Habari wana JF ,
Mwanahabari nguli Bw Pascal Mayala akiongea na Radio Dw ya Ujerumani mchana huu amekaririwa akisema anauhakika Marehem Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dr John Pombe Joseph Magufuli alimuaandaa kumkabidhi nchi mnamo mwaka 2025 aliyekua Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi na katibu mkuu kiongozi aliyetenguliwa uteuzi wake Na Rais Samia Hassan Suluhu ,ndugu Bashiru Ali Kakurwa ambapo ameapishwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
Kwenye maelezo yake amesikika akisema amepanda ngazi kwa haraka sana katika kipindi cha Dr Magufuli kwa itikadi yake ya Ujamaa ya Mwl Julius Nyerere ambayo ilimfurahisha Mteule wake Hayati Dr Magufuli .
Pia kupanda kwake kisiasa kulimtengenezea maadui ndani na nje ya Chama hivyo anasema kwa sasa itakua ngumu sana kurudi juu kisiasa kipindi hiki cha Rais Samia Hassan Suluhu.
Ni suala la kusubiri na kuona ... wakati ni shahidi mzuri !