tusubiri tuone.
 
Mayala amedai pia haoni njia ya Bashiru kufufuka tena kisiasa na ndiyo hivyo Mama Samia Suluhu ameshampoteza na Wana CCM wamefurahi mno.

Source: Radio DW Swahili, Leo mchana saa Saba, 01/04/2021.
Ni katika kukumbushana tuu!.
Mkuu MKEHA , ni kweli wakati wa uteuzi nilikuwa likizo, ila wakati wa utumbuzi nilitoa uchambuzi, BBC, DW na VOA Ubunge wa Bashiru Ali, wachambuzi wanasemaje? | DW | 01.04.2021
Na kwa vile mimi ni muumini wa freedom of expression, kweli hili la sasa la Dr. Bashiru, nimempa ushauri ufuatao Dr. Bashiru, If you are a man of Principles, Hata Wakushukie vipi Stand Firm!, Don't Apologize!, Utaheshimika Zaidi na Zaidi!
P.
 
Msimubeze Pascal ndiye alimutabiri Marehemu John Joseph Pombe Magufuri kuwa Rais. Wana Jamii Forum tumesahau?
Mkuu Anania Stephen Byarugaba, sio hii tuu ya JPM, Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli, jee uliwahi kuiona hii ya Samia?,
Hii ni kauli umba ya kumuumbia mtu urais wa JMT.

na hili "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza
Angalia kwa makini hii kauli umba hapa iliumba nini?
Hapa kuna mtu ameumbiwa urais wa JMT kwa kauli tuu, na hapa unaweza kuzishuhudia kauli umba mbalimbali

Kubwa kuliko, ni hii ya rais wa JMT 2025,
Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke, anza kuiweka hii akiba, 2025 tutakumbushana na tutaheshimiana!.

P
 
Pascal bado anaamini Tanzania ina chama kimoja cha siasa na itaendelea kuwa hivyo chini ya udikiteta wa CCM hivyo Bashiru hawezi akaibukia kwingine! Kwa maoni ya Pascal mama Samia tayari amepitishwa kuwa rais 2025 na CCM imekwisha sema imeandaliwa fomu moja tu ya mgombea urais, je, tutashuhudia tena watu wakitoweka?
 
Pascal bado anaamini Tanzania ina chama kimoja cha siasa
This is very true, Tanzania tuna chama kimoja tuu cha siasa ambacho ni capable na credible kwa huku Bara, ila Zanzibar kuna vyama wiwili, CCM na ACT-Wazalendo
CCM sio tu ni chama tawala, bali pia ni chama Dola!
na itaendelea kuwa hivyo chini ya CCM
This is also true, CCM itatawala milele!. Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!.
hivyo Bashiru hawezi akaibukia kwingine!
This is true kwasababu hakuna kungine!. NB. Japo Dr. Bashiru ni political scientist, huyu sio politician, huyu ni a technocrat!.
Kwa maoni ya Pascal mama Samia tayari amepitishwa kuwa rais 2025
Sii kweli, nimesema naunga mkono 2025 twende na mwanamke, ila sio lazima Samia!
Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye! ila pia kuna hii sauti Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
CCM imekwisha sema imeandaliwa fomu moja tu ya mgombea urais
True, huu ndio utaratibu wa CCM kwa urais mid term, inatolewa fomu moja tuu kwa incumbent
je, tutashuhudia tena watu wakitoweka?
Kwa vile walikuwa wanatoweshwa na wasiojulikana, hili siwezi kulisemea!.
P
 
Pasco nae kachemka, Bora angesema Hussein Mwinyi ndio alikuwa anaandaliwa na mwendazake
 
"Aliandaliwa kuwa Rais", inazidi kuthibitika sio wananchi wanaoamua nani awe Rais wa hii nchi, ni kikundi kidogo cha watu ndio kinatuchagulia Rais wamtakaye.
Wakati mwingine huwa najiuliza kama ni sahihi kuwaachia wananchi waamue wenyewe mambo mazito kama kumchagua rais wa nchi.

Siamini kwamba vijana kama wale waliodeki barabara lowasa apite kwenye njia safi wanastahili kuwa wapigakura.

Kanisa katoliki wangekuwa na utaratibu wa kila muumini wao kuwa na haki kumchagua papa, kungekuwa vurugu zisizokwisha huko.
 
Asante kwa kuhariri nilichokiandika kwa kuiruka sifa ya u great dictator, kutoamini haki ya anayetaka apate haki. Nilizaliwa nikiwa British subject chini ya mfalme wa uingereza baadae malkia mpaka tunapata Uhuru nikatelekezwa Tanganyika nikiwa ninamatumaini makubwa japo sikuteswa na malkia. TAA(TANU) na vyama vingine vya kina Mtemvu havikusurubiwa na malkia kama unavyotaka wewe vilivyopo visurubiwe! Malkia alivipa haki ya kujieleza mbele ya wananchi wake na akatupa Uhuru japo hakuwa mtawala wetu kwani tulikuwa chini ya Legue of Nations baadae UNO.
Umehariri sifa moja kubwa pendwa kwa sababu inakutia doa japo unaipenda sana, ingekuwa vizuri nayo ungeichambua kama ulivyochambua mengine. Hebu fikiria dunia ingekuwa vipi endapo watu wote tungekuwa na fikira moja ya ndiyo kwa kila jambo, nadhani tusingependa kuishi.
Nakusihi tu jutia mateso waliyoyapitia usiowatambua japo si ndugu zako ila kwenye maziko yako watakuwepo nawe hautawafukuza.
 
Ila Siasa mapito, leo Bashiru anaonekana adui
 
Nikuakishishie Freed Freed, ikitokea leo wewe ni Rais wa nchi hii, huyu ndugu Paskali atadai wewe ni Rais bora kuliko Rais yoyote aliyewai kutokea Tanzania. Imekuwa kawaida yake kusifia hadi kupitiliza kwa yeyote anaekuwa madarakani.
 
Nikuakishishie Freed Freed, ikitokea leo wewe ni Rais wa nchi hii, huyu ndugu Paskali atadai wewe ni Rais bora kuliko Rais yoyote aliyewai kutokea Tanzania. Imekuwa kawaida yake kusifia hadi kupitiliza kwa yeyote anaekuwa madarakani.
Na ndivyo itakavyokuwa aaaaaahhhhhhaaaaahhhh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…