Hahaha asante best, ila kuna watu humu wanashabikia, wakipata breaking news kwamba Pascal Mayalla kauwawa, hao hao watakuja kusikitika humu.
Huu sio utani mzuri kabisa, mwenzenu kazi zake zinategemea public, kumu acuse kiasi hiki lazima uwe na,solid evidence, na sio vitu vya kufikirika.
Tupingane kwa hoja lakini hili linaweza kumuharibia mahusiano na watu, wakati kazi yake inategemea mahusiano na watu.
Nchi za wenzetu hili linaweza kumfunga mleta mada, kumsababishia Pascal Mayalla msongo wa mawazo, na psychological effects. Madhira ya hili yanaweza kupelekea mtu kujiua, kwasababu reputation yake kwa jamii imevurugwa. Tusishabikie haya kama hatuna uhakika nayo.