Pascal Mayalla amchambua Dkt. Bashiru, adai aliandaliwa kuwa Rais 2025

Pascal Mayalla amchambua Dkt. Bashiru, adai aliandaliwa kuwa Rais 2025

Marehemu alikuwa anatuandalia watu wa ajabu ajabu .. eti Makonda awe waziri mkuu, Sabaya awe waziri mambo ya ndani - kutakuwa na nchi hapo ndugu zangu.
Hivi akifufuka na kukuta mabadiliko yote haya si atamvua uanachama Rais Samia?
 
Mwana JF nguli, Akihojiwa Radio DW Pascal Mayala, amemchambua Dr Bashiru. Amesema Dr Bashiru kapata ajali kubwa sana kisiasa na hatoinuka tena. Pia kadai Magufuli amiini usiamini alikuwa akimwandaa Dr Bashiru kuwa Rais 2025.

Mayala amedai Dr Bashiru aliyeibukia kuwa Katibu Mkuu wa CCM baada ya kuhakiki Mali za chama hicho alichukiwa mno kutokana na style yake ya uongozi.

Amesema amekinyoosha mno chama hadi kupitiliza na kusababisha kuchukiwa mno kuliko Katibu Mkuu yeyote katika Historia ya CCM. Pia amedai Dr Bashiru ni mjamaa mno au Mnyerere na Marehemu Magufuli alimkubali na kumpenda Sana na alipanga kumuachia Urais 2025.

Mayala amedai pia haoni njia ya Bashiru kufufuka tena kisiasa na ndiyo hivyo Mama Samia Suluhu ameshampoteza na Wana CCM wamefurahi mno.

Amesema kwa uhakika utawala wa Mama Samia Suluhu atakuwa Rais mzuri Sana kuliko Rais Magufuli.

Source: Radio DW Swahili, Leo mchana saa Saba, 01/04/2021.
The game is on again
MAHUSIANO YA BASHIRU, DIWANI NA MAJALIWA.

Kwa lugha ya kawaida, watatu hawa ni familia, ni ndugu walio na mahaba ya ndani kabisa baina yao. Undugu wao una historia ndefu, lakini kwa ufupi wake tuanzie katika kile kilichoitwa “MTANDAO” Ukatibu wa Bashiru uliratibiwa na mtandao chini ya ufadhili wa Athumani Diwani (DGIS), ukiwa na “malengo maalum”.

Mkataba wa Barabara njia nne kutoka Ubongo hadi Kibaha ni sehemu ya “uozo” uliokuwa katika mkakati. Na ikumbukwe kuwa Barabara hii Katibu wa CCM by then Dkt. Bashiru ambapo alipewa sehemu ya shilingi yaliyotokana na Ujenzi wa Barabara hii wenyewe wanasema ni 10%

Bashiru , baada ya kutia sahihi yake kwenye mkataba wa Ujenzi alitunukiwa kiwanja kikubwa tu kule Mbezi Beach, eneo ambalo ni mali ya kassimu Majaliwa ambacho ni Kiwanja Na. 936. Kiwanja hicho kinapakana na viwanja Na. 937 cha mfanyabiashara Hussein Ndama na Kiwanja Na. 938 cha Mama Mongela.

kampuni ya Dkt. Bashiru , inaporomosha majengo ya ghorofa kadhaa kwenye kiwanja hicho.

Watanzania bado wanayo kumbukumbu kuwa, Baada ya kifo cha Magufuli Akiwa hospital ya Mzena , mtu pekee aliyaaminiwa na familia na kukabishiwa jukumu la kuufuata mwili, kuutayarisha na Dkt Bashiru Ali. Hili linathibitisha kuwa mahusiano yao ni zaidi ya Undugu wa damu.

Miongoni mwa mikataba inayotajwa kuwa na harufu ya kifisadi ni ule wa Kiwanja Cha Ndege Chato ambacho kimepewa Kampuni ya Magufuli inayoitwa Mayanga Construction chini ya Usimamizi wa Bashiru akiwa katibu Mkuu ambaye tenda nyingi walipewa akiwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)

Bashiru Ali amenukuliwa mara kadhaa akiapa kwa MIUNGU yake yote kuwa atahakikisha kuwa anapambana na Samia , mapambano hayo ni sehemu ya muendelezo wa vita baina ya Haki na Batili, Ukweli na Uongo na Uzalendo dhidi ya Ufisadi.

