Pascal Mayalla ndiye aliyemchongea Erick Kabendera kwa dola

Pascal Mayalla ndiye aliyemchongea Erick Kabendera kwa dola

Niombe wasomaji wangu muelewe kuwa sina nia mbaya ninapojaribu kuja na uchambuzi wa namna hii. Lengo langu ni kuoneshana kuwa nchi yetu iko hatarini hasa pale taaluma moja ambayo Taifa linawategemea wanaposigana katika jamii nani anayeumia zaidi!

Nakumbuka siku za hivi karibuni gazeti la the Economist lilikuja na habari ambazo Mkuu Pascal aliziita kuwa ni habari za uongo dhidi ya Rais wetu wa Tanzania.

Gazeti ilo liliwahi kuja na habari kuwa "Rais wa Tanzania hapendi kukosolewa"

Gazeti ilo baada ya kuchapishwa Pascal Mayalla alikuja na bandiko la kupinga habari ile huku akionesha jinsi ambavyo sio kweli Rais wetu anapenda kukosolewa.

Alikwenda mbali zaidi akamnukuu Rais wetu kuwa aliwahi kuwaambia wanahabari kuwa yeye anapenda kukosolewe ila akosolewe kwa Staha na kwa hoja.

Pascal Mayalla kwenye andiko lake anatolea mfano kuwa yeye Pascal Mayalla ni moja ya wanahabari ambao waliwahi kumkosoa Rais na Rais alikubali kukosolewa kwa kumjibu huku akimtania.

HOJA.

Kwanza lazma watu mjue kuwa andiko la Pascal kupinga habari ya the Economist ndio iliyoamsha watu na kuanza kufuatilia ni nani na yuko wapi anae ripoti habari hizo katika gazeti la the Economist?

Hapa naomba nieleweke,hata watumishi idara nyeti walianza kufatilia gazeti ilo baada ya kusoma bandiko la Pascal Mayalla hapa JF, na ndipo wakaja kugundua kuwa kumbe mwandishi wa habari zile na nyeti kupitia gazeti lile ni ndugu yetu Erick Kabendera.

Kwanini walifuatilia,kiukweli kilichoandikwa na mwandishi huyo wa habari kilikuwa na ukweli wa 100%ingawa huyu Ndugu Mayalla alikipinga kwa lengo la kujipendekeza kwa msukuma mwemzake.

Je, Pascal Mayalla alijua tangu awali kuwa Kabendera ndie anayeandika habari nyeti na kuziripoti The Economist na alishindwa kumuita kama mdogo wake na kumpa onyo?

Kimsingi kifungo cha Kabendera nadhani ni furaha kwa Mayalla kwani alimjua tangu awali na alishindwa kabisa kumuita na kumuonya ingawa wote wanatoka kanda ya ziwa.

Je, Pascal alijua Erick akifungwa tegemezi wake watalia na kusaga meno na wengine watajitokeza mitandaoni wakimlilia kwa kukosa hata fedha ya kununua Dawa?

Nadhani yote aliyajua ndio maana tangu Kabendera awekwe korokoloni hajawahi jitokeza popote kulaani kukamatwa kwa kijana huyu zaidi inasemekana ndio kwanza anatafuta makala zote zilizoandikwa huko nyuma na kuzisoma na kuzifafanua kwa vijana wa idara nyeti ili kijana azidi kubanwa.

Andiko la Mayalla dhidi ya kumtetea ndugu yake liko hapa JF linaudhi linaumiza kwani humo ndani anawataja wakosoaji wakubwa wa nchi hii ambao leo hii wamegeuziwa rangi ya unga wa ndere wao wanaita unga mweupe sasa huku wakila kuku kwa mirija.

Nasisitiza waandishi wa habari mtengeni Mayalla na waandishi wote wenye vinasaba vya ukabila na wanaoshindwa kusimamia taaluma badala yake wanaishia kujipendekeza kwa kuhofia uhai wao.

Natoa rai kwa Serikali ya Jamhuri kumwachia huru Kabendera. Tusipomdai kwa kiswahili tutawataka kwa kilugha, na hapo ndipo tutakapozuia kiongozi yeyote kuingia mkoa wa Kagera mpaka "omwana weitu mumutaishure.""

