Pascal Mayalla ndiye aliyemchongea Erick Kabendera kwa dola

Pascal Mayalla ndiye aliyemchongea Erick Kabendera kwa dola

Umesema kwanini Pascal Mayalla hakumuita na kumuonya,inamaana nawewe unakiri kwamba alikosea? Tz wengi tunapenda kusisitiza uhuru wa maoni ila hatupendi kusikiliza mawazo ya wengine wanayotoa
 
Hahaha Aiseee chalii yangu ndio nimerudi Ghetto sasa hivi. Juzi kati nilimkonyeza mmoja mbibi yeye hakuvaa kininja ni buibui tu akatabasamu na kutingishika kichwa
Kuwa makini mkuu, naskia nyie mnaoishi huko mnaitwa diyasipora na Membe mara atakapoapishwa 2020 eti nyie mtakuwa watu mhimu kwenye uchumi wetu, hakikisha unatunza hizo senti unazopata baada ya kazi ngumu ya box.
 
LA msingi hapo ni kuwa katika uandishi wake Ndg Kabendera hakuvunja sheria/kanuni yoyote katika kazi yake. Ndio maana hata hao polisi wanahanjahanja na mashitaka, kila siku wanaokoteza.
Siku hizi kujipendekeza ndio imekuwa mwendo wa wachumia tumbo, lakini hautodumu na mwisho wao utakujakuwa mbaya wa aibu. Atakapoondoka huyo mungu wao, wao watabaki na kovu/doa daima. Itabidi watafute pa kujificha kwani watasakwa ili walipe kwa uovu wao.

Wewe unaona alifanya sawa alivyoitukana nchi na rais wetu kipenzi kwa vipande vya shekeli kutoka kwa mabeberu!!?
 
Umesema kwanini Pascal Mayalla hakumuita na kumuonya,inamaana nawewe unakiri kwamba alikosea? Tz wengi tunapenda kusisitiza uhuru wa maoni ila hatupendi kusikiliza mawazo ya wengine wanayotoa

Kwanza kusema tu economist imemtukana Rais tayari ilikuwa virtually kaonywa kama mwandishi alikuwa mtanzania.
Pasco aliandika naamini alifikiri mwandishi ni beberu, nia ya Pasco ilikuwa kupambanisha na beberu kumbe beberu ikatokea kuwa ni Erick. Ha ha ha ha.

Mbona Pasco amekuwa akiwafuatilia Akasha na Barick na makala zao mbona hamusemi kawachongea akasha? Yani uuibe wewe ule wewe wakushike huko lawama apewe mwingine?
 
WABONGO MNABIDI MJIONGEZE KIDOGO PASCAL ANAJULIKANA KWA KUUMA NA KUPULIZA ANAPONDA KIDOGO ANASAWAZISHA KIDOGO KWA HALI ILIYOPO HAPA NCHINI SASA HIVI YA WAKOSOAJI WE UNAFIKIRI ANGEBAKI SALAMA NDO KWANZA ANAENDELEA KUPATA MADILI YA SERIKALI KUPITIA KAMPUNI YAKE YA UTANGAZAJI NANE NANE MPAKA DAKIKA HII MUSIBA HAJAMSHUKIA TU.WE UNAFIKIRI MUSIBA HAZIONI MADA ZAKE HUKU MWENZAO HUYO

Inabidi tujiongeze kidogo na lazima tupate muda wa kusumbua akili kuliko kufanya conclusion kwa kile alicholeta mleta uzi kuonekana ni sahihi kwa 100%.

Hivi Pascal ni mfanyakazi wa TRA au ofisi wa ofisi ya mwendesha mashtaka hadi tufikie anatuhumiwa alienda kumchonganisha Kabendera kwa hizo taasisi?
 
Kujaribu kumhusisha Pascal Mayalla na masaibu anayoyapata mwandishi Eric Kabendera ni utovu mkubwa wa uaminifu katika uchambuzi wa habari. Na hii ni sawa na ramli chonganishi!

Alichokifanya Pascal ni kuhabarisha jamii kuhusu makala za jarida la Economist zilizokuwa zinamkosoa Rais Magufuli na, of course, kuongeza maoni yake katika ile style yake ya uandishi kwa kutumia kejeli (sarcasm). Hakukuwa na tatizo hapo.

Tatizo kubwa hapa ni mleta mada kujaribu kutumia tukio la kushtakiwa kwa Kabendera kama silaha ya kumtisha Pascal ili asitoe maoni yake kwa uhuru. Hii haikubaliki hata kidogo. Uhuru wa kutoa maoni ni lazima uheshimiwe.

Nilisoma makala husika za Economist na zikuwa na ukosoaji wa kawaida tu ambao ulipaswa kutolewa majibu (rejoinder) na msemaji wa serikali katika jarida hilo hilo. Hii ingekuwa njia rahisi na ya kisayansi zaidi kwa upande wa serikali kuliko kumsaka na kumshtaki mwandishi wa makala.