Ni Wazi kuwa mjadala huu Bashiru ameutoa kwa msaada wa Majaliwa na Diwani Athumani hii ni Plans ya kuitikisa Serikali ya awamu ya sita kwa kipindi hiki, Bashiru anataka kutest kuyaoga maji kwa kuichallange Serikali ya SSH kwa kurejesha Kigenge chao.View attachment 2422452View attachment 2422454View attachment 2422456View attachment 2422457
Duh...!. Umenikumbusha mbali
Pl
 
Quote "Mayala amedai pia haoni njia ya Bashiru kufufuka tena kisiasa na ndiyo hivyo Mama Samia Suluhu ameshampoteza na Wana CCM wamefurahi mno." EOQ.

Hayo aliyasema Paskali wakati ule. Kwa sasa katika haya yaliyojitokeza jamaa ndo wamefurahi kupitia kiasi. Je, atakwepa kitanzi hiki ambacho kinaning'inia shingoni mwake. Tusubiri tuone.
 
Mayala amedai pia haoni njia ya Bashiru kufufuka tena kisiasa na ndiyo hivyo Mama Samia Suluhu ameshampoteza na Wana CCM wamefurahi mno.

Source: Radio DW Swahili, Leo mchana saa Saba, 01/04/2021.
Ni katika kukumbushana tuu!.
Kweli dunia inaenda kasi sana jamani. Toka juzi habari inayovuma sana kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ni juu ya uteuzi wa Dr Bashiru Ally kuwa Balozi na Katibu Mkuu Kiongozi (CS) Cha kushangaza Pasco Mayalla sijaona comment wala bandiko lake kutuletea uchambuzi na matarajio yake kama tulivyozoea.

Au Pasco kuna sehemu yupo anafanya kazi zinazomweka bize mpaka anashindwa kuandika?
Mkuu MKEHA , ni kweli wakati wa uteuzi nilikuwa likizo, ila wakati wa utumbuzi nilitoa uchambuzi, BBC, DW na VOA Ubunge wa Bashiru Ali, wachambuzi wanasemaje? | DW | 01.04.2021
Na kwa vile mimi ni muumini wa freedom of expression, kweli hili la sasa la Dr. Bashiru, nimempa ushauri ufuatao Dr. Bashiru, If you are a man of Principles, Hata Wakushukie vipi Stand Firm!, Don't Apologize!, Utaheshimika Zaidi na Zaidi!
P.
 
Msimubeze Pascal ndiye alimutabiri Marehemu John Joseph Pombe Magufuri kuwa Rais. Wana Jamii Forum tumesahau?
Mkuu Anania Stephen Byarugaba, sio hii tuu ya JPM, Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli, jee uliwahi kuiona hii ya Samia?,
Hii ni kauli umba ya kumuumbia mtu urais wa JMT.

na hili "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza
Angalia kwa makini hii kauli umba hapa iliumba nini?
Makamo wa Rais wa JMT, Mhe. Samia Suluhu Hassan anauzungumzia Muungano, kiukweli huyu Mama Samia anauzumguza vizuri muungano huku akiongea kwa heshima, taratibu, kwa utulivu na unyenyekevu, na anaongea vizuri mpaka raha, na kwa wale wenzangu na mimi wenye udhaifu na macho fulani, kiukweli Mwenyenzi Mungu amemjaalia macho mashaalah, huchoki kumsikiliza, utatamani aendelee tuu kuongea na kipindi kisiishe!.

Kwa hoja za muungano Mama Samia alizoshusha, ningekuwa ni uwezo wangu, ningeshauri October 2020, Mama Samia ndiye ampokee Dr. Shein kule Zanzibar, ili 2025, aje ampokee Magufuli, maana kwa maoni yangu, kwa uongeaji huu, huyu mama ndiye Mzanzibari pekee anayekubalika kuweza kuchagulika kuwa rais wa JMT kutokea Zanzibar, vinginevyo Wazanzibari wausahau kabisa urais wa Muungano, wao mwisho wao ni umakamo wa rais pekee.

Kwa hoja kama hizi za huyu mama Samia, kama age sio issue sana, si huyu mama atatufaa sana 2025 au tuwashauri kwa vile Magufuli analamika sana kuhusu urais, mara ni mateso, mara ni kazi ngumu, mara ni mzigo mzito, tumshauri rais Magufuli, kwa vile Samia anatosha sana, hivyo tumpunguzie mateso, hana haja ya kuendelea na mateso, mzigo mzito na kazi ngumu ya urais, na hata kama ni wale tausi au wanyama wa Magogoni, au yale majabali ya Chamwino, tutamjengea Chato na kumuomba bora apumzike tuu mapema, na kumpisha Mama Samia ndio amalizie ngwe yake iliyobakia?.