Dah...sijasoma andiko hili mpaka mwisho....Lakini naweza kusema kuwa Ndugu yetu Pascchal Mayala alitumia uhuru wa kutoa maoni kwa kulipinga hilo gazeti la Economist kwa article yao dhidi ya JPM kama ambavyo huyo anayeitwa sijui Kabendera alivyotumia kalamu yake akidai ni uhuru wa kutoa maoni kwa kumshutumu vikali Rais wetu JPM...Yaani huyo anayeitwa Kabendera alisambaza habari kwa wazungu akimshambulia Rais wetu...
 
Nimekuelewa
Hahaha asante best, ila kuna watu humu wanashabikia, wakipata breaking news kwamba Pascal Mayalla kauwawa, hao hao watakuja kusikitika humu.
Huu sio utani mzuri kabisa, mwenzenu kazi zake zinategemea public, kumu acuse kiasi hiki lazima uwe na,solid evidence, na sio vitu vya kufikirika.
Tupingane kwa hoja lakini hili linaweza kumuharibia mahusiano na watu, wakati kazi yake inategemea mahusiano na watu.
Nchi za wenzetu hili linaweza kumfunga mleta mada, kumsababishia Pascal Mayalla msongo wa mawazo, na psychological effects. Madhira ya hili yanaweza kupelekea mtu kujiua, kwasababu reputation yake kwa jamii imevurugwa. Tusishabikie haya kama hatuna uhakika nayo.
 
Tumwelewe Pasco,
Haandiki hapa kuitetea Serikali bali kutupa Habari. Someni vizuri maandiko ya Paskali, someni katikati ya mstari. Pasco hawezi mchoma Kabendera kamwe. Pasco alikuwa anataka tusome magazeti bila kuonekana anayaunga mkono. Ni falsafa
 
Kosa la Pascal silioni.Kabendera anashtakiwa na jamhuri.
Kabendera hakulazimishwa kuandika,wala hajahukumiwa bado ni tuhuma tu.
Naona mkuu umekuza mambo bure,mwombe Paskali msamaha.
Kosa la Erick ni kuandika makala au utakatishaji ?
 
Hahaha asante best, ila kuna watu humu wanashabikia, wakipata breaking news kwamba Pascal Mayalla kauwawa, hao hao watakuja kusikitika humu.
Huu sio utani mzuri kabisa, mwenzenu kazi zake zinategemea public, kumu acuse kiasi hiki lazima uwe na,solid evidence, na sio vitu vya kufikirika.
Tupingane kwa hoja lakini hili linaweza kumuharibia mahusiano na watu, wakati kazi yake inategemea mahusiano na watu.
Nchi za wenzetu hili linaweza kumfunga mleta mada, kumsababishia Pascal Mayalla msongo wa mawazo, na psychological effects. Madhira ya hili yanaweza kupelekea mtu kujiua, kwasababu reputation yake kwa jamii imevurugwa. Tusishabikie haya kama hatuna uhakika nayo.



Unaenda mbali sana..sema mtoa mada uwezo wake wa kupambanua mambo ni finyu sana!arudi shule
 
Unaenda mbali sana..sema mtoa mada uwezo wake wa kupambanua mambo ni finyu sana!arudi shule
Hahaha nilifikiria mbali sana best, huwa naona habari mtu kajinyonga kwa kukataliwa na mpenzi wake, nikajiuliza hivi msongo ukizidi hapa mtu anaweza kupata high blood pressure, hata kupelekea stroke.
Tuko tofauti bali wote tunaweza kupatwa na hayo.
Nimekuelewa.
 
