Pascal Mayalla amchambua Dkt. Bashiru, adai aliandaliwa kuwa Rais 2025

Pascal Mayalla amchambua Dkt. Bashiru, adai aliandaliwa kuwa Rais 2025

Bashiru amekitendea haki Sana Chama cha mapinduzi na kukitoa katika meno ya wenye meno!! Ila sina uhakika yeye mwenyewe alikuwa safi kiasi gani? Tatizo liko hapo! Ila huwezi kujua mahesabu ya mama! Kwa kuchaguliwa kuwa mbunge, kutokea hapo anaweza kupaishwa nafasi yoyote hata kuwa PM Nani ajuaye? Ila wapigaji ndani ya Chama hawana hamu naye!
Mpaka hapo inaonekana somo la civics hukulizingatia,yaan Bashiru aje apewe u PM,kwa katiba ipi,? PM Ni lazima atokane na mbunge wa kuchaguliwa jimboni si kuteuliwa
 
Mayalla sio wa kumuanini sana ! Hapo kasema Bi Mkubwa atakua rais mzuri kuliko jiwe wakati aliwahi kusema jiwe kwa aliyoyafanya hahitaji uchaguzi atawale milele(Wamejibiwa March 9 Ombi lao)

Huyu huyu Mayalla nilishangaa alipokiri mitandao haikufungwa uchafuzi mkuu wa 2020! Pale ndio niliondoa imani na kuamini why huyu mtu aliambulia kura 1 kwenye uombaji ridhaa kwenda kugonga meza Dodoma!

Yote kwa yote naamini Paskali alijivua akili zake kutokana na aliyoyapitia baada ya kumuuliza Jiwe swali lile!sasa nikuombe Paskali urejee kwenye akili zako za zamani
 
Pascal alivyopotea jukwaani kumbe alikuwa mwandishi wa habari maalum wa mwendazake siyo??!
Wakijadiliana future plans za nchi hii?? 😂

Everyday is Saturday................................😎
 
Kwa hiyo unataka kutuaminisha kuwa mamlaka ya akina Gnassinbé Eyadema, Francisco Nguema, Teodoro Nguema, Charles Taylor, Siad Barre na Idi Amin Dada yalitoka kwa Mungu?
Exactly, kama unaamini biblia bila shaka utakuwa unafahamiana na kisa cha Nebukadneza alivyonyenyekezwa na Mungu kwa kugeuzwa ufahamu wa kibinadamu na kupewa wa mnyama hata akaenda kuishi porini kwa muda wa miaka saba.

Daniel 4:25
ya kuwa utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni, nawe utalazimishwa kula majani kama ng’ombe, nawe utatiwa maji kwa umande wa mbinguni, na nyakati saba zitapita juu yako; hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa yeye amtakaye, awaye yote.
(Msisitizo ni wa kwangu)
 
Mwana JF nguli, Akihojiwa Radio DW Pascal Mayala, amemchambua Dr Bashiru. Amesema Dr Bashiru kapata ajali kubwa sana kisiasa na hatoinuka tena. Pia kadai Magufuli amiini usiamini alikuwa akimwandaa Dr Bashiru kuwa Rais 2025.

Mayala amedai Dr Bashiru aliyeibukia kuwa Katibu Mkuu wa CCM baada ya kuhakiki Mali za chama hicho alichukiwa mno kutokana na style yake ya uongozi.

Amesema amekinyoosha mno chama hadi kupitiliza na kusababisha kuchukiwa mno kuliko Katibu Mkuu yeyote katika Historia ya CCM. Pia amedai Dr Bashiru ni mjamaa mno au Mnyerere na Marehemu Magufuli alimkubali na kumpenda Sana na alipanga kumuachia Urais 2025.

Mayala amedai pia haoni njia ya Bashiru kufufuka tena kisiasa na ndiyo hivyo Mama Samia Suluhu ameshampoteza na Wana CCM wamefurahi mno.

Amesema kwa uhakika utawala wa Mama Samia Suluhu atakuwa Rais mzuri Sana kuliko Rais Magufuli.

Source: Radio DW Swahili, Leo mchana saa Saba, 01/04/2021.
Wanafiki nyie na DW yenu..............
 
Kuna wanaccm wana piga talalila eti mama anaendeleza pale alipoishia Magu, sasa mbona aliyemuandaa hapewi ushirikiano? Aliyempenda hawampendi? Alivyokuwa anakusanya kodi mnasema (kama wapinzani walivyosema) hakutumia akili bali mabavu?
CCM acheni unafiki, Magufuli alichukiwa nanyi kwa siri bali wapinzani walikuwa wanamkosoa kikatiba!
 
Siku zote nilikua natafuta sababu ya kwa nini watu hawamkubali kabisa. Sasa nimeipata. Kumbe ni "mjamaa " sana. Dah! Basi hata mimi nadelete kabisa. Ujamaa ni kosa dhidi ya utu na ubinaadamu. Unatakiwa upingwe kwa hali na Mali. Ujamaa ushindwe na ulegee! !
 
Ndiyo tumuulize, mwendazake alimuambia?? Au tuseme naye ana connection na jamaa yule wa twitter republic??

Everyday is Saturday............................... 😎
Pascal Mayalla atakuwa na connection sio bure. Pia Kuna mwana CCM aliwahi kuniambia kuhusu Dr Bashiru 2025. Uzi upo humu. Ila bahati haipotei hucheleweshwa. May be 2030 au hata 2040 uzeeni mwake.
 
Siku zote nilikua natafuta sababu ya kwa nini watu hawamkubali kabisa. Sasa nimeipata. Kumbe ni "mjamaa " sana. Dah! Basi hata mimi nadelete kabisa. Ujamaa ni kosa dhidi ya utu na ubinaadamu. Unatakiwa upingwe kwa hali na Mali. Ujamaa ushindwe na ulegee! !
Unaambiwa Dr Bashiru alichelewa Sana kununua simu zilipoingia na usomi wake wa shahada kipindi hicho. Pia alichelewa Sana kujiunga na social networks. Yeye kwa hayo ni technology za magharibi zilizojaa upotofu na unyonyaji wa hali ya juu.
 
Back
Top Bottom