Paskali
Hapa kuna mtu ameumbiwa urais wa JMT kwa kauli tuu, na hapa unaweza kuzishuhudia kauli umba mbalimbali

Kubwa kuliko, ni hii ya rais wa JMT 2025,
Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke, anza kuiweka hii akiba, 2025 tutakumbushana na tutaheshimiana!.

P
 
Mwana JF nguli, Akihojiwa Radio DW Pascal Mayala, amemchambua Dr Bashiru. Amesema Dr Bashiru kapata ajali kubwa sana kisiasa na hatoinuka tena. Pia kadai Magufuli amiini usiamini alikuwa akimwandaa Dr Bashiru kuwa Rais 2025.

Mayala amedai Dr Bashiru aliyeibukia kuwa Katibu Mkuu wa CCM baada ya kuhakiki Mali za chama hicho alichukiwa mno kutokana na style yake ya uongozi.

Amesema amekinyoosha mno chama hadi kupitiliza na kusababisha kuchukiwa mno kuliko Katibu Mkuu yeyote katika Historia ya CCM. Pia amedai Dr Bashiru ni mjamaa mno au Mnyerere na Marehemu Magufuli alimkubali na kumpenda Sana na alipanga kumuachia Urais 2025.

Mayala amedai pia haoni njia ya Bashiru kufufuka tena kisiasa na ndiyo hivyo Mama Samia Suluhu ameshampoteza na Wana CCM wamefurahi mno.

Amesema kwa uhakika utawala wa Mama Samia Suluhu atakuwa Rais mzuri Sana kuliko Rais Magufuli.

Source: Radio DW Swahili, Leo mchana saa Saba, 01/04/2021.
Pascal bado anaamini Tanzania ina chama kimoja cha siasa na itaendelea kuwa hivyo chini ya udikiteta wa CCM hivyo Bashiru hawezi akaibukia kwingine! Kwa maoni ya Pascal mama Samia tayari amepitishwa kuwa rais 2025 na CCM imekwisha sema imeandaliwa fomu moja tu ya mgombea urais, je, tutashuhudia tena watu wakitoweka?
 
Pascal bado anaamini Tanzania ina chama kimoja cha siasa
This is very true, Tanzania tuna chama kimoja tuu cha siasa ambacho ni capable na credible kwa huku Bara, ila Zanzibar kuna vyama wiwili, CCM na ACT-Wazalendo
CCM sio tu ni chama tawala, bali pia ni chama Dola!
na itaendelea kuwa hivyo chini ya CCM
This is also true, CCM itatawala milele!. Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!.
hivyo Bashiru hawezi akaibukia kwingine!
This is true kwasababu hakuna kungine!. NB. Japo Dr. Bashiru ni political scientist, huyu sio politician, huyu ni a technocrat!.
Kwa maoni ya Pascal mama Samia tayari amepitishwa kuwa rais 2025
Sii kweli, nimesema naunga mkono 2025 twende na mwanamke, ila sio lazima Samia!
Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye! ila pia kuna hii sauti Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
CCM imekwisha sema imeandaliwa fomu moja tu ya mgombea urais
True, huu ndio utaratibu wa CCM kwa urais mid term, inatolewa fomu moja tuu kwa incumbent
je, tutashuhudia tena watu wakitoweka?
Kwa vile walikuwa wanatoweshwa na wasiojulikana, hili siwezi kulisemea!.
P
 
"Aliandaliwa kuwa Rais", inazidi kuthibitika sio wananchi wanaoamua nani awe Rais wa hii nchi, ni kikundi kidogo cha watu ndio kinatuchagulia Rais wamtakaye.
Wakati mwingine huwa najiuliza kama ni sahihi kuwaachia wananchi waamue wenyewe mambo mazito kama kumchagua rais wa nchi.

Siamini kwamba vijana kama wale waliodeki barabara lowasa apite kwenye njia safi wanastahili kuwa wapigakura.

Kanisa katoliki wangekuwa na utaratibu wa kila muumini wao kuwa na haki kumchagua papa, kungekuwa vurugu zisizokwisha huko.
 