1.Sio atengwe aliyekuwa anaandika habari bila kufuata weledi na kuishia kutukana rais.
2. Unaposema hakumuita na kumuonya ina maana ye hakuwa anaingia humu jf na kusoma maandiko ya pasco au alikuwa anapuuza?
3. Kisha ndugu zake na mama yake wanapataje shida wakati alikuwa na backup ya watu wengi wakiwemo kina zitto, waende wakahudumie familia. Au anzisheni kapu la kuchangia familia yake.
4. Unapozichokoza mamlaka na kujiona shujaa jua tu utalipia gharama siku moja, ni suala la muda. Hata tundu lissu kalipia gharama. Na akiendelea atalipia tena. Kifupi dunia ina kanuni zake. Hiyo ni principle ya dunia nzima.
5. Lakini pia watz tumshukuru sana Pasco kwa kufichua habari za huyu kinyamkera ambaye ni ant government. Watu hawa wapo nchi nyingi tu. Lakini nadhani habari yake kwisha. Mtapiga makelele baada ya muda mtasahau na maisha yataendelea. Pengine atapelekewa tu tarifa za kifo cha mama yake kwa kukosa dawa. Kina zitto nao baada ya muda watakuwa bize na mambo yao na kumsahau kabisa.
Ukweli mtupu huu bila unafiki japo mie pia ni mpinzani wa jiwe kwenye sera zake ila kichaka changu ni mtani wngu kokote nasema ili wazi wazi hata jamaa zangu wa St Peter msijisumbue na mie sie watani Bwana...
 
Pascal Mayalla Ni "Panya" smart sana ajuaye vyema kung'ata huku akipuliza.

Binafsi naheshimu uamuzi wake wakuzileta humu JF Makala Zile za lile Jarida kwa minajili kwamba alikuwa akimtetea Mkulu dhidi ya aliouita "Uongo na Matusi Yao kwa Mh. Rais" ingawa kwa hakika alikuwa ndio anafanya jukumu la kusambaza articles husika kwani kupitia Yeye wapo Wana JF wengi ndio walikua wanasoma hizo articles, at the same time he exaggerated a lot.
Kwa hili nakuunga mkono asilimia mia...
 
Hahaha nilifikiria mbali sana best, huwa naona habari mtu kajinyonga kwa kukataliwa na mpenzi wake, nikajiuliza hivi msongo ukizidi hapa mtu anaweza kupata high blood pressure, hata kupelekea stroke.
Tuko tofauti bali wote tunawezakupewa, na hayo.
Nimekuelewa.


Paskali hawez pata stroke kwa mada za kitoto kama hizi! kwanza huko anacheka..amefikisha ujumbe kwa hadhira vzr sana tumeanza kukanyagana
 
Kisa yuko kinyume na unachotaka aandike. Kwanza 96% sijui Kama IQ yako inamwelewaga Mayalla. Ndo mtu anayejielewa na yuko huru kama mwandishi. Ukiona mwandishi anaandika ubaya Wa CDM tu Au ubaya Wa CCM tu basi huyo Sio mwandishi ni mwanachama Wa upande mmoja. Demokrasia na Maendeleo mnatuambia inasimamia pia uhuru Wa mtu kaniandika ukweli na pia kutoa maoni yake. Humu wote maandikia hisia za kijinga. Then mnakaa mnadhani vyama ndo vitawaletea Maendeleo. Majungu mwaka mzima. No job. Kwa aina ya maisha ya uvivu na majungu Hakuna Kiongozi atakayekuja kuwafaa huko. JPM anawatosha. Kawabana mnabaki kumtungia Mambo as if Yeye katibu wa nyumba kumi. So kama ukweli ndo unakubore my dear just Die.

Mkuu naona umetoa maana yako mpaka ukaona bora Ututusi, kwamba wote humu tunaandika hisia za kijinga! hapo nadhani ni kasoro ww tu ndio unaandika hisia za maana. Tutake radhi samahani.
 
Pascal huwa simuelewi huwa ana like hadi quote za kijinga huwa najua kazi yake ni kumark watu humu jf and then wanafuatiliwa Trust me. Ukiona Pascal kale comment kwako basi uwe makini sana ikiwezekana change ip zako the guy is so fukin dangerous Men.
 
Mleta mada ni mkanda na mkabila. Period
kabisa kabisa,na anajaribu kwa nguvu zote kumuhusisha Mayala na yanayompata,kaflag!.
kama ikiwq ni kweli mayala kasababisha bas ni mafanikio kwa jf kuws wanatusoma vzr na jf si ya wqpinzani au watawala ni jukwaa huru kila mtu ruksa povu liwe lq kijani ,blue ,jeupe au la chama lolote lile
 
Mshamba kaonekana na kundi kubwa la JKT nyumbani kwake...hao "migambo"hawawezi kukusaidia kitu mabeberu wakikutamani
 
Back
Top Bottom