Pascal Mayalla kutoka kuwa Mwandishi Nguli hadi Mtangazaji wa kawaida East Africa Radio inamaanisha nini katika Tasnia?

Pascal Mayalla kutoka kuwa Mwandishi Nguli hadi Mtangazaji wa kawaida East Africa Radio inamaanisha nini katika Tasnia?

Mayala najuwa utasoma ila mimi sikujui wala hunijui personal na wala sio muhimu ila kwa ukweli kabisa na naongea hili kwa dhati mjitahidi media kwa ujumla Tanzania na waandishi wetu wajenge uwezo na kuongea au kuuliza mambo katika upeo wa juu sio mambo ya kureport tu unachosikia bila kuchambua taarifa kwa haki na weledi. Na wala hapa sisemi jambo zuri ni kupinga serikali tu hapana mazuri yasemwe lakini yaulizwe yanayoweza kuboresha zaidi sijui kiswahili fasaha constructive criticism. Hata wapinzani waulizwe maswali magumu maana sisi tunawasema CCM lakini pia wapinzani wanatabia zileile mtu akiwauliza basi kishakuwa adui. Mimi sina utaalamu wa habari lakini naamini haya yanawezeka na hii itachangia nchi kwenda pazuri. Media yoyote ichukue hoja upande na pia ichukue upande mwingine balance stories halafu watu watajuwa u ukweli ni upi kwa bahati mbaya news channel zote akiitwa mgeni basi unajuwa huyu wa upande huu, najuwa hili sio jambo la mtu mmoja lakini nyinyi na wengine wengi tu hili linawezekana bila kuwa na uadui wala msichukue side, kwenye hili wa Kenya wametuacha na tusiachwe zaidi ya hapa. Media zetu sio mtu anakurupuka tu anaita press watu wamejaa hakuna hoja yoyote kuna watu hawastahili kupata hata coverage lakini mambo ya msingi hawako. Sina solution ya moja kwa moja katika hili ila ningependa kuona free press bila uadui.
Tanzania haina Journalists usisumbuke.
 
Kwanza nampongeza kupata hiyo nafasi, maana kwa ninvyofaham mfumo wetu wa kiserikali/kisiasa ukiwa (kwenye tasnia) yoyote ukajifanya kuinanga na kuitweta serikali na kuonekana you're threat for future basi utasaga meno mpaka utakapoondoka duniani.

👉🏾 Kama hayaja kukuta ndiyo unaweza kumponda huyu jamaa.
Muda wote alipokuwa Hewani leo EA Radio kazi yake ilikuwa ni Kukosoa tu W Watangazaji sasa kama anajiona ni Nguli kwanini asianzishe tu Chuo chake cha Uandishi wa Habari ili awafunde vizuri huko huko Darasani? Anaboa....!!
 
wanaziua wenyewe mkuu, siku hizi badala ya media kutafuta content, content zinawatafuta. yaan ukiwa na hela unaweza kabisa kununua kipindi redioni ili wakuhoji na ukachagua maswali ya kukuuliza.

nilisikitishwa sana na kipindi cha sabaya juzi pale clouds.
Nani atapoteza mda wake kufuatilia hizo media..
tusiisingizie technology ambayo ipo kila nchi lakini hatuoni anguko kubwa kama huku, waandishi na wamiliki wa media wamekosa ubunifu, uwezo na wanaua media kwa mikono yao wenyewe
Umeelezea Ukweli mtupu Ndugu. Heko.
 
Je, kwa hali hii ina maana Tasnia ya Habari nchini imekuwa Kimafanikio au imeshuka na sasa imeanza kupoteza Umuhimu nchini?

Binafsi kwa Hadhi ya Unguli wa Habari aliokuwa nao @Pascal Mayalla nilitegemea leo hii angekuwa anamiliki Chombo chake kikubwa sana cha Habari nchini Tanzania na siyo kuwa Mtangazaji Mchangiaji wa Kawaida mno EA Radio.

Mambo yanabadilika kila siku na katika kila nyanja hivyo ni lazima mtu ahakikishe kuwa kadiri Dunia na mambo yake yanapobadilka nae pia anaendana na mabadiliko hayo ama sivyo ataachwa nyuma!!!
Technology imebadilisha sana tasnia ya habari hivyo kama mwandishi hawezi kubadilika kuendana na mabadiliko hayo matokeo yake ni kubaki nyuma na broadsheets wakati wenzie wanakwenda na digital!! Huoni siku hizi wazee nao wanajikongoja na PODCASTS!!
 
Mtafutaji hakati tamaa, ajaribu kwa Mama, anaweza kuteuliwa lkn lazima awe na connecton/mtu wa kum connect na mama. Pascal Mayalla . Mayala ulifika wakati ukawa huoni kasoro katika Jiwe, ukamsifia pale TBC1 mpaka ukawa kinyaa! Tulikushangaa sana......
 
Hata angeenda wapi mradi yuko kwenye kupata rizki its OK...pengine Huyo Abdala unayemsema sasa hivi anashika pesa nyingi kuliko alipokuwa mtangazaji jina na huku pesa hakuna haina maana yoyote.....pigana Pascal bills zinakungoja.
 
Waandishi wengi wa habari Tanzania ni vilaza haswa. Hawajui kutamka maneno mengi ya kiswahili kwa ufasaha na na hawajui kufanya uchambuzi ukiacha ule wa mpira. Wengi wako kikomedi komedi tu.
Muda wote alipokuwa Hewani leo EA Radio kazi yake ilikuwa ni Kukosoa tu W Watangazaji sasa kama anajiona ni Nguli kwanini asianzishe tu Chuo chake cha Uandishi wa Habari ili awafunde vizuri huko huko Darasani? Anaboa....!!
 
Back
Top Bottom