This is very true, Tanzania tuna chama kimoja tuu cha siasa ambacho ni capable na credible kwa huku Bara, ila Zanzibar kuna vyama wiwili, CCM na ACT-Wazalendo
CCM sio tu ni chama tawala, bali pia ni chama Dola!

This is also true, CCM itatawala milele!. Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!.

This is true kwasababu hakuna kungine!. NB. Japo Dr. Bashiru ni political scientist, huyu sio politician, huyu ni a technocrat!.

Sii kweli, nimesema naunga mkono 2025 twende na mwanamke, ila sio lazima Samia!
Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye! ila pia kuna hii sauti Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke

True, huu ndio utaratibu wa CCM kwa urais mid term, inatolewa fomu moja tuu kwa incumbent

Kwa vile walikuwa wanatoweshwa na wasiojulikana, hili siwezi kulisemea!.
P
Asante kwa kuhariri nilichokiandika kwa kuiruka sifa ya u great dictator, kutoamini haki ya anayetaka apate haki. Nilizaliwa nikiwa British subject chini ya mfalme wa uingereza baadae malkia mpaka tunapata Uhuru nikatelekezwa Tanganyika nikiwa ninamatumaini makubwa japo sikuteswa na malkia. TAA(TANU) na vyama vingine vya kina Mtemvu havikusurubiwa na malkia kama unavyotaka wewe vilivyopo visurubiwe! Malkia alivipa haki ya kujieleza mbele ya wananchi wake na akatupa Uhuru japo hakuwa mtawala wetu kwani tulikuwa chini ya Legue of Nations baadae UNO.
Umehariri sifa moja kubwa pendwa kwa sababu inakutia doa japo unaipenda sana, ingekuwa vizuri nayo ungeichambua kama ulivyochambua mengine. Hebu fikiria dunia ingekuwa vipi endapo watu wote tungekuwa na fikira moja ya ndiyo kwa kila jambo, nadhani tusingependa kuishi.
Nakusihi tu jutia mateso waliyoyapitia usiowatambua japo si ndugu zako ila kwenye maziko yako watakuwepo nawe hautawafukuza.
 
Pascal bado anaamini Tanzania ina chama kimoja cha siasa na itaendelea kuwa hivyo chini ya udikiteta wa CCM hivyo Bashiru hawezi akaibukia kwingine! Kwa maoni ya Pascal mama Samia tayari amepitishwa kuwa rais 2025 na CCM imekwisha sema imeandaliwa fomu moja tu ya mgombea urais, je, tutashuhudia tena watu wakitoweka?
Ila Siasa mapito, leo Bashiru anaonekana adui
 
Mwana JF nguli, Akihojiwa Radio DW Pascal Mayala, amemchambua Dr Bashiru. Amesema Dr Bashiru kapata ajali kubwa sana kisiasa na hatoinuka tena. Pia kadai Magufuli amiini usiamini alikuwa akimwandaa Dr Bashiru kuwa Rais 2025.

Mayala amedai Dr Bashiru aliyeibukia kuwa Katibu Mkuu wa CCM baada ya kuhakiki Mali za chama hicho alichukiwa mno kutokana na style yake ya uongozi.

Amesema amekinyoosha mno chama hadi kupitiliza na kusababisha kuchukiwa mno kuliko Katibu Mkuu yeyote katika Historia ya CCM. Pia amedai Dr Bashiru ni mjamaa mno au Mnyerere na Marehemu Magufuli alimkubali na kumpenda Sana na alipanga kumuachia Urais 2025.

Mayala amedai pia haoni njia ya Bashiru kufufuka tena kisiasa na ndiyo hivyo Mama Samia Suluhu ameshampoteza na Wana CCM wamefurahi mno.

Amesema kwa uhakika utawala wa Mama Samia Suluhu atakuwa Rais mzuri Sana kuliko Rais Magufuli.

Source: Radio DW Swahili, Leo mchana saa Saba, 01/04/2021.
Nikuakishishie Freed Freed, ikitokea leo wewe ni Rais wa nchi hii, huyu ndugu Paskali atadai wewe ni Rais bora kuliko Rais yoyote aliyewai kutokea Tanzania. Imekuwa kawaida yake kusifia hadi kupitiliza kwa yeyote anaekuwa madarakani.
 
Na ndivyo itakavyokuwa aaaaaahhhhhhaaaaahhhh
 
Back
Top Bottom