Katika miaka ya 70 na 80, gazeti la serikali la Daily News lilikuwa na safu iliyokuwa inaitwa What They Say About Us ambayo ilikuwa makhsusi kwa ajili ya kuchapisha makala na stori kutoka vyombo vya habari vya nje zilizokuwa zinakosoa serikali ili wananchi wazisome.

Ingekuwa wakati huo, Daily News ingechapisha makala zote husika za jarida la Economist.

Hivyo kama serikali inatekeleza sera zake kikamilifu na kwa uaminifu, kamwe haiwezi kuogopa kukosolewa. Na ukosoaji ujibiwe kwa hoja. This is how politics works.
 
Huo ni unafki mkubwa, kwani Hilo gazeti la Economist linasomwa na Pascal mayalla pekee?!
Kwa nini umuandame mayalla wakat gazeti linasomwa na kila mtu?
Kwani kaflag hakujuwa kile alichokuwa anakiandika kwamba iko siku kitakuja kutoa majibu bila kujua yatakuwa hasi au chanya?
Nakubaliana na wewe mkuu.


Au kwanini awakumshauri aandike na MWANDISHI WETU badala ya ERICK KABENDERA
 
Hapa kuna maswali.

1. Kwanini MSAMBAZA UONGO Pascal hajashitakiwa. Yaani nikiandika uongonna wewe ukausambaza basi na wewe unakuwa umetenda kosa.

2. Ni ushahidi upi kwamba mwandishi wa huo UONGO alikiwa ni KABENDERA. Tunaomba kujua hili.

3. Kwanini kabendera hajashitakiwa kwa kosa la kisema aj kuandika UONGO
Pascal Mayalla Ni "Panya" smart sana ajuaye vyema kung'ata huku akipuliza.

Binafsi naheshimu uamuzi wake wakuzileta humu JF Makala Zile za lile Jarida kwa minajili kwamba alikuwa akimtetea Mkulu dhidi ya aliouita "Uongo na Matusi Yao kwa Mh. Rais" ingawa kwa hakika alikuwa ndio anafanya jukumu la kusambaza articles husika kwani kupitia Yeye wapo Wana JF wengi ndio walikua wanasoma hizo articles, at the same time he exaggerated a lot.
 
Erick
Kama alikuwa anaandika makala na hao economist wanamlipa pesa, hapo kosa ndo lilipo. Nikosa kufanya kazi nchi nyingine ukiwa nchi nyingine, hilo hata nchi yoyote ya kibeberu wanakutia nguvuni(tax invading)

Pia kama hao economist walitia mwamala wa aina yoyote hapo, lazima wamtie nguvuni, ya kufanya kazi na kukwepa kodi. Hapo huyu mwandishi atakuwa na hali ngumu sana, kama kwa namna yoyote alilipata mwamala kutoka nje.
 
Erick
Kama alikuwa anaandika makala na hao economist wanamlipa pesa, hapo kosa ndo lilipo. Nikosa kufanya kazi nchi nyingine ukiwa nchi nyingine, hilo hata nchi yoyote ya kibeberu wanakutia nguvuni(tax invading)

Pia kama hao economist walitia mwamala wa aina yoyote hapo, lazima wamtie nguvuni, ya kufanya kazi na kukwepa kodi. Hapo huyu mwandishi atakuwa na hali ngumu sana, kama kwa namna yoyote alilipata mwamala kutoka nje.

Tax invading!!!? Malkia njoo huku uone lugha yako inanajisiwa!
 
Upo sahihi mimi nilisoma na kuona Mwandishi Mtanzania na yupo Tanzania sikumuelewa pascal nilipita tuu nikajua anawapa watu taarifa kijanja sana...amefanikiwa ila alichokifanya sio kitu kizuri kabisa...
 
Huyo Mayala Pascal yn hadi kawaumiza ndo munalalamika wenye akili tuligundua anacho fanya humu jamii forum mulimushangilia bila kufikiria

Huyo Pascal ni mkabila mara elfu hana nia njema na waandishi wenzake
Hilo kuwa angemuonya limetoka wapi? Acheni ujinga yy nani?
Huyo pascal ni mutafuta fursa na ipo tayari

Yote aliyo kuwa anaandika yalichonganisha waanfishi wenzake na siyo kujenga

Jifunzeni kwa nyakati kwnn kipindi aanze kuandika
Mara eti jamaa kabadilika huyu Mayala kipimo cha kumuita Raisi kabadilika je alijua vipi kama sio munafiki huyu

Naunga mkono huyu jamaa atengewe hadi kabendera atoke nje.musicheke na joka hili linalo itwa Mayala
Ataanza mafumbo kwa mtu mwingine naye Atakamatwa soon
Mwenye kura nyama ya mtu haachi

Eti wasukuma si wakabila je anakipimo gani kujua kabila lipi lina ukabila na lipi halina ukabila, acha kugawa watanzania wewe mayalaNjaa itakuua

Lyamba lya mufipa
 
Pasco huwa anaandika kutokana na utashi wake,sioni kama ana kisa/ukabila/upendeleo kama walio wengi walivyo tafsiri maandiko yake.
Nimekuwa nikisoma maandiko yake mengi kwa kipindi kirefu sasa,namwona ndio style yake ya uandishi.
Humu ndani kila moja aheshimike kwa jinsi anavyo shiriki.
 
