Paschal Mayalla anaweza kuungana na wakongwe wenzake kama Dr. Slaa, Zitto, Mtatiro, Kitila Mkumbo na wengine kupoteza ushawishi ndani ya jukaa hili baada ya kundi maalum "Folks" wa Jamii forum kuweka mijadala ya kumpinga kama walivyompinga Zitto na ACT yake, Dr. Slaa, Kitila na wengine baada tu ya wao kukengeuka.
Paschal Mayalla anatuhumiwa kumchongea mwana habari mwenzake Erick ambaye kwa sasa hatima ya uhuru wake imeshikiliwa na DPP.
Kundi hili (folks) limekuja juu na kwa hakika ndani ya siku mbili tu tayari Paschal anatoa mkono wa kwaheri ndani ya ushawishi wa Jf.
Nini kitafuata baada ya hapo?
Paschal ategemee kukutana na kila aina ya kejeli na vijembe pale atakapoanzisha ama kuchangia mada yoyote ndani ya Jukwaa hili la siasa. Aidha kundi hili (Folks wa Jf) ambao hujipambanua waziwazi kuwaunga mkono wanaharakati wanaokabiliana na madhaifu ya serikali yoyote ile itakayokuwepo madarakani lina nguvu sana ndani na nje ya Jf. Kama kundi hili likiamua kukujadili kwa mrengo hasi humu Jf basi utachafuka hata nje ya Jf. Hiyo ndiyo karma ya kundi hili.
Ikumbukwe kuwa Rais Magufuli alipoingia tu madarakani alielekea kusambaratisha nguvu ya kundi hili lakini iliwachukua wadau miezi minne tu ya utawala wake kumfahamu kiundani na kundi hili mara moja lilirudi katika makali yake na ukawa mwanzo wa ubaya wa Rais Magufuli kuanza kuonekana.
Aidha kundi hili lina maono mapana kwani tuhuma zote walizoibua kihisia tu mfano za Zitto, Dr. Slaa, Rais Magufuli na wengine wengi baada ya muda huibuka na kuwa kweli.
Wapo wakongwe kama
barafu ambao wamejijengea heshima kubwa ndani ya kundi hili. Haitarajiwi kumuona mkongwe huyu akiondoka kwenye hisia nzuri za kundi hili ingawa kila kitu kinawezekana mathalan pale utakapoona tu kundi hili limeanza kuhisi kama walivyofanya kwa Paschali na sasa anakula jeuri yake.
Kundi hili ni ngumu sana kuja kumuweka mtu wao madarakani kutokana na hisia zao kali.
Nimtakie tu Paschali maisha mema mengine kabisa ndani ya Jf na awe tayari kupewa kila aina ya baya ila angalizo kwake ni kuwa kundi hili halijawahi kamwe kurejesha sawasawa heshima ya mtu aliyesaliti mawazo yao hata kama amerudi na kutubu kweli kweli mfano
Nape Nnauye ambaye bado anaambiwa "Anaongea vile kwakuwa kapokonywa tonge mdomoni"