Niombe wasomaji wangu muelewe kuwa sina nia mbaya ninapojaribu kuja na uchambuzi wa namna hii. Lengo langu ni kuoneshana kuwa nchi yetu iko hatarini hasa pale taaluma moja ambayo Taifa linawategemea wanaposigana katika jamii nani anayeumia zaidi!

Nakumbuka siku za hivi karibuni gazeti la the Economist lilikuja na habari ambazo Mkuu Pascal aliziita kuwa ni habari za uongo dhidi ya Rais wetu wa Tanzania.

Gazeti ilo liliwahi kuja na habari kuwa "Rais wa Tanzania hapendi kukosolewa"

Gazeti ilo baada ya kuchapishwa Pascal Mayalla alikuja na bandiko la kupinga habari ile huku akionesha jinsi ambavyo sio kweli Rais wetu anapenda kukosolewa.

Alikwenda mbali zaidi akamnukuu Rais wetu kuwa aliwahi kuwaambia wanahabari kuwa yeye anapenda kukosolewe ila akosolewe kwa Staha na kwa hoja.

Pascal Mayalla kwenye andiko lake anatolea mfano kuwa yeye Pascal Mayalla ni moja ya wanahabari ambao waliwahi kumkosoa Rais na Rais alikubali kukosolewa kwa kumjibu huku akimtania.

HOJA.

Kwanza lazma watu mjue kuwa andiko la Pascal kupinga habari ya the Economist ndio iliyoamsha watu na kuanza kufuatilia ni nani na yuko wapi anae ripoti habari hizo katika gazeti la the Economist?

Hapa naomba nieleweke,hata watumishi idara nyeti walianza kufatilia gazeti ilo baada ya kusoma bandiko la Pascal Mayalla hapa JF, na ndipo wakaja kugundua kuwa kumbe mwandishi wa habari zile na nyeti kupitia gazeti lile ni ndugu yetu Erick Kabendera.

Kwanini walifuatilia,kiukweli kilichoandikwa na mwandishi huyo wa habari kilikuwa na ukweli wa 100%ingawa huyu Ndugu Mayalla alikipinga kwa lengo la kujipendekeza kwa msukuma mwemzake.

Je, Pascal Mayalla alijua tangu awali kuwa Kabendera ndie anayeandika habari nyeti na kuziripoti The Economist na alishindwa kumuita kama mdogo wake na kumpa onyo?

Kimsingi kifungo cha Kabendera nadhani ni furaha kwa Mayalla kwani alimjua tangu awali na alishindwa kabisa kumuita na kumuonya ingawa wote wanatoka kanda ya ziwa.

Je, Pascal alijua Erick akifungwa tegemezi wake watalia na kusaga meno na wengine watajitokeza mitandaoni wakimlilia kwa kukosa hata fedha ya kununua Dawa?

Nadhani yote aliyajua ndio maana tangu Kabendera awekwe korokoloni hajawahi jitokeza popote kulaani kukamatwa kwa kijana huyu zaidi inasemekana ndio kwanza anatafuta makala zote zilizoandikwa huko nyuma na kuzisoma na kuzifafanua kwa vijana wa idara nyeti ili kijana azidi kubanwa.

Andiko la Mayalla dhidi ya kumtetea ndugu yake liko hapa JF linaudhi linaumiza kwani humo ndani anawataja wakosoaji wakubwa wa nchi hii ambao leo hii wamegeuziwa rangi ya unga wa ndere wao wanaita unga mweupe sasa huku wakila kuku kwa mirija.

Nasisitiza waandishi wa habari mtengeni Mayalla na waandishi wote wenye vinasaba vya ukabila na wanaoshindwa kusimamia taaluma badala yake wanaishia kujipendekeza kwa kuhofia uhai wao.

Natoa rai kwa Serikali ya Jamhuri kumwachia huru Kabendera. Tusipomdai kwa kiswahili tutawataka kwa kilugha, na hapo ndipo tutakapozuia kiongozi yeyote kuingia mkoa wa Kagera mpaka "omwana weitu mumutaishure.""
Kumbe kumpa like zangu kote kumbe huyu ni ndumila kuwili?? Sishangai makala zake zote akiandika huwa anauma huku na huku.
 
Back
Top Bottom